Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya, mwelekeo ambao binadamu hajawai kuupitia. Kwa kuwa dunia imebadilika na binadamu anakabili Jumuiya Kubwa ya waangavu ulimwenguni – mabadiliko makubwa, kizingiti kikubwa katika evolution ya binadamu, wakati wa mageuzi makubwa na wasiwasi, wakati wa hatari kwa familia ya binadamu, wakati ambao utasonga kwa haraka na matukio yatayojitokeza kwa haraka.

 

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya, katika mwelekeo wa jamii ya dunia ambayo ina uwezo wa kuendeleza dunia na kukabiliana na hali halisi ya maisha katika ulimwengu, ambayo itabidi mukabiliane nayo na hata kwa sasa munalazimishwa kukabiliana nayo.

 

Ni mabadiliko makubwa ambayo watu wengi wanayahisi lakini hawayaelewi. Harakati ya dunia inatokea kwa kasi, ambapo maisha ya watu itakuwa ya kuzidiwa na ya kushindwa katika mabadiliko makubwa ya mazingira ambayo yanajitokeza kwa njia ya mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Haya yote sasa yako katika mwendo na hayawezi kupunguzwa, inaweza tu kuwa tu kuwa mitigated. Hapa watu wanaweza tu kukabiliana nayo.

Ni katika kizingiti hiki kikubwa katika historia ya binadamu kuwa Ufunuo Mpya umemtumwa duniani, na Mtume ametumwa hapa kuupokea, kuuandaa Ujumbe huu na kuueleza. Kwake, safari hii ilikuwa ndefu, safari ndefu na ngumu.

Ujumbe wa ubinadamu sasa ni mkubwa, ni mpana zaidi na ni kamilifu zaidi kuliko Ujumbe wowote uloyowahi kumtumwa duniani, kamili na mafundisho na ufafanuzi ili hekima yake na Knowledge yaweze kuonekana na kutumiwa ipasavyo na si tu kuachwa kwa utafsiri wa binadamu.

Watu hawaoni, hawasikii. Hawajijui wenyewe. Na ujuzi wao wa asili wa kutambua mazingira, kwa wengi, umepotea na haujakuzwa.

Hii inafanya kazi ya Mtume iwe ngumu zaidi. Yeye lazima abebe fumbo, kwa kuwa Ufunuo umo zaidi ya eneo la akili na kwa hakika hailinganishwi na matarajio ya watu, imani au ufahamu.

Mungu anaongoza dunia katika mwelekeo mpya. Ni mwelekeo ambao ulikuwa ni hatima ya binadamu, lakini utakuwa mpya kwa watu wa dunia. Utakuwa mpya kwa uelewa wao.

Mafunuo yote kutoka kwa Muumba daima huwa kama hii. Yote huwasilisha ukweli mpya, mwamko mpya, mwelekeo mpya na ahadi kubwa zaidi.

Giza inaongezeka duniani, na ahadi hii kubwa zaidi inahitajika sasa. Ni mwangaza wa Knowledge peke yake, akili kubwa ile Muumba ameitoa kwa familia ya binadamu na kwa jamii zote ulimwenguni, inaweza sasa kuwawezesha muelewe na mujibu.

Kwa kuwa unarudi kwa Mungu kwa masharti ya Mungu, Ujumbe wa Mungu lazima ueleweke, kama vile ulivyo na vile lengo lake liko.

Kutakuwa na mapambano na ubishi kuhusu haya, na Mtume na wafuasi wa Mtume lazima wakabiliane na ugumu huu, kuchanganyikiwa huku na wawe na uvumilivu mkubwa.

Ufunuo kama huu hautakubaliwa hapo awali, na ni wachache tu watakuwa na uwezo wa kujibu kabisa. Lakini wakati ukiendelea na dunia ikizidi kuwa na matata, Ujumbe Mpya utapata kivutio kikubwa, utambuzi mkubwa na umuhimu mkubwa.

Unayajibu maswali ambayo bado hamujajifundhisha kuyauliza. Ni maandalizi ya mustakabali na pia tiba ya wakati wa sasa.

Wanafalsafa na wanateolojia wenyu hawatajua cha kufanya na ujumbe huu. Watakuwa na masuala na Ujumbe huu. Hautaendana na uelewa wao, ule ambao wamewekeza wakati yao.

Viongozi wa dini watateta dhidi yake kwa sababu inaongea kuhusu ukweli ambao hawajatambua.

Mungu anaongoza bunadamu katika mwelekeo mpya.

Mtume yuko hapa kutoa Ufunuo. Imemuchukua miongo kuupokea. Itachukua miongo kadhaa kutambuliwa duniani.

Lakini tatizo ni wakati. Binadamu hana muda mrefu wa kujiandaa kwa dunia mpya na kwa Mawasiliano na maisha katika ulimwengu – Mawasiliano ambayo tayari yanatokea, Mawasiliano ya kusudi na nia hatari.

Watu wako obsessed na mahitaji yao, masuala yao, tamaa yao na matakwa yao. Hawaoni harakati ya dunia.

Kwa kua dunia imebadilika, lakini watu hawajabadilika nayo. Na sasa munakabiliwa na seti mpya ya ukweli.

Ni nini Mungu atasema kuhusu haya watu wakihisi kuzidiwa, kama unabii wao wa mustakabali hautatokea, kama kurudi kwa mwokozi wao hakutafanyika, kama wanaamini kuwa Mungu anajenga matatizo haya yote kwao?

Ufunuo unasemea haya yote, lakini lazima muwe wazi kwa Ufunuo, na lazima mukabiliane na matarajio ya mabadiliko makubwa, kwa kuwa mabadiliko haya tayari yamo kwenyu na kwa dunia, na yatazidi kuendelea.

Hamuwezi kurudi nyuma maelfu ya miaka na kujaribu kutafakari yanayotokea leo, kwa kua mageuzi ya binadamu yamehama katika sehemu mpya, sehemu ya kuhodhi duniani na sehemu ya mazingira magumu ulimwenguni.

Mafundisho ya kutayarisha binadamu kukabiliana na dunia mpya na Jumuiya Kubwa yataanza wapi – matukio mawili ambayo yatabadilisha mwelekeo wa historia ya binadamu na kuathiri kila mtu?

Serikali haijui. Viongozi wa dini hawajui. Wataalam hawajui. Vyuo vikuu haviwezi kuandaa watu.

Ufunuo lazima utoke kutoka kwa Muumba wa maisha yote, na tukio hili ndilo linatokea sasa, kwa kuwa munaishi katika wakati wa Ufunuo na Mtume yuko duniani.

Kama bado yuko duniani muna fursa ya kujitayarisha.

Akitoka duniani, hali itakuwa tofauti. Itakuwa ngumu.

Kwa haya, yeye ni mwangaza duniani.

Yeye ni mtu mnyenyekevu na hana madai yoyote ila kuwa Mtume, kwa kuwa hii ndio ile kazi aliyopewa.

Lazima atayarishe ubinadamu kukabiliana na dunia mpya kupitia njia ya Ufunuo.

Lazima atayarishe ubinadamu kukabiliana na Jumuiya Kubwa kupitia njia ya Ufunuo.

Lazima azungumze kuhusu mabadiliko makubwa yanayokabili binadamu na tayari yanakabili watu kila mahali kupitia njia ya Ufunuo.

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya.

Je, ubinadamu unaweza kusonga?

Je, ubinadamu unaweza kujibu?

Je, unaweza kujibu?

Unaweza kukubali kuwa unaishi katika wakati wa ufunuo na kufikiri maana ya hii kwa maisha yako na changamoto ambayo inaleta kwa maisha yako?

Watu hawatambui kiasi ambacho hali ya maisha na mazingira yao inategemea hali ya dunia na harakati ya dunia.

Ni katika mataifa maskini ambapo haya yote yamo wazi.

Katika mataifa tajiri, utajiri unawalinda kutokana na ukweli wa maisha kwa kiasi fulani na kwa muda fulani. Lakini utajiri huu utaisha, na ukweli mkubwa tayari umo nanyi.

Uamuzi utatokana na jinsi ubinadamu utajibu.

Uamuzi utatokana na kile ambacho kitatoa taarifa kwa watu binafsi.

Ni sauti gani ambayo wataisikiliza, kama itakuwa sauti ya nguvu na uwepo wa Knowledge ile Mungu amewapa iwaongoze na iwalinde, ama kama itakuwa sauti ya utamaduni wao ama sauti ya hofu au sauti ya hasira au tamaa.

Uchaguzi ni msingi kwa mtu binafsi, na kwa kile watu watachagua kitaamua hatima na mustakabali wa binadamu.

Kwa hivyo uwajibika ni wa kila mtu na sio tu viongozi na taasisi.

Hii ndio sababu Mungu anatoa Ujumbe Mpya kwa watu na sio kwa viongozi wa mataifa.

Kwa kuwa viongozi hawana uhuru. Wamefungwa na ofisi zao na wale ambao wamewachagua, na matarajio ya wengine.

Hii ndio maana ufunuo unakuja kwako wewe na kwa watu. Ni uchaguzi wao na uwezo wao ambao utatoa uamuzi.

Watu wanataka vitu vingi. Hawataki kuyapoteza yale wanayomiliki. Wanaishi kwa wakati wa muda mfupi. Hawana mtazamo wa kuona mahali maisha yao inaenda.

Ufunuo utakuwa wa mshtuko mkubwa na changamoto kubwa kwa kila mtu, lakini mshtuko huu na changamoto ni mshtuko wa Ufunuo. Na changamoto hii inakabiliwa ni mapenzi ya Muumba. Na changamoto ni kuona kama unaweza kujibu na asili ya majibu yako.

Huwezi kusimama mahali upo, kwa kuwa dunia inabadilika, na itazidi kubadilika. Inasonga na lazima usonge nayo.

Hii ndio kutungamana na maisha.

Hii ndio kutoka kwa utenganisho.

Hii ndio kujikomboa kutoka kwa distractions na obsession.

Hii ndio kujifunza kusikiza, kuona, kutuliza akili yako ndio uweze kuona.

Hii ndio kuyawacha malalamiko yako ili upate kuelewa pale ulipo.

Nii ndio kuchukua Hatua kwa Knowledge ndiyo uwepo na nguvu ya Mungu izungumze kukupitia na ikuzungumzie.

Huu ndio Ufunuo unaoongoza ubinadamu katika mwelekeo mpya.

Je, watu wako tayari kwenda, ama watakaa nyuma – wakikabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, kama wamelala katika pwani wakati Mawimbi Makubwa yanapata nguvu, wanaishi katika ufukwe na kufikiri kwamba yote yamo salama, na wakiishi kwa muda, wakiwa hawawezi kukabiliana na ishara za dunia, wakiishi kulingana na mawazo ambayo hayafuatani na hali halisi ya maisha?

Ni nani anayeweza kujibu?

Ni nani ataagalia?

Ni nani atasikiliza?

Ni nani atakayeweka kando dhana zake na imani yake na mapendeleo yake ndio aweze kukiona kitu, kukisikia kitu, kukijua kitu?

Hii ndio Mtume atakuuliza uifanye.

Hii ndio Unfunuo unahitaji kutoka kwako.

Hii ndio maisha katika dunia mpya itahitaji.

Hii ndio uibuka katika Jumuiya Kubwa ya waangavu inahitaji.

Je, binadamu atakuwa mjinga na dole, chachili na asiyewajibika, akili yake kubwa ikose kutambuliwa na kutumiwa?

Haya ndio maswali.

Majibu yeke hayako wazi, kwa kuwa bado hayajaibuka. Bado hayajakabiliana na jaribio la kweli ambalo limo katika familia ya binadamu.

Lakini Muumba wa maisha yote anaipenda dunia na anapenda ubinadamu na ameituma nguvu ya ukombozi duniani – kukomboa mtu binafsi na kurejesha nguvu yake na uadilifu, ili aweze kukabiliana na changamoto ya maisha inayoibuka katika upeo wa macho.

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya.

Huu ndio wakati wa kujitayarisha, kupokea na kusaidia ufunuo.

Watu watateta, Watalalamika. Watapinga. Watamulaani Mtume. Watakemea Ufunuo. Hawawezi kujibi, hawatataka kuwaza maisha yao na dhana zao upya. Watapinga Ufunuo.

Haya yote hufanyika wakati wa Ufunuo.

Wale walio na uwekezaji mkubwa katika siku za nyuma watapinga dunia mpya na kila kitu ndani yake.

Hawaoni. Hawataweza kujua. Hawana ujasiri wa kifikiria msimamo wao upya. Hawana unyenyekevu wa kusimama wakikabiliwa na Ufunuo.

Ni nini Mungu anaweza kuwafanyia?

Wanauliza vitu vingi kutoka kwa Muumba, lakini hawawezi kujibu jibu la Muumba.

Ni nini Mungu anaweza kuwafanyia?

Kuwa miongoni mwa kwanza kujibu ili zawadi zako kubwa katika maisha ziweze kuwa imara na kuwa na nafasi kujitokeza katika siku na miaka ya maisha yako.

Hii ndio nguvu ya Ufunuo – kutoa hekima na Knowledge ambayo binadamu mno anahitaji sasa kwa kujitayrisha kwa mustakabali ambao utakuwa tofauti na siku zilizopita.

Baraka ziko nanyi. Nguvu ya ukombozi iko ndani yenyu, kwa Knowledge ndani yenyu.

Lakini ni jambo gani ambali linaloweza kuignite Knowledge hii na kuiita na kukuwezesha uikaribie, uielewe na uifuate kwa mafanikio?

Ni lazima iwe ignited na Mungu, na ufunuo uko hapa ili kuweka katika mwendo ukombozi mkubwa wa watu binafsi katika maandalizi ya dunia mpya na kwa hatima ya binadamu ulimwenguni, ambayo bado haijatambuliwa na haijatimizwa.

Sasa ndio wakati wa kujibu.

Ni wakati wa kuwa mwaminifu kwako mwenyewe, bila kulingana maisha yako na mapendekezo yako, lakini kwa utambuzi wa kweli ndani yako.

Kukabiliana na Ufunuo kutaleta changamoto ya kujibu kwa uaminifu huu mkubwa.

Kukabiliana na Ufunuo kutaleta changamoto ya uaminifu huu mkubwa.

Ni changamoto kubwa ya maisha yako.

Ni changamoto muhimu zaidi ya maisha yako.

Ni tukio muhimu ya maisha yako.

Mungu anaongoza ubinadamu katika mwelekeo mpya.