Ujumbe Mpya uko hapa kutoa ahadi na nguvu kubwa kwa bunadamu. Nguvu ya Knolwedge ambayo Mungu ameiweka ndani ya kila mtu ni majaliwa makubwa, majialiwa yanayosubiri kugunduliwa.
Ubinadamu bado haujagundua nguvu yake iliyo kubwa zaidi na uwezo wake mkubwa, uadilifu wake mkubwa na maadili yake makubwa ya msingi. Bado unalalamika, kama tamaduni haijakomaa, ikiendeshwa na uchoyo na uroho, chuki na hukumu. Bado haijakomaa katika kile ambacho kinatumikia na kinafuata. Lakini hii haikani ukweli kwamba ubinadamu una uwezo mkubwa ambao bado haujagundua na haujaendeleza.
Mwumba wa maisha yote ametuma Ujumbe Mpya duniani kutayarisha binadamu katika Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yanayokuja duniani na kutayarisha binadamu katika makutano na ulimwengu wa waangavu. Lakini matayarisho haya yanahitaji binadamu agundue na aendeleshe nguvu yake kubwa na uadilifu wake mkubwa.
Lakini binadamu kwa jumla hiawezi kufundishwa ama kutayarishwa mara moja, kwa kuwa mafundisho yanatokea kwa mtu binafsi. Kuleta mtu binafsi katika ufahamu wa nguvu yake zaidi na uwezo zaidi na uadilifu wake zaidi ndipo mbegu zitapandwa na ahadi ya binadamu imo. Kwa hivyo, usifikiri kile watu wote wanafaa kufanya, ama daima utakata tamaa. Yafikirie basi yale yako mbele yako.
Jamii na tamaduni zako labda zinataka tu utumbikie katika matumizi ama utumbukie katika kazi, mwanachama wa kikundi, mteja wa maadili ya utamaduni na vipaumbele. Lakini una ahadi kubwa zaidi katika maisha, ahadi kubwa iliyo na hakika kwa sababu ni sehemu ya asili yako ya ndani. Katika utamaduni, asili yako ya ndani husahaulika ama hupuuzwa na katika kesi zingine, hukanwa kabisa. Lakini huwezi kukana asili yako ya ndani milele, kwa kuwa inaishi ndani yako zaidi ya ufikio wa utamaduni, zaidi ya ufikio wa ufisadi, zaidi ya ufikio wa ghiliba na udanganyifu. Hiyo ndiyo sababu nguvu hii ya ndani ni nguvu yako kubwa na ina uwezo wako mkubwa na dhamira yako kubwa zaidi ya kukuja ulimwenguni.
Kile kilichohifadhiwa kwa wasomi hapo awali, kwa wajuzi lazima kiwe kama mlangu ulio wazi kwako na kwa watu wengine duniani. Kwa kuwa dunia inakabiliwa ya majaribio makubwa, hatari kubwa. Binadamu hajajitayarisha kwa Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Binadamu bado ni mjinga na mpumbavu katika maoni yake na mtazamo kuhusu matarajio ya waangavu ulimwenguni. Kwa hivyo ahadi ya binadamu ni ahadi ya mtu binafsi, kuamka kwa mtu binafsi. Hii ndiyo itampa binadamu nguvu kubwa zaidi ya msingi na uwezekano mkubwa kwa mazoezi ya hekima halisi ikikabiliwa na mustakabali haitabiriki na isiyo na hakika.
Ndiyo watu waweze kukabiliana na ufunuo wa Mungu, ni lazima watambue kwanza kuwa hawawezi kujitimiza wenyewe kutumia tabia zao za kawaida, tafrija na mabirudisho yale watu walio karibu nao wamejitolea. Ni lazima watambue wana haja kubwa na uwajibikaji zaidi katika maisha. Hii itaoneshwa hapo awali kupitia mateso yao na kuvunjika moyo kwao na dunia inayowazunguka wakizidi kupoteza maslahi katika michezo na burudani ya watu walio karibu nao kwa sababu wana haja zaidi ambayo sasa inajitokeza.
Kama wameridhi mahitaji ya mwili kupitia chakula, malazi, mavazi, na usalama; kama wmeridhi mahitaji ya akili kupitia upatikanaji wa elimu na fursa, basi haja kubwa itaanza kujitokeza ndani yao. Hii ni haja ya roho, ambayo inaweza tu kutimizwa kwa kutambua, kukubali na kutimiza dhamira yako kubwa iliyowaleta hapa-ambayo ni kitu ambacho kinaishi zaidi ya eneo la akili. Huwezi kuiwaza, lakini unaweza na ni lazima ufarisi nguvu hii. Na ina subiri kugunduliwa.
Kuwa mtu wa Ujumbe Mpya, lazima utambue kwamba ubinadamu unaingia katika zama mpya na kizingiti kikubwa na kisicho na uhakika. Hamuwezi tu kutegemea mafundisho ya kale au maagizo ya kale au unabii wa zamani sasa uwaongoze katika siku zijazo. Kwa maana dunia imebadilika na mabadiliko yafanyika haraka, lakini watu hawajabadilika nayo na wala hawaoni haja ya kubadilika. Mtu wa Ujumbe New basi lazima atambue kwamba yeye anasimama katika kizingiti cha mabadiliko makubwa katika hali halisi ya dunia, katika hali ya maisha ya hapa na katika ugunduzi kwamba upweke wao ulimwenguni umeisha, na kamwe hawatakuwa nao tena.
Dharuba hapa itakuwa kubwa, lakini ni dharuba iliyo na dhamira. Kwa kuwa inakuongoza kwa ugunduzi mkubwa unaoweza kuwa nao maishani, huo ni ugunduzi wa nguvu na uwepo wa Knowledge ndani yako – akili zaidi, akili kubwa, akili iliyo na nia na umakini, akili isiyo aliwasihi au kushawishiwa na dunia, akili iliyo safi na isiyo ya ufisadi, akili ambayo haiwezi kupotoshwa na dunia katika vishawishi vya dunia na majanga.
Ufunuo Upia unayataja haya kwa sababu binadamu lazima apate huduma kutoka kwa uwezo wake mkubwa zaidi, nguvu zaidi na uadilifu mkubwa. Kama hataweza kufanya hivyo,atashindwa akikabiliwa na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, na atashindwa kwa sababu ya udanganyifu na wa vikosi vya kutoka ulimwengu ambavyo viko hapa kuchukua faida kotokana na udhaifu wa binadamu na binadamu isiyo na umoja.
Kwa sababu ya hatari kubwa kwa utamaduni wa binadamu na ustawi na uhuru wa familia ya binadamu, Muumba wa uhai wote ametuma Ujumbe Mpya ulimwenguni, Ufunuo mkubwa kama Ufunuo wowote uliotumwa hapa.Upo hapa katika fomu safi, haujapotoshwa na serikali, haujapotoshwa na watu binafsi wenye tamaa, haujaunganishwa na utamaduni na siasa na nia ya chini ya ubinadamu.
Mtu wa Ujumbe Mpya anatambua kuwa anaishi wakati wa Ufunuo, wakati ambapo Ufunuo unahitajika kama watu karibu nao – hata katika nafasi ya uongozi katika serikali – wanaonekana kuwa hawajibu ishara ya dunia na kuibuka kwa mabadiliko makubwa.
Uwezo wa mtu binafsi kufanya maandalizi, kupata huduma kutoka kwa nguvu ya Knowledge na kufuatilia jambo hili kwa uaminifu – bila ya kujaribu kudhibiti au kuendesha akili hii kubwa – ni changamoto kubwa na fursa. Na bado inawakilisha ukombozi kwa mtu binafsi kwa sababu ni kwa kupitia njia ya Knolwedge ndiyo utaweza kuunganishwa tena na Mungu, ndio utagundua upya kwamba una dhamira kubwa zaidi maishani na uwezo wa kufuata hatua ya ufunuo wake, ufunuo binafsi.
Hapa unatambua kuwa wewe ni mwaanzilishi. Unakifanya kitu kipya. Uko katika mwanzo wa harakati kubwa sana, mabadiliko makubwa. Kama mwaanzilishi, utakabiliwa na upweke na ukosefu wa kutambuliwa na wengine. Lazima ujenge nguvu yako mwenyewe na dhamana na wengine ambao wanakabiliana na Ufunuo.
Hapa unatambua kuwa huna jibu ya siku zijazo, na huna jibu ya maisha yako, na majibu yako ni majibu yote uliopewa na utamaduni. Hata majibu ambayo unahisi una umba bado majibu yaliotolewa na wengine. Lakini kuna jibu moja tu, na kwamba ni kujiandaa kukabiliana na dunia ya mabadiliko makubwa. Ni kuiandaa maisha yako na akili yako ya itumikie katika uwezo wa juu. Ni kwa kupitia maandalizi makubwa ambayo haukuunda mwenyewe, lakini ambayo uliyopewa kupitia neema na Providence.
Hapa unavunja minyororo ya tabia ya upotovu unayoshinda ukirudia, haja ya idhini na kuzingatia utamaduni na dikteta ya taifa lako, kwa dhamana na kuungana na Nguvu Kubwa na uwezo ambao ni chanzo cha maisha yote katika Ulimwengu. Na unafanya hivyo kwa unyenyekevu, na haujitangazi, kwa maana unajua Nguvu Kubwa sio yako ya kutumia au kudhibiti. Lakini una heri kwa kuipokea na kuiruhusu ijenge maisha upya na mwelekeo wako ili utimizo halisi na uridhiki uweze kupatikaka kwako.
Basi, unajitayarisha, kuwa mume au mwanamke wa Knowledge – sio tu kwa ukombozi wako na utimilifu, lakini kwa kuchangia sehemu yako wakati wa kipindi cha mpito mkubwa duniani. Haujui maana ya hii au umuhimu wake. Labda utadhani utakuwa kiongozi mkubwa, lakini watu wachache tu ndio watakuwa viongozi mashuhuri. Utachangia tu katika sehemu ambayo ikuchukua sura na umbo ukiendelea na kama mahusiano yako na watu wengine yatapata ufafanuzi zaidi na uaminifu mkubwa.
Wewe ni mtu wa Ufunuo Mpya, na wewe unapata uhuru na huzuliwi na siku za nyuma, kwa maana unabeba mbegu ya siku zijazo. Unabeba chombo cha siku zijazo. Haitoshi tu kuishi kwa muda mfupi, kwa kuwa hiyo ni nusu tu ya maana ya maisha. Lazima pia ujiandae kwa siku zijazo, na Knowledge ndani yako inajua jinsi mustakabali utakuwa na jinsi utaweza kujiandaa kwa busara, ufanisi na kwa usalama.
Njia kwa kweli ni rahisi kabisa, lakini kwa sababu imo nje ya eneo la akili, watu wanaweza kuwa na mashaka sana na kuchanganyikiwa kuihusu, kujaribu kumechi ukweli wake na imani yao ya sasa na mitazamo. Na bila shaka imani yako ya sasa na mitazamo ni vuimbe vya utamaduni na mara nyingi ni bidhaa ya hofu. Hayalingani na hali halisi ya maisha yao kubwa zaidi. Hayo ni mabaki tu ya zamani na ya utambulisho wa zamani, ambao bado wanabeba na lazima wajifunze kuyawacha.
Kuwacha utambulisho huu ni jambo la kawaida kabisa. Ni kama kuwacha ujana na kuwa mtu mzima. Kama kijana, unajitambua na umri yako na vijana wengine, na unashawishiwa na maadili yao na shughuli zao. Lakini ukiwa mtu mzima, vipaumbele vyako hubadilika. Unapanieni mambo ya maana na thamani kubwa zaidi, na kujitolea katika majukumu zaidi maishani. Kwa hivyo ni hapa unawacha utambulisho wako wa zamani. Unachukua wajibu mkubwa, na unatafuta maana zaidi. Shughuli za zamani zinaonekana ni kama zinakosa na hazitoshi kwa mahitaji yako ya ndani zaidi.
Hii ndio kukomaa kiroho. Hii ndio maana ya kuendelea kutimiza ngazi ya mahitaji ya ndani yenu. Na hii ndiyoinakuunganisha na dunia na wale waliokutuma hapa. Ni hapa unapata utimilifu wako mkubwa ndani ya uadilifu wako, ndani ya ubora wa mahusiano ambayo sasa yataanza kukuja kwako na kwa hisia ya maana itakayoenea katika maisha yako.
Kile kilichokuwa cha kuepuka hapo awali sasa kinakuwa muhimu zaidi kwa mtazamo wako. Mazoezi ya kiroho sio tu aina ya kutolewa shinikizo. Kinakuwa sasa msingi wa kujenga nguvu, lengo kuu la shughuli zako. Hapa unaleta mazoea yako ya kiroho katika kila kitu unachokifanya kwa sababu ni muhimu kwa kila kitu unachokifanya, na yatakusaidia na kuleta uwazi katika kila kitu utakachokifanya.
Hapa hakuna dhabihu ya kweli. Unayawacha yale ambayo yanaonekana kuwa yanakosa au hata ni pumbavu, yale ambayo yalikua muhimu kwako hapo awali. Watu wengi kamwe hawakui wakubwa katika mambo yanayohusu kiroho, na hivyo hubaki katika hali ya utoto au ujana kiroho. Ingawa wana mvi na kuwa wenye umri wa miaka mengi kimwili, kamwe kweli hawakui wakubwa katika mambo yanayohusu kiroho. Lakini mchakato wa ukuaji ni sawa-kukiacha cha zamani, uibuka wa kipya, maumivu ya kuongezeka ya kuwa mtu wa kuwajibika, mtu wa uwezo zaidi, na nafasi kubwa ya kufarisi mahusiano katika eneo ya juu ya dhamira katika maisha, ambayo ni kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kimo nje ya uwezo wa wengine ambao bado maendeleo haya hayajitokeza kwao.
Mtu wa Ujumbe Mpya anatambua kuwa yeye ni sehemu ya kitu kikubwa kinachojitokeza. Hawana haja ya kuona hitimisho au matokeo, kwa kuwa imo nje ya uwezo wao na zaidi ya maono yao. Si wajibu wao kuhakikisha matokeo, lakini kuchangia sehemu yao kwa harakati ya binadamu katika mwelekeo chanya. Na ubinadamu unaweza vipi kusonga katika mwelekeo chanya bila msaada mkubwa ambao Muumba wa uhai wote anautoa? Ni dhahiri ya kusikitisha kuwa binadamu hawezi kufanya hivyo mwenyewe, au hataki, vile kesi ilivyo.
Watu huomba Mungu awasaidie, awape nafasi, awakomboe, waepuke maumivu na mateso, awape upya au ufufuo. Lakini Ujumbe ukikuja kwa fomu kubwa kama hii, hawaoni, wala kujibu au wanakana jambo hilo kwa sababu haithibitishi na haitimilizi matarajio yao au imani yao ya awali.
Kama kweli unataka Mungu akusaidie, basi ni bora uwe tayari kubadilisha maisha yako. Mungu atakusaidia kabisa. Kama huna uhakika unaitaka, basi labda uwache kuomba na kusema affirmations zako.
Watu wa Ujumbe Mpya lazima wamusaidie Mtume wakati yeye bado ako duniani. Kazi yake ni kubwa mno. Ni kubwa zaidi kuliko kile mtu mmoja angeweza kufanya. Lazima waushuhudie. Lazima wauwakilishe. Lazima wawe na ujasiri wa kuwa sehemu ya Ufunuo na si tu waangalizi wake au watazamaji wake.
Nguvu ya Ufunuo kurejesha ubinadamu na kuandaa ubinadamu utahitaji matendo ya watu wengi. Ufunuo ni safi. Haujapotoshwa. Umetolewa kikamilifu. Mtume hajafariki na nusu Ujumbe mikononi. Muumba wa maisha yote amekihakikisha hicho. Kila kitu kiko mahali pake.
Ufunuo anasemea hali halisi tofauti ndani ya watu. Hauridhishi akili yao au kiburi wanachomiliki. Hauingiliani na virahi vyao na mawazo yao yasio kamilifu au sahihi. Haujafungwa na upendeleo wa binadamu au nia ya binadamu, kwa hivyo unaonekana ni wa ajabu lakini no confounding, mpya na tofauti lakini kwa kiasi fulani wa kale na usiyo na wakati.
Mtu wa Ujumbe Mpya lazima awe sehemu ya Ujumbe Mpya. Hawawezi tu kuwa mlaji ambaye atauiba na kutoroka nao na kujaribu kuutumia kujenga utajiri, au nguvu binafsi au kupata faida binafsi. Kama wezi usiku, wataiba na kudai kuwa nguvu ya Ujumbe Mpya ni nguvu yao wenyewe na faida ya Ujumbe ni faida yao, uandishi wa Ujumbe Mpya ni uandishi wao. Utaona jaribio la jambo hili, ndiyo, kwa sababu ubinadamu kwa jumla una ufisadi mno na hauwezi kukabiliana na jambo hili safi, hii ndiyo maana mtu binafsi ndiye lengo shabaha na sio raia wote wa dunia.
Ni watu wakijifunza na kuishi Ujumbe Mpya ndio watakuwa na uwezo wa kuhamisha na kutafsiri nguvu na hekima yake ndani ya familia zao, jamii zao, mataifa yao, dini zao, kila kitu-wakileta mabadiliko katika mtazamo wa binadamu ambao utatokea pole pole na kwa mdua.
Watu wataanza kufikiria kwamba wao ni wenyeji wa dunia hii na lazima waanzishe kanuni zao za ushiriki kuhusu kujiliwa na kuingiliwa. Bila shaka, ni dhahiri. Watu watasema, “Bila shaka, hatuwezi tu kuwacha mtu yeyote aje hapa na afanye chochote anachokitaka. Na hatutaruhusu tuambiwe kuwa vikosi hivi viko hapa kutuokoa au kutukomboa.”
Bila shaka. Itakuwa ni kama akili ya kawaida katika wakati huo, lakini kwa wakati huu, inaonekana kuwa ni ya ajabu na haiwezekani. Yawezekanaje hivyo? Kwa sababu watu bado wanafikiri kama tamaduni haijakomaa. Bado wanafikiri kuwa wako peke yao ulimwenguni. Hawaifikirii mustakabali. Hawaoni kuwa ubinadamu tayari umenyonya dunia kwa kiasi itakuwa vigumu kuwa na uwezo wa kujilisha katika siku zijazo, na hivyo umesababisha Mawimbi Makuu ya Mabadiliko.
Ahadi iko kwa mtu binafsi, na hii daima imekuwa ndiyo kesi. Ufunoa wote mpya, maboresho yote mapya, ubunifu na hatua kubwa katika sayansi, biashara na haki za kijamii zimekuwa zikiendeshwa na watu binafsi ambao walivuviwa na kujitolea kwa huduma yao. Hivi ndivyo jamii zote katika ulimwengu zinaendelea na zina ahadi.
Kwa mtu wa Ujumbe Mpya, ana wajibu mkubwa hapa, pengine ni ana wajibu kubwa zaidi kuliko kitu chochote ambacho wamewahi kukichukua. Baadhi ya sehemu yao bado inataka kwenda mbali na kuwa na furaha na kuishi maisha ya ustaarabu mahali fulani, kuishi maisha ya aina ya uvivu, maisha ya kutokuwajibika. Lakini ndani yao kunajitokeza nguvu na uwezo na sauti kubwa na hali ya kujutolea na mwelekeo ambao sasa unakuwa mfumo wao na mazingira yao.
Wameshikamana na siku zijazo. Wameshikamana na Jumuiya Kubwa. Wameshikamana na muda wao na nyakati zijazo. Wanaanza kujibu kama wao kwa kweli walitumwa duniani kutimiza kitu fulani katika mahusiano na watu wenginne. Wanaanza kufikiri na kujisikia kama viumbe vinavyoishi milele na vilivyo hapa kutoa huduma katika mazingira ya muda mfupi na ya wasiwasi.
Lakini kufikia katika ufahamu huu na nguvu ya ukweli huu inahitaji dhamira kubwa na maandalizi. Huwezi kukabili jambo hili shingo upande. Huwezi kuwa na papara au manipulative au kuendeshwa na mapendekezo yako, ama hutaweza hata kuwa na uwezo wa kuanza. Utashindwa katika changamoto ya kwanza au kikwazo, jaribio la kwanza litafanya ukate tamaa, ukijua watu walio karibu nawe wale ulidhani walikuwa marafiki na walio karibu nawe kwa kweli kuwa hawana kidokezo au hawataki kushughulika na mambo haya na watakukana ukijitangaza.
Hapa unatambua kuwa una uchaguzi. Unaweza kufuata nguvu inayojitokeza ya Knowledge, hata kama hauielewi, ama utaendana na mahitaji na matakwa ya familia yako au marafiki. Watu wengi hushindwa katika hatua hii, wanajiunganisha tena ndani ya amnesia ya utamaduni, na tabia ya upotovu wanayoshinda wakirudia ya utamaduni, kwa ushawishi wa utamaduni. Waliamka kwa muda mfupi, halafu wakashindwa na nguvu za mazingira ya akili karibu nao, zilizo wanyakua – katika vivinyovinyo, katika kutowajibika, katika ndoto.
Lazima sasa uushugulikie wito wako na maendeleo na maendeleo ya wengine karibu na wewe ambao unawajua, ambao wana uwezo wa kukabiliana na Ufunuo Mpya maishani. Lakini huwezi kupanda mlima huu ukisubiri wengine. Lazima wewe mwenyewe uupande mlima huu, hata kama marafiki wako wa dhati hawawezi kuenda nawe. Unaweza kusaidia dunia na kuwasaidia kama unaweza kupaa na kufunga safari hii zaidi kuliko vile unaweza kuwasaidia ukikaa nyuma na kuwatia moyo.
Kuna hekima nyingi na uwazi wa kupatwa njiani. Kiasi chake hakiwezi kuonekana wakati huu, lakini kinakusubiri katika safari yako. Na huwezi kujifunza mambo haya isipokuwa ufunge safari hii. Huwezi kujifunza hayo kama amri au kama mawazo, kwa sababu huwezi kumiliki uwezo uliopo, kuufuata na kuuonyesha.
Mtu wa Ujumbe Mpya ni sehemu ya Ujumbe Mpya kama mchangiaji, bila kujaribu kufafanua jukumu lako au kudai mamlaka au kudai nafasi yako mwenyewe. Hii itahitaji mpango mkubwa wa kujizuia kwa upande wako, kwa ajili haya maelekeo yote bado yamo ndani yako-mbegu za uovu, mbegu za uchoyo, mbegu za udanganyifu, mbegu za udanganyifu wa kibinafsi – zote ziko hapo. Mbegu mingi zimo hai ndani yako wakati huu. Kwa hivyo lazima uzuie haya yote na urejee Knowledge na kuomba msaada kutoka kwa watu wengine ikibidi.
Kwa maana hautaki kupoteza wito huu. Umetoka mbali sana. Hutaki kushindwa. Tayari umeongozwa nje ya obsessions za utamaduni kwa kiwango kikubwa. Hutaki kushindwa katika kutekeleza azma hii, fursa kubwa unaweyoza kuwa nayo-wewe ambaye umeteuliwa na una bahati kubwa mno, na bahati ya kuwa miongoni mwa wa kwanza wa kupokea Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.
Je, unakitambua kilicho mbele yako? Je, una wazo lolote? Katika deprecation yako ya kibinafsi, unaweza kukiona kilicho mbele yako? Mungu amekupa njia, njia ya kutoka mwitu, maze isiyo na matumaini ya vivinyivinyo vya binadamu na maelewano ya binadamu.
Kwa hiyo, usivunjike moyo. Kaa pamoja na maandalizi yako na mazoezi. Wache ishara za dunia zikuambia nini kinachokuja, na uwache ishara ndani yako izuie tabia yako mbaya ya kithiri na jinsi unajilaumu – bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa usahihisha binafsi ule lazima uwe nao katika mawazo yako, dhana zako na tabia yako. Mwalimu mwenye busara hawaadhibu wanafunzi, lakini tu husahihisha wanafunzi wake. Hivi ndivyo lazima ujifundishe. Hivi ndivyo jinsi mzazi mwenye busara na upendo hufundisha mtoto wake aliye kijana bila hatia.
Wewe ni kama mtoto sasa katika kuendeleza ufahamu wako ya Jumuiya Kubwana na katika kugundua nguvu ya Knowledge. Umo katika hatua ya mwanzo, na kuna barabara kubwa mbele yako. Hatimaye, una dhamira, maana na mwelekeo. Lakini ni lazima ukae na hili na usiepushwe na vikwazo, masumbuko na mawazo ya zamani na imani zinayoleta mawingu kwa akili yako, mawingu yanayoweza kufanya upoteze njia yako juu ya mlima. Usitongozwe na sehemu nzuri za kuburudika njiani, kwa kuwa una hatima na safari ya kuchukua. Hivi ndivyo Mungu atakukomboa, kwa njia ambayo kamwe hungeweza kujikomboa.