Author Archives: admin

Kuwa mtu wa Ujumbe Mpya


Ujumbe Mpya uko hapa kutoa ahadi na nguvu kubwa kwa bunadamu. Nguvu ya Knolwedge ambayo Mungu ameiweka ndani ya kila mtu ni majaliwa makubwa, majialiwa yanayosubiri kugunduliwa.

Ubinadamu bado haujagundua nguvu yake iliyo kubwa zaidi na uwezo wake mkubwa, uadilifu wake mkubwa na maadili yake makubwa ya msingi. Bado unalalamika, kama tamaduni haijakomaa, ikiendeshwa na uchoyo na uroho, chuki na hukumu. Bado haijakomaa katika kile ambacho kinatumikia na kinafuata. Lakini hii haikani ukweli kwamba ubinadamu una uwezo mkubwa ambao bado haujagundua na haujaendeleza.

Mwumba wa maisha yote ametuma Ujumbe Mpya duniani kutayarisha binadamu katika Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yanayokuja duniani na kutayarisha binadamu katika makutano na ulimwengu wa waangavu. Lakini matayarisho haya yanahitaji binadamu agundue na aendeleshe nguvu yake kubwa na uadilifu wake mkubwa.

Lakini binadamu kwa jumla hiawezi kufundishwa ama kutayarishwa mara moja, kwa kuwa mafundisho yanatokea kwa mtu binafsi. Kuleta mtu binafsi katika ufahamu wa nguvu yake zaidi na uwezo zaidi na uadilifu wake zaidi ndipo mbegu zitapandwa na ahadi ya binadamu imo. Kwa hivyo, usifikiri kile watu wote wanafaa kufanya, ama daima utakata tamaa. Yafikirie basi yale yako mbele yako.

Jamii na tamaduni zako labda zinataka tu utumbikie katika matumizi ama utumbukie katika kazi, mwanachama wa kikundi, mteja wa maadili ya utamaduni na vipaumbele. Lakini una ahadi kubwa zaidi katika maisha, ahadi kubwa iliyo na hakika kwa sababu ni sehemu ya asili yako ya ndani. Katika utamaduni, asili yako ya ndani husahaulika ama hupuuzwa na katika kesi zingine, hukanwa kabisa. Lakini huwezi kukana asili yako ya ndani milele, kwa kuwa inaishi ndani yako zaidi ya ufikio wa utamaduni, zaidi ya ufikio wa ufisadi, zaidi ya ufikio wa ghiliba na udanganyifu. Hiyo ndiyo sababu nguvu hii ya ndani ni nguvu yako kubwa na ina uwezo wako mkubwa na dhamira yako kubwa zaidi ya kukuja ulimwenguni.

Kile kilichohifadhiwa kwa wasomi hapo awali, kwa wajuzi lazima kiwe kama mlangu ulio wazi kwako na kwa watu wengine duniani. Kwa kuwa dunia inakabiliwa ya majaribio makubwa, hatari kubwa. Binadamu hajajitayarisha kwa Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Binadamu bado ni mjinga na mpumbavu katika maoni yake na mtazamo kuhusu matarajio ya waangavu ulimwenguni. Kwa hivyo ahadi ya binadamu ni ahadi ya mtu binafsi, kuamka kwa mtu binafsi. Hii ndiyo itampa binadamu nguvu kubwa zaidi ya msingi na uwezekano mkubwa kwa mazoezi ya hekima halisi ikikabiliwa na mustakabali haitabiriki na isiyo na hakika.

Ndiyo watu waweze kukabiliana na ufunuo wa Mungu, ni lazima watambue kwanza kuwa hawawezi kujitimiza wenyewe kutumia tabia zao za kawaida, tafrija na mabirudisho yale watu walio karibu nao wamejitolea. Ni lazima watambue wana haja kubwa na uwajibikaji zaidi katika maisha. Hii itaoneshwa hapo awali kupitia mateso yao na kuvunjika moyo kwao na dunia inayowazunguka wakizidi kupoteza maslahi katika michezo na burudani ya watu walio karibu nao kwa sababu wana haja zaidi ambayo sasa inajitokeza.

Kama wameridhi mahitaji ya mwili kupitia chakula, malazi, mavazi, na usalama; kama wmeridhi mahitaji ya akili kupitia upatikanaji wa elimu na fursa, basi haja kubwa itaanza kujitokeza ndani yao. Hii ni haja ya roho, ambayo inaweza tu kutimizwa kwa kutambua, kukubali na kutimiza dhamira yako kubwa iliyowaleta hapa-ambayo ni kitu ambacho kinaishi zaidi ya eneo la akili. Huwezi kuiwaza, lakini unaweza na ni lazima ufarisi nguvu hii. Na ina subiri kugunduliwa.

Kuwa mtu wa Ujumbe Mpya, lazima utambue kwamba ubinadamu unaingia katika zama mpya na kizingiti kikubwa na kisicho na uhakika. Hamuwezi tu kutegemea mafundisho ya kale au maagizo ya kale au unabii wa zamani sasa uwaongoze katika siku zijazo. Kwa maana dunia imebadilika na mabadiliko yafanyika haraka, lakini watu hawajabadilika nayo na wala hawaoni haja ya kubadilika. Mtu wa Ujumbe New basi lazima atambue kwamba yeye anasimama katika kizingiti cha mabadiliko makubwa katika hali halisi ya dunia, katika hali ya maisha ya hapa na katika ugunduzi kwamba upweke wao ulimwenguni umeisha, na kamwe hawatakuwa nao tena.

Dharuba hapa itakuwa kubwa, lakini ni dharuba iliyo na dhamira. Kwa kuwa inakuongoza kwa ugunduzi mkubwa unaoweza kuwa nao maishani, huo ni ugunduzi wa nguvu na uwepo wa Knowledge ndani yako – akili zaidi, akili kubwa, akili iliyo na nia na umakini, akili isiyo aliwasihi au kushawishiwa na dunia, akili iliyo safi na isiyo ya ufisadi, akili ambayo haiwezi kupotoshwa na dunia katika vishawishi vya dunia na majanga.

Ufunuo Upia unayataja haya kwa sababu binadamu lazima apate huduma kutoka kwa uwezo wake mkubwa zaidi, nguvu zaidi na uadilifu mkubwa. Kama hataweza kufanya hivyo,atashindwa akikabiliwa na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, na atashindwa kwa sababu ya udanganyifu na wa vikosi vya kutoka ulimwengu ambavyo viko hapa kuchukua faida kotokana na udhaifu wa binadamu na binadamu isiyo na umoja.

Kwa sababu ya hatari kubwa kwa utamaduni wa binadamu na ustawi na uhuru wa familia ya binadamu, Muumba wa uhai wote ametuma Ujumbe Mpya ulimwenguni, Ufunuo mkubwa kama Ufunuo wowote uliotumwa hapa.Upo hapa katika fomu safi, haujapotoshwa na serikali, haujapotoshwa na watu binafsi wenye tamaa, haujaunganishwa na utamaduni na siasa na nia ya chini ya ubinadamu.

Mtu wa Ujumbe Mpya anatambua kuwa anaishi wakati wa Ufunuo, wakati ambapo Ufunuo unahitajika kama watu karibu nao – hata katika nafasi ya uongozi katika serikali – wanaonekana kuwa hawajibu ishara ya dunia na kuibuka kwa mabadiliko makubwa.

Uwezo wa mtu binafsi kufanya maandalizi, kupata huduma kutoka kwa nguvu ya Knowledge na kufuatilia jambo hili kwa uaminifu – bila ya kujaribu kudhibiti au kuendesha akili hii kubwa – ni changamoto kubwa na fursa. Na bado inawakilisha ukombozi kwa mtu binafsi kwa sababu ni kwa kupitia njia ya Knolwedge ndiyo utaweza kuunganishwa tena na Mungu, ndio utagundua upya kwamba una dhamira kubwa zaidi maishani na uwezo wa kufuata hatua ya ufunuo wake, ufunuo binafsi.

Hapa unatambua kuwa wewe ni mwaanzilishi. Unakifanya kitu kipya. Uko katika mwanzo wa harakati kubwa sana, mabadiliko makubwa. Kama mwaanzilishi, utakabiliwa na upweke na ukosefu wa kutambuliwa na wengine. Lazima ujenge nguvu yako mwenyewe na dhamana na wengine ambao wanakabiliana na Ufunuo.

Hapa unatambua kuwa huna jibu ya siku zijazo, na huna jibu ya maisha yako, na majibu yako ni majibu yote uliopewa na utamaduni. Hata majibu ambayo unahisi una umba bado majibu yaliotolewa na wengine. Lakini kuna jibu moja tu, na kwamba ni kujiandaa kukabiliana na dunia ya mabadiliko makubwa. Ni kuiandaa maisha yako na akili yako ya itumikie katika uwezo wa juu. Ni kwa kupitia maandalizi makubwa ambayo haukuunda mwenyewe, lakini ambayo uliyopewa kupitia neema na Providence.

Hapa unavunja minyororo ya tabia ya upotovu unayoshinda ukirudia, haja ya idhini na kuzingatia utamaduni na dikteta ya taifa lako, kwa dhamana na kuungana na Nguvu Kubwa na uwezo ambao ni chanzo cha maisha yote katika Ulimwengu. Na unafanya hivyo kwa unyenyekevu, na haujitangazi, kwa maana unajua Nguvu Kubwa sio yako ya kutumia au kudhibiti. Lakini una heri kwa kuipokea na kuiruhusu ijenge maisha upya na mwelekeo wako ili utimizo halisi na uridhiki uweze kupatikaka kwako.

Basi, unajitayarisha, kuwa mume au mwanamke wa Knowledge – sio tu kwa ukombozi wako na utimilifu, lakini kwa kuchangia sehemu yako wakati wa kipindi cha mpito mkubwa duniani. Haujui maana ya hii au umuhimu wake. Labda utadhani utakuwa kiongozi mkubwa, lakini watu wachache tu ndio watakuwa viongozi mashuhuri. Utachangia tu katika sehemu ambayo ikuchukua sura na umbo ukiendelea na kama mahusiano yako na watu wengine yatapata ufafanuzi zaidi na uaminifu mkubwa.

Wewe ni mtu wa Ufunuo Mpya, na wewe unapata uhuru na huzuliwi na siku za nyuma, kwa maana unabeba mbegu ya siku zijazo. Unabeba chombo cha siku zijazo. Haitoshi tu kuishi kwa muda mfupi, kwa kuwa hiyo ni nusu tu ya maana ya maisha. Lazima pia ujiandae kwa siku zijazo, na Knowledge ndani yako inajua jinsi mustakabali utakuwa na jinsi utaweza kujiandaa kwa busara, ufanisi na kwa usalama.

Njia kwa kweli ni rahisi kabisa, lakini kwa sababu imo nje ya eneo la akili, watu wanaweza kuwa na mashaka sana na kuchanganyikiwa kuihusu, kujaribu kumechi ukweli wake na imani yao ya sasa na mitazamo. Na bila shaka imani yako ya sasa na mitazamo ni vuimbe vya utamaduni na mara nyingi ni bidhaa ya hofu. Hayalingani na hali halisi ya maisha yao kubwa zaidi. Hayo ni mabaki tu ya zamani na ya utambulisho wa zamani, ambao bado wanabeba na lazima wajifunze kuyawacha.

Kuwacha utambulisho huu ni jambo la kawaida kabisa. Ni kama kuwacha ujana na kuwa mtu mzima. Kama kijana, unajitambua na umri yako na vijana wengine, na unashawishiwa na maadili yao na shughuli zao. Lakini ukiwa mtu mzima, vipaumbele vyako hubadilika. Unapanieni mambo ya maana na thamani kubwa zaidi, na kujitolea katika majukumu zaidi maishani. Kwa hivyo ni hapa unawacha utambulisho wako wa zamani. Unachukua wajibu mkubwa, na unatafuta maana zaidi. Shughuli za zamani zinaonekana ni kama zinakosa na hazitoshi kwa mahitaji yako ya ndani zaidi.

Hii ndio kukomaa kiroho. Hii ndio maana ya kuendelea kutimiza ngazi ya mahitaji ya ndani yenu. Na hii ndiyoinakuunganisha na dunia na wale waliokutuma hapa. Ni hapa unapata utimilifu wako mkubwa ndani ya uadilifu wako, ndani ya ubora wa mahusiano ambayo sasa yataanza kukuja kwako na kwa hisia ya maana itakayoenea katika maisha yako.

Kile kilichokuwa cha kuepuka hapo awali sasa kinakuwa muhimu zaidi kwa mtazamo wako. Mazoezi ya kiroho sio tu aina ya kutolewa shinikizo. Kinakuwa sasa msingi wa kujenga nguvu, lengo kuu la shughuli zako. Hapa unaleta mazoea yako ya kiroho katika kila kitu unachokifanya kwa sababu ni muhimu kwa kila kitu unachokifanya, na yatakusaidia na kuleta uwazi katika kila kitu utakachokifanya.

Hapa hakuna dhabihu ya kweli. Unayawacha yale ambayo yanaonekana kuwa yanakosa au hata ni pumbavu, yale ambayo yalikua muhimu kwako hapo awali. Watu wengi kamwe hawakui wakubwa katika mambo yanayohusu kiroho, na hivyo hubaki katika hali ya utoto au ujana kiroho. Ingawa wana mvi na kuwa wenye umri wa miaka mengi kimwili, kamwe kweli hawakui wakubwa katika mambo yanayohusu kiroho. Lakini mchakato wa ukuaji ni sawa-kukiacha cha zamani, uibuka wa kipya, maumivu ya kuongezeka ya kuwa mtu wa kuwajibika, mtu wa uwezo zaidi, na nafasi kubwa ya kufarisi mahusiano katika eneo ya juu ya dhamira katika maisha, ambayo ni kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kimo nje ya uwezo wa wengine ambao bado maendeleo haya hayajitokeza kwao.

Mtu wa Ujumbe Mpya anatambua kuwa yeye ni sehemu ya kitu kikubwa kinachojitokeza. Hawana haja ya kuona hitimisho au matokeo, kwa kuwa imo nje ya uwezo wao na zaidi ya maono yao. Si wajibu wao kuhakikisha matokeo, lakini kuchangia sehemu yao kwa harakati ya binadamu katika mwelekeo chanya. Na ubinadamu unaweza vipi kusonga katika mwelekeo chanya bila msaada mkubwa ambao Muumba wa uhai wote anautoa? Ni dhahiri ya kusikitisha kuwa binadamu hawezi kufanya hivyo mwenyewe, au hataki, vile kesi ilivyo.

Watu huomba Mungu awasaidie, awape nafasi, awakomboe, waepuke maumivu na mateso, awape upya au ufufuo. Lakini Ujumbe ukikuja kwa fomu kubwa kama hii, hawaoni, wala kujibu au wanakana jambo hilo kwa sababu haithibitishi na haitimilizi matarajio yao au imani yao ya awali.

Kama kweli unataka Mungu akusaidie, basi ni bora uwe tayari kubadilisha maisha yako. Mungu atakusaidia kabisa. Kama huna uhakika unaitaka, basi labda uwache kuomba na kusema affirmations zako.

Watu wa Ujumbe Mpya lazima wamusaidie Mtume wakati yeye bado ako duniani. Kazi yake ni kubwa mno. Ni kubwa zaidi kuliko kile mtu mmoja angeweza kufanya. Lazima waushuhudie. Lazima wauwakilishe. Lazima wawe na ujasiri wa kuwa sehemu ya Ufunuo na si tu waangalizi wake au watazamaji wake.

Nguvu ya Ufunuo kurejesha ubinadamu na kuandaa ubinadamu utahitaji matendo ya watu wengi. Ufunuo ni safi. Haujapotoshwa. Umetolewa kikamilifu. Mtume hajafariki na nusu Ujumbe mikononi. Muumba wa maisha yote amekihakikisha hicho. Kila kitu kiko mahali pake.

Ufunuo anasemea hali halisi tofauti ndani ya watu. Hauridhishi akili yao au kiburi wanachomiliki. Hauingiliani na virahi vyao na mawazo yao yasio kamilifu au sahihi. Haujafungwa na upendeleo wa binadamu au nia ya binadamu, kwa hivyo unaonekana ni wa ajabu lakini no confounding, mpya na tofauti lakini kwa kiasi fulani wa kale na usiyo na wakati.

Mtu wa Ujumbe Mpya lazima awe sehemu ya Ujumbe Mpya. Hawawezi tu kuwa mlaji ambaye atauiba na kutoroka nao na kujaribu kuutumia kujenga utajiri, au nguvu binafsi au kupata faida binafsi. Kama wezi usiku, wataiba na kudai kuwa nguvu ya Ujumbe Mpya ni nguvu yao wenyewe na faida ya Ujumbe ni faida yao, uandishi wa Ujumbe Mpya ni uandishi wao. Utaona jaribio la jambo hili, ndiyo, kwa sababu ubinadamu kwa jumla una ufisadi mno na hauwezi kukabiliana na jambo hili safi, hii ndiyo maana mtu binafsi ndiye lengo shabaha na sio raia wote wa dunia.

Ni watu wakijifunza na kuishi Ujumbe Mpya ndio watakuwa na uwezo wa kuhamisha na kutafsiri nguvu na hekima yake ndani ya familia zao, jamii zao, mataifa yao, dini zao, kila kitu-wakileta mabadiliko katika mtazamo wa binadamu ambao utatokea pole pole na kwa mdua.

Watu wataanza kufikiria kwamba wao ni wenyeji wa dunia hii na lazima waanzishe kanuni zao za ushiriki kuhusu kujiliwa na kuingiliwa. Bila shaka, ni dhahiri. Watu watasema, “Bila shaka, hatuwezi tu kuwacha mtu yeyote aje hapa na afanye chochote anachokitaka. Na hatutaruhusu tuambiwe kuwa vikosi hivi viko hapa kutuokoa au kutukomboa.”

Bila shaka. Itakuwa ni kama akili ya kawaida katika wakati huo, lakini kwa wakati huu, inaonekana kuwa ni ya ajabu na haiwezekani. Yawezekanaje hivyo? Kwa sababu watu bado wanafikiri kama tamaduni haijakomaa. Bado wanafikiri kuwa wako peke yao ulimwenguni. Hawaifikirii mustakabali. Hawaoni kuwa ubinadamu tayari umenyonya dunia kwa kiasi itakuwa vigumu kuwa na uwezo wa kujilisha katika siku zijazo, na hivyo umesababisha Mawimbi Makuu ya Mabadiliko.

Ahadi iko kwa mtu binafsi, na hii daima imekuwa ndiyo kesi. Ufunoa wote mpya, maboresho yote mapya, ubunifu na hatua kubwa katika sayansi, biashara na haki za kijamii zimekuwa zikiendeshwa na watu binafsi ambao walivuviwa na kujitolea kwa huduma yao. Hivi ndivyo jamii zote katika ulimwengu zinaendelea na zina ahadi.

Kwa mtu wa Ujumbe Mpya, ana wajibu mkubwa hapa, pengine ni ana wajibu kubwa zaidi kuliko kitu chochote ambacho wamewahi kukichukua. Baadhi ya sehemu yao bado inataka kwenda mbali na kuwa na furaha na kuishi maisha ya ustaarabu mahali fulani, kuishi maisha ya aina ya uvivu, maisha ya kutokuwajibika. Lakini ndani yao kunajitokeza nguvu na uwezo na sauti kubwa na hali ya kujutolea na mwelekeo ambao sasa unakuwa mfumo wao na mazingira yao.

Wameshikamana na siku zijazo. Wameshikamana na Jumuiya Kubwa. Wameshikamana na muda wao na nyakati zijazo. Wanaanza kujibu kama wao kwa kweli walitumwa duniani kutimiza kitu fulani katika mahusiano na watu wenginne. Wanaanza kufikiri na kujisikia kama viumbe vinavyoishi milele na vilivyo hapa kutoa huduma katika mazingira ya muda mfupi na ya wasiwasi.

Lakini kufikia katika ufahamu huu na nguvu ya ukweli huu inahitaji dhamira kubwa na maandalizi. Huwezi kukabili jambo hili shingo upande. Huwezi kuwa na papara au manipulative au kuendeshwa na mapendekezo yako, ama hutaweza hata kuwa na uwezo wa kuanza. Utashindwa katika changamoto ya kwanza au kikwazo, jaribio la kwanza litafanya ukate tamaa, ukijua watu walio karibu nawe wale ulidhani walikuwa marafiki na walio karibu nawe kwa kweli kuwa hawana kidokezo au hawataki kushughulika na mambo haya na watakukana ukijitangaza.

Hapa unatambua kuwa una uchaguzi. Unaweza kufuata nguvu inayojitokeza ya Knowledge, hata kama hauielewi, ama utaendana na mahitaji na matakwa ya familia yako au marafiki. Watu wengi hushindwa katika hatua hii, wanajiunganisha tena ndani ya amnesia ya utamaduni, na tabia ya upotovu wanayoshinda wakirudia ya utamaduni, kwa ushawishi wa utamaduni. Waliamka kwa muda mfupi, halafu wakashindwa na nguvu za mazingira ya akili karibu nao, zilizo wanyakua – katika vivinyovinyo, katika kutowajibika, katika ndoto.

Lazima sasa uushugulikie wito wako na maendeleo na maendeleo ya wengine karibu na wewe ambao unawajua, ambao wana uwezo wa kukabiliana na Ufunuo Mpya maishani. Lakini huwezi kupanda mlima huu ukisubiri wengine. Lazima wewe mwenyewe uupande mlima huu, hata kama marafiki wako wa dhati hawawezi kuenda nawe. Unaweza kusaidia dunia na kuwasaidia kama unaweza kupaa na kufunga safari hii zaidi kuliko vile unaweza kuwasaidia ukikaa nyuma na kuwatia moyo.

Kuna hekima nyingi na uwazi wa kupatwa njiani. Kiasi chake hakiwezi kuonekana wakati huu, lakini kinakusubiri katika safari yako. Na huwezi kujifunza mambo haya isipokuwa ufunge safari hii. Huwezi kujifunza hayo kama amri au kama mawazo, kwa sababu huwezi kumiliki uwezo uliopo, kuufuata na kuuonyesha.

Mtu wa Ujumbe Mpya ni sehemu ya Ujumbe Mpya kama mchangiaji, bila kujaribu kufafanua jukumu lako au kudai mamlaka au kudai nafasi yako mwenyewe. Hii itahitaji mpango mkubwa wa kujizuia kwa upande wako, kwa ajili haya maelekeo yote bado yamo ndani yako-mbegu za uovu, mbegu za uchoyo, mbegu za udanganyifu, mbegu za udanganyifu wa kibinafsi – zote ziko hapo. Mbegu mingi zimo hai ndani yako wakati huu. Kwa hivyo lazima uzuie haya yote na urejee Knowledge na kuomba msaada kutoka kwa watu wengine ikibidi.

Kwa maana hautaki kupoteza wito huu. Umetoka mbali sana. Hutaki kushindwa. Tayari umeongozwa nje ya obsessions za utamaduni kwa kiwango kikubwa. Hutaki kushindwa katika kutekeleza azma hii, fursa kubwa unaweyoza kuwa nayo-wewe ambaye umeteuliwa na una bahati kubwa mno, na bahati ya kuwa miongoni mwa wa kwanza wa kupokea Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Je, unakitambua kilicho mbele yako? Je, una wazo lolote? Katika deprecation yako ya kibinafsi, unaweza kukiona kilicho mbele yako? Mungu amekupa njia, njia ya kutoka mwitu, maze isiyo na matumaini ya vivinyivinyo vya binadamu na maelewano ya binadamu.

Kwa hiyo, usivunjike moyo. Kaa pamoja na maandalizi yako na mazoezi. Wache ishara za dunia zikuambia nini kinachokuja, na uwache ishara ndani yako izuie tabia yako mbaya ya kithiri na jinsi unajilaumu – bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa usahihisha binafsi ule lazima uwe nao katika mawazo yako, dhana zako na tabia yako. Mwalimu mwenye busara hawaadhibu wanafunzi, lakini tu husahihisha wanafunzi wake. Hivi ndivyo lazima ujifundishe. Hivi ndivyo jinsi mzazi mwenye busara na upendo hufundisha mtoto wake aliye kijana bila hatia.

Wewe ni kama mtoto sasa katika kuendeleza ufahamu wako ya Jumuiya Kubwana na katika kugundua nguvu ya Knowledge. Umo katika hatua ya mwanzo, na kuna barabara kubwa mbele yako. Hatimaye, una dhamira, maana na mwelekeo. Lakini ni lazima ukae na hili na usiepushwe na vikwazo, masumbuko na mawazo ya zamani na imani zinayoleta mawingu kwa akili yako, mawingu yanayoweza kufanya upoteze njia yako juu ya mlima. Usitongozwe na sehemu nzuri za kuburudika njiani, kwa kuwa una hatima na safari ya kuchukua. Hivi ndivyo Mungu atakukomboa, kwa njia ambayo kamwe hungeweza kujikomboa.

Ujumbe Mpya unasimamia nini?

1.Uhuru– Kujifunza kujenga uhuru, kudumisha na kulinda uhuru wa mtu binafsi na uhuru wa ubinadamu ukikabiliwa na changamoto kubwa na ya kipekee.

 

2.Umoja wa ubinadamu, ushirikiano na kumalizika kwa vita na migogoro -sio kwa sababu ya maadili kamilifu lakini kwa uhai wa ubinadamu.

 

3.Uendelevu na marejesho ya kuhifadhi mazingira– kuhufadhi na kugawa rasilimali ya dunia inayopunguka badala ya kuyapigania, ili kuepuka vita ndiyo ubinadamu uweze kuwa na mustakabali.

 

4.Umuhimu wa Knowledge ndani ya mtu binafsi– Knowlegde ni kipaji kutoka kwa Mwumba kinachoishi ndani yako na kinachokupatia uwezo wa uzoefu na kueleza Kiroho Moja cha ubinadamu, zaidi ya matenganisho ya rangi ya ngozi, mataifa, utamaduni na dini. Knowlegde peke yake ndiyo ina nguvu ya kuongoza na kulinda mtu binafsi na kuwaunganisha na kuwawezesha wanadamu kubuni njia mpya kwa mwenendo wa mbele.

 

5.Mshikamano wa amani na ushirikiano kati ya dini za dunia– Dini zote duniani zilianzishwa na Mungu na kamwe lengo la dini hizi halikuwa kushindana na kuwa na mgogoro kati yao.

 

6.Kuwa na nguvu katika mazingira ya akilii- Unaishi katika mazingira ya akili na pia katika mazingira ya kimwili. Mazingira ya akili ni mazingira iliyo enea ya fikra na ushawishi ambayo sisi wote tunaishi. Kuwa na uwezo wa kufikiri kwa uhuru, wa kuweza kutambua na kupinga ghiliba ya akili, lazima ujifunze kuhusu mazingira ya akili na uwe mwenye nguvu ndani yake.Hatua kwa Knowledge, Kitabu cha Ujumbe Mpya ya mazoezi, kitakufunza jinsi utaweza kufanya hivyo.

 

7.Kujiandaa kwa Jumuiya Kubwa-Upweke wetu umeisha. Unabii wa Ujumbe Mpya unafumbua kwamba binadamu hako peke yake ulimwenguni nahata ndani ya dunia hii. Ujumbe Mpya uko hapa kuwatayarisha watu na mataifa kwa ukweli, hatari na nafasi ya kuibuka Jumuiya Kubwa ya waangavu ulimwenguni. Kama watu asili wa dunia hii, Lazima tupambane kuingiliwa na mataifa kutoka nje kwa hekima na utambuzi na tuanzishe sheria zetu za shughuli.

 

8.Kujiandaa kwa Mawingu Makubwa ya Mabadiliko– Unabii wa Ujumbe Mpya unafumbua kwamba binadamu anakabiliwa na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, yatayoleta hali isiyokuwa ya kawaida katika historia ya binadamu. Kati ya Mawimbi Makubwa kuna mabadiliko ya hali ya hewa na hali ya hewa ya janga, kushuka kwa rasilimali za nishati, uchakavu mkubwa wa mazingira, kupungua uzalishaji wa chakula, migogoro ya kiuchumi na tishio kubwa ya migogoro ya ushindani, na vita dhidi ya rasilimali ya dunia iliyobaki. Mawimbi Makubwa yataleta hali ya ukosefu wa utulivu duniani, hata katika mataifa tajiri. Ugundulifu na tayarisho kwa ukweli wa Jumiiya Kubwa na kukabiliwa na Mawimbu Makubwa ya Mabadiliko unawakilisha hitaji kubwa ya wataki huu wetu. Ujumbe Mpya uko hapa kututayarisha katika kukabiliwa na nyakati ngumu zilizo mbele.

 

9.Kuchangilia kwa dunia ya mahitaji- Furaha ya ukweli inakuja unapofanya kazi uliokija kuifanya. Kutimiza hii, lazima uunganishe akili yako ya ma_kirio na akilli yako iliyo ndani yako ya Knowledge na kukuza hekima na nguvu ya kutimiza misioni yako duniani.

 

10.Kujenga nguzo nne za maisha yako– Maisha yako iko na nguzo nne. Kama miguu minne ya meza, ambayo yanazingatia maisha yako na kukupa nguvu, utulivu na usawa:

Nguzo ya Uhusiano

Nguzo ya Afya

Nguzo ya Kazi na Providership

Nguzo ya Kiroho

Ujumbe Mpya unafumbua maana ya hizi nguzo nne na jinsi zinavyoweza kuwa za nguvu na kuamirishwa. Utahitaji nguzo zilizo imara na za nguvu ili kuwa na uwezo wa kuhimili Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na kuwa duru ya nguvu kwa wengine.

 

11.Mahusiano ya dhamira muhimu-Ulizaliwa ma mision na Knowledge ya kukusaidia kugundua na kutimiza mision hii. Kwa sababu ya hiyo, kuna watu fulani unafaa kukutana nao na kuwasiliana nao. Ndani ya roho yako, hii inawakilisha utaftishi wako wa mahusiano. Katika Ujumbe Mpya, mahusiano haya yanaitwa mahusiano ya dhamira muhimu. Ujumbe Mpya unakufundisha kutafuta na kutambua watu hawa zaidi ya fomu zozote za kivutio na wajibu. Hauwezi kupata na kutimiza mision yako peke yako. Utahitaji mahusiano ya kipekee ya uaminifu na uadilifu ambayo mision na hatima yao ni sawa na yako.

Lazima kuwe na agano inayotetea mambo haya. Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni agano mpya, uelewa mpya, njia mpya, inayoenda zaidi ya imani na dhana za kale, zaidi ya mashindano na ugomvi wa kale.

Ujumbe Mpya unasimamia hekima, uhuru, dhamira, umoja, na ushirikiano ulio na msingi katika Kiroho Moja ya ubinadamu na haja kubwa ya wakati wetu.

Jinsi Ujumbe Mpya ulikuja.

“Upendo mkubwa umeleta Ujumbe huu Mpya katika dunia – upendo wa Muumba kwa maumbile, upendo wa Muumba kwa familia ya binadamu- kuonyesha ubinadamu nafasi yake kubwa ndani ya dunia kuwa taifa ya umoja na iliyo huru.”

Ujumbe Mpya unamilikisha mapenzi na Mungu kwa binadamu, wa sasa na wakati ujao. Mapenzi ya Mungu yametafsiriwa katika lugha, katika maandalizi na katika mafundisho kamili na Malaika ambao wanawakilisha mapenzi ya Mungu na madhumuni ya Mungu kwa binadamu katika ulimwengu huu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ulitolewa katika kipindi cha zaidi ya miaka 25. Ilitolewa katika hali ya kupokea ufunuo na Marshall Vian Summers.Kila neno la ujumbe lilisemawa na likarekodiwa, halafu baadaye likanukuliwa.Hii imelinda uadilifu na usafi wa Ujumbe Mpya katika fomu yake ya asilia. Kile ambacho hatimaye kilikuwa vitabu nzima kilitolewa katika siku au hata masaa. Kwa mfano, sura 27 za Kiroho kutoka kwa Jumuiya Kuu: Ufunuo Mpya zilitolewa katika siku kumi na moja tu. Utaratibu huu wa ufunuo unaendelea.

Hii ndio jinsi Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umekuja ulimwenguni, na mfululizo huu unalingana na Ujumbe yote kubwa ambayo yamewahi kumtumwa ulimwenguni kwa maendeleo ya binadamu. Mungu hutoa mawasiliano haya makuu na ya wakati muafaka kwa njia ya Malaika, katika dunia hii na dunia zote ndani ya Ulimwengu. Hii ni hali ya mawasiliano na Mungu. Hii ni jinsi Mungu huwasiliana na watu binafsi na mataifa yote na jamii.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu unafaa kutumikia ubinadamu wakati huu na wakati ujao. Ni Ujumbe kubwa sana. Zawadi yake, ufanisi wake na muda wake wa milele kwa familia ya binadamu kamwe usidunishwe.

Inamiliki hekima na maarifa, maarifa na hekima zaidi ya kitu chochote ambacho ubinadamu umeshawahi kupewa. Na itachukua ujasiri mkubwa, unyenyekevu na uvumilivu kupokea kiasi kamili ya maneno ambayo Ujumbe Mpya inamiliki. Nguvu yake, ukweli wake na amani ambayo inyotoa inazidi akili ya binadamu.

Ujumbe Mpya wa Mungu una matumaini na ahadi ya kuongoza familia ya binadamu katika siku zijazo ili binadamu aweze kujenga uhuru na haki kuu katika dunia na kuchukua nafasi yake kama taifa huru na umoja katika Jumuiya Kubwa.

 

Mungu ni nini?

“Hapa lengo lako halitakuwa Mungu wa dunia yako na muda wako, bali ni Mungu wa dunia zote na wakati wote.”

Katika Ujumbe Mpya, Mungu hufikiriwa ndani ya muktadha mpana wa ulimwengu mzima, badala ya ndani ya hii dunia moja. Ni hatima ya binadamu kuibuka ndani ya Jumuiya hii Kubwa ya maisha ya waangavu.Katika Kiroho cha Jumuiya Kubwa, kitabu cha theolojia ya Ujumbe Mpya, hivi ndivyo Mungu ameelezwa,

“Katika Jumuiya Kubwa Mungu ni kamili. Katika dunia yenyu, Mungu ni Mungu wa dunia yenyu, Mungu wa jamii yenyu, Mungu wa historia yenyu, Mungu wa asili yenyu, Mungu wa hofu na matarajio yenyu, Mungu wa mashujaa wenyu, Mungu wa janga yenyu, Mungu aliye na mahusiano na kabila yenyu na wakati wenyu. Lakini katika Jumuiya kubwa, Mungu ni mkubwa sana, kamili zaidi ya ufafanuzi wa taifa yeyote, zaidi ya historia ya taifa yeyote zaidi ya asili, hofu na matarajio ya taifa yeyote, zaidi ya uelewa wa filosofia. Na hata hivyo, unapata Mungu katika sirika safi, katika wakati usio na muda wa utambuzi, katika hamu ya kutenda zaidi ya nyanja ya maslahi na nia yako binafsi,katika utambuzi wa wengine, katika maarubu ya kutoa, katika ufarisi usioweza kuelezwa wa mvuto. Hizi zinaweza kutafsiriwa. Hii ni Mungu katika vitendo.Kwenyu, hii ni Mungu.

Muwaze Mungu katika mtazamo kwa Jumuiya Kuu– sio kama Mungu wa binadamu. Sio kama Mungu wa historia yenyu, sio kama Mungu wa mateso na majaribu, lakini kama Mungu wa wakati wote, wa mataifa yote ulimwenguni,wa vipimo vyote, kwa wale walio katika mwanzo wa mfululizo wa mabadiliko ya utamaduni, na kwa wale walio mwisho wa mfululizo wa mabadiliko ya utamaduni, kwa wake wanaofikiri kama wewe na kwa wale ambao wanafikiro tofauti, kwa wale ambao wanaamini na kwa wale abao imani ni kile ambacho hakiwezi kuelezwa. Hii ndiyo Mungu katika Jumuiya Kubwa na hapa ndipo lazima uanze.”

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni nini?

 

“Ujumbe Mpya umetumwa na Mwumba wa maisha yote. Ni ujumbe wa kumutyarisha binadamu binafsi na kuwatayarisha watu wa dunia ili waishi na waweze kupenya hatari kubwa itayokabili binadamu. Ni zawadi kubwa katika uso wa haja ya haraka. “

Kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani. Ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwumba wa maisha yote ya kulinza na kuendelesha binadamu. Ina onyo, baraka na maandalizi kwa watu wote wa dunia.

Ujumbe Mpya hauna msingi na dini za utamaduni duniani au mafundisho ya kiroho. Ni zawadi kwa watu wa mataifa yote na imani zote. Ina heshimu ukweli unaodumu katika Ujumbe kuu ambazo Mwumba amewahi kutuma duniani, na sio kama chochote kile ambacho kishawahi kufuniliwa kwa binadamu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni mawasiliano ya halisi kutoka kwa Mwumba ambao umetumwa ulimwenguni wakati wa mabadiliko makubwa, migogoro na mapinduzi. Ujumbe Mpya unatoa maarifa, hekima na mwelekeo ambao ubinadamu wenyewe hauwezi kutoa ili ukabiliane na changamoto kubwa ambayo kwa sasa inakabiliwa na familia nzima ya binadamu.

Ujumbe Mpya ni jibu ya maombi ya dhati kutoka kwa watu mataifa yote na imani za utamaduni kwa uhuru, usalama na ukombozi. Ni ufunuo mpya kuhusu Kiroho Moja, hifadhi ya dunia na mustakabali ya binadamu na hatima ya binadamu ndani ya Jumuiya kubwa ya maisha ya waangavu katika ulimwengu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umo ndani ya mfululizo wa maandiko matakatifu na mafundisho. Ulifunuliwa katika kipindi cha miaka ishirini na tano. Ufunuo bado unaendelea mpaka leo.

Je, Mungu huwasiliana aje na wewe?

“Kupitia Knowledge unaweza kuhisi uwepo wa mahusiano yote. Hii ni ufarisi wa Mungu.”

 Mungu ni Chanzo cha Knowledge ndani yako, Knowledge ni roho ya ndani ya akili, ile Muumba ameweka ndani yako iwe nawe na iwe na viumbe vyote ambavyo vinamiliki hisia na fahamu isiyo na muundo, katika Ulimwengu.

Mungu aliumba ulimwengu wa kimwili, lakini sio vile wewe unafikiri. Mungu aliendesha mchakato wa mageuzi katika ulimwengu wa kimwili uchukue nafasi na muda kwa wale ambao wanaishi katika nafasi na muda, kwa wale ambao walitenganishwa na Muumba kwa mapenzi yao na nia yao.

Kuelewa taarifa hii, kwamba Mungu ndiye Muumba wa Knowledge ndani yako, lazima uelewe tofauti kati ya akili yako ya kiroho na akili yako ya dunia. Lazima uelewe tofauti kati ya Roho yako, akili yako na mwili wako. Knowledge ndani yako inawakilisha uhusiano wako na Mungu na maisha yako nje ya dunia hii. Uhusiano huu uwepo kati ya na zaidi ya dini zote za ukweli. Knowledge ni safi na ni ya kudumu na haiko kiasi ya nguvu au ushawishi wa chochote duniani.

Ujumbe Mpya utakufundisha jinsi ya kuyaelewa mambo haya kwa njia wazi iwezekanavyo. Lakini kwa sababu hiki ni kizingiti kipya na uelewa upya kwa binadamu, itachukua muda na kutia moyo kutoka kwa wengine ambao wanajifunza na wewe. Ni vigumu na changamoto kujifunza kitu kwa mara ya kwanza wakati kila mmoja aliye karibu na wewe anazingatia maadili na mawazo tofauti na wewe. Kama unaweza kuona kuwa Knowledge ndani yako ni ile sehemu itakayo dumu, ile sehemu iliyoumbwa na Mungu na bado inayoshikamana na Mungu, sehemu ambayo Mungu amerishai na hekima yake kuongoza na kulinda maisha yako katika dunia hii na kwa wakati huu, basi unaweza kuanza kuona hali halisi ya uandishi huu wa Mungu na umuhimu kwako wewe unayetaka kupata kusudi ya ukweli, maana na mwelekeo katika maisha yako.

Kwa nini Ujumbe uko hapa?

 

“Binadamu anaelekea katika mustakabali ambayo itakuwa tofauti na siku zilizopita, lakini hako tayari. Hiyo ndiyo sababu kuna ujumbe mpya kutoka kwa Mungu.”

Binadamu anasimama katika genge la mabadiliko makubwa na na mustakabali wa geugeu

Kuongezeka kwa idadi ya watu katika dunia ya rasilimali chache,tishio la kuenea kwa kunyimwa kwa binadamu, migogoro na vita kwa sasa ni makubwa zaidi kuliko hapo awali. Hiyo ndiyo sababu kuna ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Ubinadamu inakabiliwa na kuongezeka kwa madhara ya uharibifu wa joto duniani, mabadiliko ya hali ya hewa ya janga na kuzorota kwa mazingira. Hiyo ndiyo sababu kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Dini mingi za dunia ni vigae,zina mwelekezo wa zamani na pia zinashiriki katika mashindano ili kuweza kutahadhari na kuandaa familia ya binadamu kwa yale yakatakayokuja. Hiyo ndiyo sababu kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Watu wamegawana na hawajui Kiroho Moja cha ubinadamu na Chanzo Moja cha dini za utamaduni za binadamu wote. Hiyo ndiyo sababu kuna Ujumbe Mpya kutotka kwa Mungu.

Watu wanatumia Mungu na dini kuhalalisha vitendo vya ukatili na vya kutisha na pia vya kulipiza kisasi dhidi ya wengine. Hii inagawa familia ya binadamu wakati ambapo umoja na ushirikiano wa binadamu ni muhimu. Hiyo ndiyo sababu kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Binadamu anasimama katika kizingiti cha angani na Mawasiliano na jamii ya mataifa ya waangavu kutoka nje ya dunia. Hii ni hatima yetu. Hili ni tukio kubwa katika historia ya binadamu. Hata hivyo binadamu hayuko tayari. Hiyo ndio sababu kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Hata kwa wakati huu, kuna maingilio na vikosi vya mataifa kutoka nje ya dunia ambayo yanataka kuchukua faida kwa sababu ya udhaifu na magawanyo ya familia ya binadamu. Hata hivyo binadamu bado hayajatambua mambo haya na hajajiandaa. Hiyo ndiyo sababu kuna Mpya Ujumbe kutoka kwa Mungu.

Mawimbi Makubwa ya mabadiliko ambayo yatakuja duniani yanahatarisha maisha ya binadamu na uwezo wa binadamu kuishi kama taifa iliyo huru katika siku zijazo. Hiyo ndiyo sababu kuna Mpya Ujumbe kutoka kwa Mungu.

Watu hawajui ukweli na nguvu ya Knowledge ndani yao, kipaji kikubwa kutoka kwa Muumba kwamba kilichopewa kuongoza na kulinda kila mtu. Hiyo ndiyo sababu kuna ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Kuna hamu kubwa ndani ya watu kila mahali kwa kutaka uhusiano mpya na Mungu. Hiyo ndiyo sababu kuna Mpya Ujumbe kutoka kwa Mungu.

Watu wengi wanaanza kuamka kwa sababu ya haja kubwa ya nafsi yao: haja kwa maana, kusudi na mwelekeo wa maisha yao na haja ya kuchanga duniani. Hiyo ndiyo sababu kuna Mpya Ujumbe kutoka kwa Mungu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umetumwa kutahadhari, kubariki na kuandaa familia nzima ya binadamu. Ujumbe Mpya ni kubwa sana. Inasemea karibu kila kipengele cha maisha yetu. Kwa zaidi ya miaka 25, Mjumbe wake amekuwa akipokea zawadi hii ya binadamu. Na ufunuo unaendelea mpaka leo.

Je, hii ni dini mpya? Kwa nini dunia inahitaji dini Mpya?

Dunia inahitaji uelewa na utambuzi mpya. Kutoka kwa Ujumbe Mpya, aina ya mazoezi ya kiroho na jamii itatokea na, kwa kweli, kutokea hivyo Ujumbe Mpya ni kama dini mpya. Lakini kusudi la Ujumbe Mpya si tu kwa kuunda dini nyingine iliyo katika mashindano au tofauti na dini zote, lakini ni ya kuendeleza uelewa wa binadamu kuhusu ukweli wa kiroho, changamoto zake kubwa katika dunia na hatima yake katika dunia ya waangavu.

Ubunadamu unahitaji uzoefu na uelewa mpya wa nia ya Mungu, lengo na uhai wake duniani, wa mabadiliko makubwa yanayokuja na pia kuhusu mataifa kutoka ulimwengu yanayotisha kudhoofisha umoja, uhuru na enzi ya banadamu duniani.

Dunia basi haihitaji dini mpya kama vile inahitaji uelewa mpya na ufahamu na ahadi mpya ya umoja wa binadamu inayokabiliwa na mabadiliko makubwa ya kudhoofisha. Hii sio tu wazo nzuri. Hii sio tu maadili kanuni. Hii ni muhimu kama ubinadamu utaweza kuishi na kubaki huru.

Ni jambo la muhumi peke yake inayoweza kuita Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani. Hi haja kubwa peke yake inayoweza kuita agano mpya duniani.Ni hali ambayo binadamu hawezi kujiandaa mwenyewe peke yake inayoweza kuita Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu na pamoja nayo, maandalizi yanayowezesha watu kupata uzoefu na uelewa huu mpya, unayohitajika duniani kwa sasa.

 

Ni nini Ujumbe Mpya unahitaji kutoka kwangu?

 

Ujumbe Mpya unahitahi uaminifu, ukweli, uadilifu na uazimaji- yale yote ambayo kila mtu anahitaji kujenga katika maish ayake na kla kitu kinacho hitaji kuwa imara katika jamii na kaya, miji na mataifa ya dunia.

Ujumbe Mpya unahitaji uheshimu unachokihitaji na kile dunia inachokihitaji. Inahitaji ugundue na upokee baraka ya Mwumba na ile maandalizi Mwumba ametuma duniani kwa ufaida ya binadamu.

Kama hii inalemea mtu yeyote, basi watu hao hawajatambua mahitaji yao. Hawajatambua mahitaji ya roho yao na mahitaji ya moyo wao. Wanajishugulisha na kile ambacho wanataka na kile ambacho wanakiogopa. Hawaja_ka mahali pa kugundua wanahitaji kutafuta dhamira muhimu katika maisha yao.

Wanahitaji kuchanga ili waweze kuridhika na kuwa na furaha. Wanahitaji kuchangia kwa kingojo cha dunia ndio maisha yao yawe muhimu, ya maana na ya dhamira

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu unahitaji ugundue haja ya Ujumbe Mpya, usome Ujumbe Mpya, uwaze na utimize maelekezo yake.

Unahitaji upokee baraka yake, faida yake, nguvu yake na uwezo wake katika maisha yako.

Unahitaji ushiriki Ujumbe Mpya na wengine na kuuweka kwa hali sa_, bila kuubadilisha au kuugeuza au kujaribu kuuoanisha na kiti chochote.

Kwa asili, unaulizwa kuupokea Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu na ushuhudie Ujumbe huu. Na ukiweza kupokea baraka yake, unaulizwa utetee Ujumbe huu na utetee ulinzi wake duniani.

Kwa hivyo Ujumbe Mpya unahitaji ukipokee kile unachokihitaji na kile dunia kinahitaji. Iwache hii ile uelewa wako

Kufahamu Mungu

Sasa ni wakati wa ufahamu zaidi wa Mungu na kupanua uelewa wa Mungu. Mungu ndiye chanzo cha na mwandishi wa maisha yako na maisha ya wote duniani na katika Jumuiya Kuu ya mataifa yote ambayo wewe huishi. Uelewa huu mpya sio wa kukosoa uelewa wa awali, ila ni wa kuupanua, kuukamilisha zaidi na kuuwacha mlango wazi kwa ufarisi wa mapenzi ya Mungu hudhurio ya Mungu katika maisha yake.

Kwa kuwasilisha Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu, ni muhimu basi kufufua ufarisi huu wa Mungu- kuufufua, ili kuutenganisha na yale yote am-bayo taasisi za binadamu na uvumbuzi ule binadamu alioongeza, na kuuleta katika lengo kubwa zaidi na na kwa uwazi kwako.

Hapa ni muhimu kutochanganya Mungu na dini, kwa sababu mambo mengi ya kutisha yalifanywa kwa jina la dini na kwa jina la Mungu. Lakini Mungu huishi mbali zaidi ya mambo yote haya, mbali zaidi ya makosa ya binadamu,mbali zaidi ya mawazo ya binadamu, mbali zaidi ya uvumbuzi wa binadamu na mbali zaidi ya ufisadi wa binadamu.

Sasa ni muhimu kwako wewe kufikiria Mungu ndani ya uwanja mkubwa wa waangavu ambao wewe unaishi, ambao umo pamoja na maisha yote duniani na unaelekea zaidi ya dunia hii, ndani ya Jumuiya kuu ya Mataifa yote.

Kuwa na uzoefu safi wa ukeli wa Mungu na mapenzi ya Mungu kwa maisha yako, lazima upate ufahamu huu mkubwa, kutoka kwa Jumuiya Kubwa, wa Mungu. Ila, unaweza kufikiria Mungu kama makadirio ya maisha yako mwenyewe na asili ya mwanadamu, kama makadirio ya hisia yako mwenyewe, mawazo na maono yako. Utasihia kwa Mungu hasira yako, mapendekezo yako, hukumu yako, mapendekezo yako ya kulipa kisasi, mawazo yako ya haki na adhabu na kadhalika.

Hata hivyo, Mungu huishi zaidi ya haya yote. Mungu wa ukweli, Mungu wa usafi ambaye amekuwa anang`aa kama jua juu yako. Bila kujali mawingu angani, bila kujali uchafuzi wa mazingira katika anga na bila kujali masumbuko katika ardhi. Mungu ni kama jua inayong`aa juu yako. Lakini Mungu huishi zaidi ya jua, zaidi ya ufafanuzi wowote unayoweza kufikiria, Zaidi ya historia yako, zaidi ya walimu wakubwa na watumwe wakubwa kutoka kwa Mungu, zaidi ya vitabu vikubwa vya kiroho na ushahidi, kuna Mungu, Muumba na mwandhishi wa maisha yako.

Kile Mungu alichokiunda kinaishi ndani yako. Kinaishi zaidi ya akili yako, zaidi ya fikira yako na ufahamu wako, zaidi ya dhana yako, zaidi ya mawazo yako na imani. Inaishi ndani yako, katika akili yako ya ndani, na Ujumbe Mpya unakiita Knowledge. Akili hii ya ndani ndiyo akili inayojua. Ni akili inayongojea.

Ni akili ambayo huona wazi bila kuvuruga, bila hofu, bila upendeleo, bila fujo na bila uvumi. Ni akili inayoishi ndani yako. Hii ndiyo Mungu aliyeumba ndani yako ambayo itadumu, ambayo itadumu milele.Zaidi ya utambulisho wa muda wako katika dunia hii, zaidi ya matukio yote ya dunia hii na zaidi ya uzoefu wako katika maisha haya, kuna Knowledge ndani yenyu, na Mungu ndiye mwandishi wa Knowledge hii.

Ukimfikiria Mungu katika muktadha huu mkubwa, unaweza kuanza kufahamu nguvu na ukuu wa uumbaji wa Mungu ndani ya ulimwengu na hata ndani yako mwenyewe. Mwili wako, akili yako na utu wako ni magari ya muda ambayo lengo lao ni kueleza uhusiano wako na Mungu na hekima ambayo Mungu amekupatia ili uweze kuwasiliana na kuchangia katika dunia wakati wa haja.Fikiria basi kama mwili wako, akili yako ni magari ya kueleza, na zina thamani,lakini sio muhimu kama kile ambacho zinafaa kueleza na kutumikia.

Basi utaanza kuona kwamba Mungu anaruhushu vitu vyote, Mungu anaishi ndani ya kila kitu, na bado Mungu ni zaidi ya kila kitu. Unaweza kuhisi uwepo wa Mungu popote ulipo, na unaweza kupata na kufuata Maarifa popote ulipo.

Kwa hiyo, kuelewa na kuhisi Mungu ndani ya maisha yako, lazima ukuje kwa Knowledge ndani yako, ambayo ni akili zaidi, ile ambayo itayodumu, ambayo Mungu ameumba ndani yako na kwa ajili yako. Knowledge ni asili yako ya ukweli. Zaidi ya mawazo yote, fikira na ndoto, ni asili yako ya kweli. Ni kwa kupata uhusiano na Knowledge, kwa kujifunza kupambanua Knowledge kutoka kito chochote na kufuata Knowledge ndio utaweza kujufunza na kutambua ufarisi wake, nguvu yake na mapenzi ya Mungu katika maisha yako.

Hata hivyo ujumla wa Mungu utakuwa milele zaidi ya dhana ya akili, zaidi ya uvumbuzi wote wa binadamu na zaidi ya filosofia zote za mtu binafsi na za watu wote. Ni seti gani za mawazo na dhana zinazoweza kufafanua Mungu wa Jumuiya Kubwa, Mungu ambaye ni mwandishi wa mataifa ya viumbe visiyoweza kuhesabiwa katika ulimwengu, mataifaa ya kipekee na tofauti na nyengine kwa njia nyingi?

Kukuja kwa Mungu basi ni kukuja kwa Knowledge ndani yako, kwa sababu Knowledge ndiyo itakayokuita kwa Mungu. Labda utaitwa kuenda mahali fulani au kwa mtu fulani, lakini ni kwa kusudi hii- kwa ufarisi wa uwepo wa Mungu ndani yako. Kwa sababu utahitaji zaidi ya imani kufahamu, kuelewa na kufuata kile ambacho Mungu amewapa kuona, kujua na kufanya.

Wacha basi hii iwe chanzo chako, ambapo utachukua hatua kwa Knowledge, ambapo utachukua hatua kwa Mungu. Ufanye hivyo hata kama wewe ni Mkristo, Buddhist, Muislamu au unafuata imani yeyote unayozingatia. Hata kama hauna imani, bado kuna hatua kwa Knowledge. Mungu ndiye alieumba dini zote duniani, na Knowledge ndiyo ambayo inayounganisha dini zote, licha ya matengano na vita zilizopo kati yao. Kwa kuwa matengano na vita ni uvumbuzi wa binadamu sio uzushi wa Mungu.

Wito unaduta ndani ya mila hizi zote-ndani yao na hata zaidi yao. Ni wito unaopatikana katike ulimwengu, unaoviita vyumba yva Mungu virudi kwa nguvu na hadhara ya Knowledge, kugundua kile Knowledge alichowapangia, kuona na kujua. Hii inaanzisha kurudi kwa Mungu– wito, kusikiliza, kukabiliana na kurudi.

Wacha basi huu uwe uelea wako