Wakati fulani utakuja kutambua kwamba Ufunuo huu Mpya huko hapa ili kukupatia maisha mapya. Hauko hapa kuboresha maisha yako kwa kutia maana ya kiroho au kusamehe mawazo yako na imani na matendo yako ya zamani kupitia aina ya baraka kutoka juu.
Wakati fulani utakuja kutambua kwamba maisha unayoishi kwa kweli si sahihi kwako. Ni maisha ya kuafikiana. Na maafikiano yamekuwa makubwa mno. Kwa hakika yamekuwa makubwa mno. Ni maafikiano kuhusu vile unajiona, kuhusu vile unawaona wengine, kuhusu vile unaiona dunia. Na ingawa labda utapinzana na utambuzi huu, labda utaukana, na maafikiano mengine yatatafutwa, katika ukweli unawakilisha mwanzo wa matumaini makubwa kwako.
Kwa maana Mungu anajua kwamba bila Knowledge, akili zaidi ile imewekwa ndani yako, basi utaishi maisha ya maafikiano. Utatafuta maafikiano ili upate usalama, ili upate idhini, ili upate mali na faida. Utatafuta maafikiano ili uepuke kejeli au upinzani au hukumu au hata kukataliwa na jamii. Maafikiano yatapenya kila kitu, kuanzia imani yako, mitazamo yako, matarajio yako, shughuli yako, mipango yako, malengo yako. Na hii itaongezeka hadi pale ambapo kwa kweli utapoteza mawasiliano na asili yako.
Sasa umekuwa bidhaa ya jamii yako, bidhaa ya matarajio ya jamii, bidhaa ya mawazo yako binafsi, lakini umepoteza mawasiliano na asili yako ya undani na maana ya maisha yako. Na hata kama utafanikiwa na kufikia malengo yako, yatakuwa tupu, na furaha yako itakuwa ya muda mfupi, na itakuja kwa bei kubwa ya muda, nishati, juhudi, na Manufaa yake yatakuwa ya muda mfupi na itakukimbia.
Ugunduzi huu, ambao hukanwa na kuepukwa, ni mwanzo wa ahadi kubwa zaidi kwako. Usipingane nao. Usibishane nao. Usilalamike kuwa lazima ubadilishe maisha yako kwa kiasi kikubwa. Bila shaka lazima ubadilike! Kwa sababu unapewa maisha mpya – sio maisha bora kidogo kuliko ya zamani, si tu scenery mpya au nyuso mpya au aina mpya ya kusisimua. Haya sio mabadiliko ya mapambo. Haya ni mabadiliko ya umuhimu mkubwa sana na wa kina kikubwa cha maana kwako. Haya ni aina ya mabadiliko ya moyo wako uliokuwa unautamani kwa muda mrefu. Kwa muda mrefu umekuwa ukifanya kazi.
Na sasa inaonekana kuwa umeshindwa. Inaonekana umeshindwa kutimiza matarajio ya utamaduni wako. Hata labda unajisikia kuwa umeshindwa, kuwa hujatimiza malengo na matarajio ya familia yako, utamaduni wako na hata dini yako. Lakini katika maono ya kushindwa huku kuna ahadi ya mafanikio makubwa zaidi. Maisha yako ya zamani lazima ikushinde au lazima uiwache ndio uweze kuwa na nafasi mpya, ufunguzi huu katika maisha yako, huu ni mwanzo mpya.
Watu wengi wanataka tu kuwa na ufunuo kama kuwa ni aina fulani ya kitambi ya maisha yao ya zamani, kama kiroho ni kama kitoweo kwa udufu wa maisha yao. Ni kitu ambacho wataongeza. Sasa watakuwa watu wa kiroho na watafanya mambo ya kiroho na kufikiri mawazo ya kiroho na kufanya shughuli ambazo zitaonekena kuwa ni za kujenga na kuinua, Lakini tena, hii yote ni ya idhini. Hii yote ni ya kutafuta radhi zaidi, faraja zaidi, usalama zaidi. Motisha huu hauna tofauti na motisha wa kuongoza watu kutafuta mali na furaha na kuepuka maisha. Hii sio halisi. Na matokeo yake, hauzai matokeo halisi. Tunaongea kuhusu kitu tofauti sana hapa.
Na maisha haya mapya, bado haujui maana yake. Bado huwezi kujua vile itakavyokuwa kwa sababu ni mpya. Haitakuwa uvumbuzi wako. Haitakuwa kama ile umezoea. Kwa hivyo unaanza kugeuka kona hii polepole sana. Hata kama kuna matukio makubwa katika maisha yako yaliyokuleta katika ufahamu huu, sasa , safari ina hatua nyingi, ndio ikuruhusu uwe na muda wa kujifunza na kukabiliana na kupata msingi zaidi wa kujiamini ndiyo maisha yako iweze kuongozwa na kilicho ndani badala ya vilivyo nje, ndiyo upate kuwa mtu wa uwezo na nguvu na uadilifu, badala ya mtu ambaye ananakala maadili ya tamaduni yao.
Hapa lazima mambo mengi yafunzwe tena. Lazima yachunguzwe tena. Mawazo yako mengi yatabidi yachunguzwe tena. Dhana zako za imani ulizoimarisha zitabidi zichunguzwe na kwa baadhi ya kesi ingine itabidi ziwekwe kando. Hii ni bei ya uhuru. Hii ndiyo bei ile watu hulipia ndio wawe na fursa ya kuishi maisha makubwa, maisha halisi, maisha ambayo inalingana na Knowledge ndani yao, maisha yale yanatimiza hatima ile walitumawa duniani kukamilisha.
Mpaka hatua hii ifikwe, unaishi nusu ya maisha. Ndiyo, moyo wako unapiga, na damu inapitia mishipa ya damu yako, na akili yako ni inatoa taarifa ya dunia karibu nawe, na unaenda kwa miendo ya maisha yako, unatimiza majukumu na wajibu wa maisha yako na unajaribu kutafuta baadhi ya fomu ya furaha. Lakini uwepo huu ni tupu. Bado hujagundua maana halisi na thamani ya maisha yako. Hadi hatua hii, Knowledge, akili kubwa ile Mungu ameweka ndani yako ikuongoze na ikulinde, itajaribu kuwalinda dhidi ya madhara, itajaribu kukushika na kukushikilia ili usifanye makosa makubwa na ya muda mrefu na kujitolea kwa ahadi ambazo zitakuwa katika upinzani na uwezo wako wa kugundua na kuishi maisha makubwa katika siku zijazo.
Hapa katika hatua hii ya kwanza Knowledge itaonekana latent ndani yako, lakini kwa kweli bado inajaribu kukuweka nje ya taabu na kuzuia uitolee maisha yako kwa wengine au kwa hali au mahali, kwa watu, kuweka maisha yako iwe wazi. Watu wengi bila shaka wako katika hatua hii ya kwanza. Uibuka bado haujatokea kwao. Wakati utatokea, na jinsi utatokea na hata kama utatokea ni kitu wewe haujui. Ni fumbo.
Unaweza kuona, kabla ya uibuka huu, kwa kweli unajenga msingi wa kuwa mtu anayeweza kuishi duniani. Unajenga stadi za maisha. Unahisi raha na maumivu ya dunia hii. Unatafuta radhi na unaepuka maumivu na kupata yale yanayokata tamaa njiani. Maandalizi haya ya mapema yanaweza kuwa muhimu sana kwa kile ambacho unachoweza kukitambua, kukikamilisha na kushirikisha na wengine katika siku zijazo. Hata makosa yale ya ujinga zaidi utayofanya katika hatua hii ya mwanzo yanaweza kuwa muhimu sana katika kukupatia hekima, kukufundisha yaliyo ya kweli, kuthamani yale ya kweli, kukusaidia uweze kutambua kile kinachonekana ni kizuri kutoka kile kilicho kizuri, kukusaidia kutambua kile kilicho kizuri kutokana na kile tu kinaonekana ni kizuri, kukusaidia kutambua mwelekeo wako halisi kutokana na impulses zinazowakilisha udhaifu wako na ukosefu wa usalama.
Pengine katika hatua hii ya kwanza utahisi kuna uwepo unakuangalia mara kwa mara. Utahisi uwepo umo nawe. Na utadhani mara kwa mara kuwa kuna kitu kikubwa unafaa kukifanya katika maisha, lakini utambuzi bado haujatokea. Bado haujateketeza msingi wako. Ni kitu tu unakifikiri katika eleo la akili yako. Bado haujapenya moyo wako.
Kushindwa kwako na kukata tamaa hapa itashikilia ahadi kubwa kwako. Kukata tamma katika nafsi yako na wengine na katika furaha kubwa ambayo umelipa bei kubwa, kweli, hii ita banar njia kwa utambuzi huu. Na utambuzi huu hautadumu wakati mfupi. Itakuwa ni kitu ambacho kitabadilisha mwelekeo wa maisha yako, na hutaelewa kilichotokea kwako au asili na dhamira ya mabadiliko ya mpaka usafiri katika hatua ya pili ya safari yako.
Miongozo ya kuishi yatayotolewa hapa yanahusiana na hatua hii ya pili ya safari ya maisha yako. Hayahusiki na watu ambao hawajavuka kizingiti hiki kikubwa, ambao hawajafarisi hatua hii ya kugeuka. Kwao yataonekana kuwa ya manufaa lakini ya utata. Yataonekana ni kama yatwarudisha watu nyuma. Yatakuwa ni changamoto kwa mawazo yao ya uhuru. Yataonekana yanahitaji juhudi kubwa na wajibu kwa sababu hawako tayari kufanya juhudi hii au kuchukua jukumu hili. Bado wanajaribu kupata kutoka kwa maisha kile wanachotaka, zaidi ya mahitaji yao ya msingi. Wanajaribu kupata kutoka kwa maisha wanachotaka. Hawatambui kwamba walitumwa duniani kwa dhamira. Hawana kumbukumbu ya Nyumba yao ya Kale, kwa hivyo wanafikiri maisha haya ndiyo muhimu sana, ni kila kitu. Wanataka kuishi kwa muda, kwa wenyewe. Kwa hivyo mtu huanza kupata baada ya kizingiti hiki kikubwa uelewa tofauti. Na miongozo ya ya kuishi hapa sio tu ya kusaidia lakini ni muhimu kwa mafanikio.
Matakwa ya kwanza ni kukubali mabadiliko makubwa yanayotokea na kuwacha maelezo yawe wazi. Hutaweza kuwa na uwezo wa kuelewa. Akili yako inajua tu maisha yako ya hapo awali na ya zamani. Haiwezi kuakaunti linalojitokeza kwako, na impulses ambazo unahisi, na mwelekeo ambao polepole unaojitokeza ndani yako. Akili yako itajaribu lakini itashindwa katika kufahamu maana ya hii.
Baadhi ya watu hujaribu kurudi nyuma hapa. Wanataka kurudia kile walidhani kiliwapa hali ya usalama na utulivu na uhakika wa kibinafsi, lakini kwa bahati mbaya wameenda mbali sana sasa, majaribio hayo yataonekana kuwa tupu, yatawarudisha tu kwa maisha yao ya zamani iliyopatikana kuwa inakosa utimizo – inakukosa dhamira, maana na thamani. Sasa wanajiingiza katika safari ya aina mpya, na hawawezi kuifafanua.
Kwa hiyo, ruhusu mabadiliko hayo yatokee. Usijaribu kuyafafanua. Usitumie hata mawazo kutoka tamaduni zengine za kiroho kujaribu kuyafafanua. Ruhusu yawe ni ya fumbo, kwa kuwa kwako yatakuwa ni ya fumbo. Fumbo imo zaidi ya eneo la akili. Iheshimu. Ikubali. Fumbo sasa imeanza kujitokeza katika maisha yako, ambapo hapo awali ilikuwa imefungwa. Hapo awali, hapakuwa na mahali katika maisha yako ijitokeze, ikuongoze, ikubariki na ikukuandae. Sasa fumbo zimeanza kujitokeza. Basi wacha ijitokeze.
Utachanganyikiwa kuhusu kile unafaa kukifanya kuhusu mahusiano yako na watu, kimsingi, na pili, uhusiano wako na pale unapoishi, kazi unayofanya, shughuli zako, hobbies zako, maslahi yako na kadhalika. Wacha uchanganikio huu uishi. Ni wa afya. Ni wa kawaida. Ni sehemu ya mpito, unajenga daraja ya maisha mapya. Bado huishi maisha mapya kikamilifu. Unajenga daraja. Uko katika kipindi cha mpito. Mabadiliko huchanganisha kwa sababu unasonga kutoka uelewa mmoja hadi mwingine, kutoka kwa ufarisi mmoja wa maisha hadi ufarisi mwengine wa maisha. Mabadiliko ya maanisha kwamba huwezi kurudi nyuma, na hujaenda mbali kutosha ili ufike mbele, kwa hivyo lazima uwe juu ya daraja hii, kupitia mabadiliko haya.
Wacha mustakabali uwe wazi. Weka kando mipango zaidi ya yale lazima uyafanye ili uweze kudumisha maisha yako duniani. Hapa lazima uwe na imani kwamba uhakika utakuja, na uhakika utakuja utakapoona uko tayari kusonga mbele na uko tayari kusonga mbele katika wilaya mpya. Lakini ukisita, basi, uhakika hautakuja. Ukijadiliana na kujaribu kufanya kazi nje ya mpango ili uweze kuweka kitu kutoka maisha yako ya awali, uhakika hautakuja. Uhakika hautakuja kwa sababu bado hujageuka hiyo kona. Ni kama jibu limo upande wa mlima, na lazima uzunguke ulima huo ndio uupate.
Hii inachanganya akili, lakini sasa akili lazima itumikie nguvu kubwa ndani yako, nguvu ile Mungu ameweka ndani yako ikuongoze na ikubariki na ikuandae kwa maisha haya makubwa. Bado lazima uwajibike kwa kile unachofanya na kile unachotumikia, kwa kile utajitolea katika maisha, katika jinsi ya unataumia muda na nguvu yako na kadhalika, lakini kuna kitu kikubwa kinachosonga ndani yako sasa.
Halafu, usiende kuwaambia marafiki wako wote na familia, kwa kuwa hawatafahamu. Isipokuwa mmoja wao amegeuka kona hii, watadhani umekuwa mjinga au watafikiri kwamba kitu kimbaya kimetokea kwako au umeshawishiwa na kitu ambacho ni tuhuma. Wanaweza hata kufikiri umekuwa wazimu! Kwa hivyo, lazima usiutangaze ufarisi wako vile iwezekanavyo. Kama una bahati, kutakuwa na mtu mmoja, iwe ndani ya familia yako kwa sasa au mtu utakutana naye atayekupa ishara usonge mbele.
Utataka kushiriki ufarisi wako mpya, na ugeni na uajabu wa mawazo hayo na dhana ambayo yatakuja kwako, na mabadiliko yale unahisia yanakukomboa kutoka siku zilizopita, lakini lazima uwe makini haswa kuhusu wale ambao unashiriki nao mambo haya, kwa kuwa wengine hawatafahamu, na ukosefu wao wa kufahamu na upinzani wao na hukumu itakuumiza na itafanya usijiamini.
Kutoka kuwa mtu anayeongozwa na kilicho nje kuwa mtu anayeongozwa na cha ndani ni mabadiliko makubwa, na mara ya kwanza utahisi una wasiwasi. Hutahisi kuwa una nguvu. Hutakuwa na hakika kuhusu unachokifanya. Utakuwa kama mmea mdogo zabuni katika msitu kubwa ambao lazima ulinzwe mpaka upate nguvu ya kutosha kusimama peke yake. Hivyo kuna hatari katika hatua hii ya mwanzo, katika sehemu hii ya kwanza katika sehemu hii ya mwanzo wa safari yako – mahitimisho ya mapema, indiscretion na watu wengine, kujishuku, jaribio la kujaribu kufafanua maisha yako – haya yote yana hatari kwa sababu yanaweza kuzuia uendelee, na wakati safari hii inaanza, lazima uendelee. Hii ni muhimu sana! Fikiria kuwa unapanda mlima mkubwa, basi, ukianza kupata mwinuko kidogo, basi, hutaki kurudi nyuma. Unahitaji kwenda mbele.
Knowledge ile Mungu ameweka ndani yako itakusihi uendelee, kuwa macho, kusikiliza kwa makini, kuwa mwaangalifu sana, kutia makini sana. Usidhani kuwa Mungu atakulinda kutoka kila namna ya madhara na kuzuia uumie na usikate tamaa na upate janga. Lazima utie makini sana. Hii ni sehemu ya kupata uelewa mkubwa. Hapo awali, haukutia makini. Ulikuwa reckless. Ulikuwa mpumbavu,na impulsive. Sasa ni lazima uwe mwaangalifu, mutambuzi, mvumilivu, makini. Katika kufanya hivyo, utaona jinsi umekuwa ukipoteza maisha yako, muda wako, nguvu yako, kwa shughuli zisio na maana na kwa mafikiro ambayo kamwe hayatasababisha azimio – kujishuku, kujihukumu, kuwahukumu wengine – mazungumzo makubwa ya juu juu yale watu wengi huendelea kudumisha karibu nawe.
Halafu, lazima ukukusanye rasilimali yako na kuhifadhi nguvu yako ili upate muda wa kuwa peke yako, ujifunze kutulia na kusikiliza. Unatafuta utulivu sasa zaidi ya sisimua. Utakuta kwamba shughuli za kijamii karibu nawe zitakukera, kwa maana unahitaji kitu kingine sasa. Unahitaji kusikiliza. Unahitaji kuwa na utulivu. Unahitaji kupata uhusiano mkubwa na nguvu hii inayojitokeza kutoka ndani.
Hii itabadilisha vipaumbele vyako. Hii itabadilsha tamaa yako. Hii itaathiri maamuzi yako. Na utakuta kwamba utakuwa tena hauna nia ya kufanya mambo na watu wengine ambayo hapo awali uliyafanya. Mambo yale kwa kweli kamwe hayatakupa utimizo, sasa utataka kuiepuka. Utaona utupu wao, na hautayataka, na yatakukera. Na utoto na purukushani ya mazungumzo ya watu, na hukumu yao ya mazoea dhidhi watu wengine, utakuta kuwa yanakukera. Hii ni asili.
Hii ndio inamaanisha kuja nyumbani kwako, kupata maadili yako halisi, vipaumbele vyako halisi, mwelekeo wako asili badala ya yale yote ambayo umeshawishiwa kuaamini. Utatafuta muda mbali na watu wengine. Utatafuta muda peke yake. Hautataka kuwa na kusisimua mara kwa mara. Unahitaji ujasiri wa kufanya hivyo. Watu wengi hawawezi kukaa zaidi ya sekunde tano kabla ya kuendeshwa nje yao. Hapa lazima ukukae na usikilize. Nadhari katika asili. Sikiliza sauti ya dunia, dunia ya kawaida.
Utaona hapa jinsi nishati yako yako – nishati ya akili na mwili wako – imekuwa ikitumiwa vibaya hapo awali, na utataka kuihifadhi, maana sasa unaihitaji. Sasa unakusanya nguvu yako. Unakusanya rasilimali yako. Hautupi maisha yako mbali. Unataka kuziba mashimo yote ambapo meli yako inavuja, ambapo unapoteza msimamo wako kwa wengine au kwa hali-kwa njia ya tabia au kwa njia ya miundo ya wengine.
Ujumbe Mpya utakuzungumzia hapa, kwa maana una nguvu na ufumbo wa Mungu. Na ni nguvu hii na fumbo hii inakuvuta sasa, kwa kweli kinachotokea katika maisha yako ni Mungu anasonga ndani yako. Mungu anakusongesha. Lakini msongu huu ni uhuru kutoka kwa mambo yote ya awali. Lazima udisengage. Huwezi kuchukua maisha ya zamani katika maisha mpya, kwa hivyo ni unaendelea kwa njia ya kudisengage hatua kwa hatua. Sehemu ya kudisengage ni ya kimwili. Inahusu shughuli na mahusiano yako na wengine, lakini kwa kiasi kikubwa inahusu mambo ya ndani. Ni mawazo yako. Ni compulsions zako. Ni kile unafikiri lazima ukikufanyae Ni kile unafikiri lazima uwe au unapaswa kuwa nacho au jinsi unapaswa kuwa na watu wengine. Kwa kuwa hapa ndipo mashawishi ya kijamii kweli hufanyika.
Na kila siku unasonga mbele, unavunja minyororo. Mamlaka yake kwako inapunguka. Ukipanda mlima, mvuto wa tambarare unapunguka, na unapata uhuru na unahisi u mwepesi kutoka kwa mzigo na matarajio ya wengine na kwa mahitaji yako yale hayakuwa halisi kuanzia.
Wakati huu, punguza wakati ule unaotumia kwa vyombo vya habari. Usisome vitabu vingi. Usiende sinema isipokuwa sinema hiyo ni inspirational, kwa maana unakusanya nguvu yako. Unaita nguvu kwako. Unahifadhi nishati yako. Unakisikiliza kwa makini kilicho ndani yako zaidi ya vile vilivyo nje. Unasonga mbali na Racket ya dunia. Iruhusu hii itokee. Ifuate. Iimarishe. Kwa maana hii ni mwendeko asili.
Kama urafiki wa dhati na hauwezi kukufuata sasa, itabidi uuwache, kwa upendo. Urafiki wenyewe utajitenganisha nawe, kwa sababu marafiki hao bado hawawezi kwenda nawe juu ya mlima huu. Unaenda mbali kuliko vile hao bado wanaweza kwenda. Umegeuka kona mabayo hao bado hawajageuka.
Jambo ngumu sana katika hatua za mwanzo ni wajibu kwa watu wengine, kwa marafiki wao, familia zao. Isipokuwa tu kwa wajibu wa kulea watoto wako, ambao ni lazima ufanye mpaka wawe watu wazima. Lakini kwa wengine wote, uhusiano wako sasa utakuwa katika mashaka. Pia itahitajika utoe huduma kwa mzazi wazee au mgonjwa, na hii ni sahihi. Lakini zaidi ya hii, unajenga utii wako kwa Mungu, na hii itatia utii wako kwa wengine na ngome kwako kwa mashaka. Kwa watu wengi, hii ni changamoto ngumu sana, Kizingiti kikubwa cha kwanza katika maandalizi yao.
Usijieleze kwa wengine. Sema tu kuwa kuna mikondo ya ndani zaidi katika maisha yako na unajaribu kuyafuata. Kuna mwelekeo ndani ya moyo wako na wewe unajaribu kuufuata. Waambie kwamba unahitaji muda peke yako, wakati wa utulivu, wakati wa faraghani, wakati wa utathmini. Usihisi kwamba lazima ujibu maswali. Sio lazima uwape majibu. Jipuri kutoka uchungu wa kujaribu kufanya hivyo.
Katika hatua ingine, itakuwa muhimu kwako ujifunze kuhusu njia ile Ujumbe Mpya umeutoa, kwa kuchukua hatua kwa Knowledge, kwa kusoma Hekima kutoka Jumuiya Kubwa, kujifunza juu ya Kiroho kutoka Jumuiya Kubwa. Hii itakuwa kama chakula kwako, chakula kwa moyo wako, chakula kwa nafsi yako. Utahitaji hii sasa kwa sababu itakupa nguvu na kuthibitisha mwelekeo mkubwa wa maisha yako. Itawapa uwazi zaidi, ufafanuzi mkubwa, na itakuonyesha kwamba kona hii uliopiga inawakilisha hatima yako na sio ajali katika maisha yako. Ni maisha yenyewe inayosonga ndani yako sasa. Na Ujumbe Mpya utaresonate na asili yako ya ndani zaidi, asili ambayo inayojitokeza polepole. Na hii italeta watu wapya katika maisha yako, watu ambao pia wanageuka kona na wameanza safari kubwa zaidi.
Ni muhimu hapa kuwa usiwe na imani imara. Huna haja ya kukubali imani imara. Unatafuta ufarisi wa ndani sasa. Ufarisi utakuwa msingi wako, sio imani imara. Unajitoa kutoka imani imara. Unaingia ndani ya eneo kubwa zaidi ya ufunuo na ufarisi wa asili. Kila mtu chini ya mlima anafuata imani imara, lakini imani imara haitakuwezesha kuupanda mlima huu, wala kupata mwinuko wa juu ambapo unaweza kuona ukweli wa maisha iliyo karibu nawe kama itakuwa dhahiri. Usifuate imani imara. Kama unahisi wasiwasi, kama huna uhakika, ni sawa, ni asili. Wacha maelezo yawe wazi. Usijiambatisha kwa seti nzima mpya ya imani. Hiyo ni sawa na kutoka gereza moja na kwenda kwa ingine. Oh, hapa ni mahali mpya! Lakini ni hali kama ya zamani. Oh, ni mpya na ya kusisimua na kutuliza, lakini ni hali ile ile ya zamani.
Ruhusu hatua zikufunulie kwa kweli safari hii. Sio safari ambayo inaeleweka kwa theorists au pundits au wanafalsafa, idealists, wasomi au wananchi kwa ujumla. Ni njia ya fumbo, safari ya ndani zaidi. Aya zake kitatokea zaidi ya eneo ya akili, kwa maana si safari ya kitaaluma. Akili yako itakomaa ili iweze kuelewa kwa kiasi. Na utajifunza kwa muda kupata mtazamo mkubwa na hekima kubwa kuhusu mambo mengi. Lakini sio safari ya kiakili, kwa kuwa akili ni uvumbuzi wa binadamu. Kile kilicho kuumba na kukuleta ndani ya dunia si uvumbuzi wa binadamu. Kile kitachokufunulia maisha makubwa ile unafaa kuishi na kutimiza si uvumbuzi wa binadamu. Lakini kinahitaji ushiriki wa binadamu, hekima ya binadamu, uwezo wa binadamu, imani ya binadamu, utambuzi wa binadamu ili kiweze kujitokeza.
Hapa hutoi nguvu yako yote kwa Mungu, kwa kufikiri kuwa Mungu atakuongoza katika kila kitu. Hiyo ni ujinga! Hapa unajitolea kwa mamlaka kubwa ndani yako ile sio ya uvumbuzi wako, lakini mamlaka hii inahitaji uwajibike, uwe mwaaminifu, uweze kuamua maisha yako. Itahitaji ufuate mambo ya fumbo, lakini mara nyingi utakuwa ukifanya mambo ya kawaida.
Kama uko katika uhusiano na una watoto, usifanye hatua yoyote kwa ghafla katika maisha yako. Kwanza jenga nguvu hii. Jenga uhusiano na Knowledge ndani yako. Jifunze kusikiliza. kuwa na wakati wa faraghani. Fuata mwelekeo wa asili yako. Shiriki sehemu tu ya fumbo na mume wako au mke, kwa maana labda hawatakuwa na uwezo wa kuelewa. Waulize wakupe wakati huu na imani hii, kwa kuwa kuna mambo yanayojitokeza ndani ya moyo wako. Dumisha wajibu wako na majukumu, lakini chukua muda wa kuwa pamoja na Knowledge ndani yako. Chukua muda wa kuchukua hatua kwa Knowledge, wa kujifunza Hatua kwa Knowledge na kujiweka katika nafasi ambapo hatua zitaweza kufunua ukweli wao mkubwa kwako.
Waambie watoto wako kwamba kuna nguvu kubwa ndani yao ambayo itawaongoza na itawalinda kama wataisikiliza. Shirikiana nao katika ufahamu wako. Lakini usijaribu kushiriki kila kitu, kwa maana unajenga nguvu, ukijaribu kushiriki kila kitu, unapeana nguvu yako. Usijaribu kutunza watu wengine zaidi ya watoto wako au mzazi mzee hapa, kwa maana unapata nguvu ndani yako. Unajifunza kuhifadhi nishati yako. Unajishikilia usijitolee kila mahali, unajishikilia ndio usipeane nguvu yako.
Usifanye maamuzi yoyote kwa ghafla kuhusu mahusiano yako ya msingi kama umeoa au umeolewa na watoto, kwa kuwa katika kesi nyingi itakuwa mapema. Ndoa hapa itakuwa katika changamoto. Mambo mengi ndio yataweza kuamua kama ndoa itaweza kuendelea, na huwezi kuwa na uwezo wa kuyajua mambo haya katika wakati huu.
Kazi yako ni kufuata uibuka wa Knowledge ndani yako, kuitumikia, kuipokea, kujivuta ndani, kuchukua muda unaochukua hadi uibuka mkubwa utokee ndani yako. Na usiwe na papara, kwa maana utaibuka wakati wake mwenyewe. Bado hutambui ukubwa wa kile kinachotokea au ukubwa wa uwezekano kwa nyakati zijazo.
Punguza mvuto ulio karibu na wewe. Kuwa kimya na wale wanajitembeza au wale wanahukumu dunia. Usijadili na wengine katika hatua hii. Usishindane na wengine. Usibishane kuhusu masuala. Usitetee mawazo yako. Kwa maana kwa sasa haya sio muhimu na yatakuwa counterproductive kwako.
Nguvu na uwepo wa Knowledge unajitokeza kwako. Hii ndio jambo la muhimu sana. Unajifunza kuwa na nguvu na kufuata mwelekeo wa ndani. Hii ndio jambo la muhimu sana. Dumisha majukumu yako. Jitolee kwa watoto wako. Lakini shikilia hii kama jambo la muhimu zaidi, hatimaye uhusiano wako mkubwa ni uhusiano wako na Mungu. Wajibu wako mkubwa ni kwa Knowledge ile Mungu ameweka ndani yako uijibu, uifuate na uieleze. Hii ndio uhuru usiyoweza kulinganishwa, lakini unahitaji nguvu kubwa ya ndani na uvumilivu.
Hizi ni miongozo za hatua za mwanzo. Zaidi ya hii, lazima ujifunze kujenga nguzo nne za maisha yako-Nguzo ya Mahusiano, nguzo ya Kazi, nguzo ya Afya na nguzo ya Maendeleo ya Kiroho. Lazima ujifunze kuhusu Jumuiya Kubwa. Lazima ujifunze kuhusu Mazingira ya Akili. Lazima ujifunze kuhusu mahusiano na madhumuni ya dhamira kubwa. Haya yote yanakusubiri. Lakini kwanza ni lazima ujenge msingi, bila msingi huu, huwezi kuwa na uwezo wa kupenya maana zaidi, umuhimu na matumizi ya Ufunuo hizi zilizomo ndani ya Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.
Msingi ni muhimu sana na unahitaji uvumilivu mkubwa na forbearance. Ni uvumilivu huu na forbearance ambao utahamisha utii wako kutoka kwa akili yako na maonyo ya wengine kwa Nguvu Kubwa ndani yako – nguvu ya Knowledge, nguvu ya Mungu. Kamwe hutaweza kuielewa nguvu hii kikamilifu. Kamwe hutaweza kuidai kwako mwenyewe. Kamwe hutaweza kuwa sahibu wake. Kamwe hutaweza kuitumia kwa kujaribu kuwa bora kuliko wengine. Huwezi kuitumia kukipata unachotaka . Huwezi kuitumia kupata utajiri na nguvu na radhi. Unaweza tu kujifunza kuifuata na kujifunza kufunga safari kubwa juu ya mlima uliotayarishwa kwako.