Ufunuo mpya kutoka kwa Mungu unafungua milango ya ulimwengu wa waangavu, ukitoa mtazamo, ufahamu na uelewa ambao hujawahi kutolewa hapo awali.
Familia ya binadamu haitambui kuwa iko dhaifu katika Jumuiya hii Kubwa ama katika uhusiano wake na Jumuiya hii Kubwa.
Imeishi katika upweke kwa muda mrefu, mtazamo wake mwenyewe, mtazamo wa Uumbaji na Uungu, unahusisha dunia hii moja peke yake. Lakini kuna watu wengi katika dunia leo ambao walio na mizizi katika Jumuiya Kubwa, kwa kuwa ufarisi wao wa zamani ulitokea hapo kabla waje dunia hii katika maisha haya.
Nyinyi ni kama kabila iliyotengwa ambayo haijawahi kugunduliwa na dunia ya nje, ambayo haijui kuwa kuna nguvu kubwa ambazo zinaishi karibu nayo na ambayo haijatayarishwa kukabiliana na ile siku ambayo uwepo wake utagunduliwa na walio nje.
Binadamu ameshinda akitangaza huko angani, bila shaka kama mjinga, na kwa hivyo uwepo wake umejulikana na majirani wake na vikundi vingine ambavyo vinachungilia dunia kwa makini.
Kwa wengine, mumekuwa mukichunguzwa kwa muda mrefu sana. Na hata kama wameona kuwa asili yenyu ya ndani haieleweki, tabia zenyu za nje zinaweza kutambuliwa na kutabiriwa kwa urahisi.
Munasimama katika kizingiti cha mazingira tofauti kabisa, ulimwengu ambapo viumbe havifanani na binadamu – ulimwengu ambapo maadili ya binadamu, matarajio ya binadamu hayathaminiwi na wengine, ulimwengu ambapo uwepo wenyu una muhimu au thamani ndogo, ila tu kwa mataifa ambayo yanataka kusaidia uhuru wa binadamu katika dunia ama kwa mataifa ambayo yanataka kuwanyanganya uhuru wenyu.
Jumuiya Kubwa itageuza jinisi mnajiona, na jinsi mataifa yanajadiliana hapa na ingine na vipaumbele vya binadamu. Athari yake inaweza kuwa ya faida kubwa mkiielewa vizuri.
Kwa kuwa ni Jumuiya Kubwa ambayo itashawishi mataifa yenyu yashiriki, yaungane kwa uhifadhi wa dunia na kwa ulinzi wa familia ya binadamu.
Ni Jumuiya Kubwa ambayo itawaonyesha kuwa hamuwezi kuendelea na migogoro yenyu ambayo haiihsi hapa duniani, na kuwa rasilimali yenyu ni ya thamani kubwa, na uwezo wenyu wa kujilisha hapa ni wa umuhimu mkubwa mno.
Na ufahamu huu, hamutaendelea kunyonya dunia kwa kiasi kile ambacho munafanya sasa. Hamutafikiri kama wajinga kuwa mtaweza kuchukua kile kilicho ulimwenguni mkimaliza mali ya dunia hii. Mtaelewa kuwa dunia hii tu ndio kile mlicho nacho. Dunia hii, mfumo huu wa Jua na Sayari zake, ndio kile mlicho nacho.
Nje ya hii, mnaingia mazingira ambayo yanamilikiwa na yanathibitiwa na wengine, na hamuwezi kuwanyanganya walio nacho. Hamujui sheria za ushiriki katikia ulimwengu ama mahusiano kati ya mataifa ama kile ambacho kinakubaliwa na kile ambacho hakikubaliwi katika Jumuiya hii Kubwa ya waangavu.
Nyinyi ni kama mtoto anayeingia katika mji mkubwa – bila makosa, bila kujua, bila ufahamu.
Watu wanataka mengi kutoka kwa wageni hapa. Wanatarajia mengi. Watu wanajiona kuwa hao ni muhimu katika ulimwengu na kuwa wengine bila shaka watakuja hapa kuwasaidia na kuwapa kile wanataka na kile wanahitaji. Watu wanafikiri kuwa Mawasiliano ni aina ya tukio la kusisimua, likizo kutoka mambo ya kawaida ya maisha ya binadamu. Wanataka kufikiri kuwa Mawasiliano haya yatakuwa mazuri sana na ya manufaa kwa sababu hawana nguvu, ujasiri au maandalizi ya kufikiria kwa njia yoyote ingine.
Ufunuo Mpya wa Mungu unawatolea dirisha ya kuangalia Jumuiya Kubwa, dirisha ambayo Mungu peke yake anaweza kutoa. Kwa kuwa hakuna lolote ulimwenguni ambalo Mungu halifahamu. Hakuna taifa ambayo inaweza kudai hivyo. Hatika taifa ambayo ina uelewa wa galaxy hii. Hakuna taifa ambayo ina uelewa wa asili ya ndani ya ubinadamu.
Hata yale mataifa katika sehemu hii ya anga ambayo yana uhuru na yanajitawala, hata hao hawawezi kuelewa maana kamili ya asili ya ndani ya binadamu.
Kila mtu ulimwenguni anatafuta rasilimali, na yale mataifa yameendelea kiteknolojia yanategemea rasilimali kabisa. Kamwe hamutawahi kufika mahali ambapo hitaji hili litaisha kwa sababu mukizidi kuendelea kiteknolojia, basi hitaji la rasilimali linazidi.
Binadamu haijui kuwa iko katika kizingiti kikubwa, pointi kubwa ya mageuko, pointi ambayo itatengeza mustakabali ambao ulio tofauti na siku za zamani. Ikiishi katika dunia ya upungufu. dunia ya rasilimali zinazopunguka na fursa ambazo zinapunguka. Serikali zenyu zimetumbukia katika shida zao za ndani na shida na serikali za taifa ziingine.
Dunia ni mahali pazuri sana, pakiwa na utajiri wa kibiolojia, pakiwa na rasilimali mingi ya muhimu ambazo hazipatikani kwa urahisi katika ulimwenngu ya dunia zilizo tasa.
Ufunuo wa Mungu lazima uwaamushe kwa ukweli, ugumu na fursa za kuibuka katika Jumuiya ya waangavu. Hakuna ufunuo yoyote ya zamani kutoka kwa Mungu ambayo ilihitaji kufanya hivi kwa sababi hitaji haikuwa hapo. Ubinadamu haukuwa umeendelea sana.
Lakini sasa muna tamaduni ya kidunia – iliyotenganishwa, iliyo katika migogoro, inayoharibu, isiyo na ufahamu na isiyowajibika, lakini hata hivyo ni jamii ya kidunia. Muna mawasiliano ya kidunia. Muna uchumi ya kidunia. Na kwa watu wengi, ufahamu wa kidunia. Ni katika pointi hii ambapo maingilio yatajaribiwa. Ni katika pointi hii ambapo binadamu itakuwa kama nyara ya kumilikiwa.
Wale ambao watakuja hapa na tayari wako hapa hawawezi kuishi katika mazingira ya kibiolojia kama mnayoishi na mumejifunza kuishi. Wanahitaji usaidizi kutoka kwa binadamu. Wanahitaji utii kutoka kwa binadamu. Wanahitaji ushiriki kutoka kwa binadamu ndio waweze kupata uwezo wa kutawala na kudhibiti hapa. Na watachukua faida kutoka kwa matarajio yenyu, tamaa yenyu, fantasies zenyu, na malalamiko yenyu ndio waweze kujiimarisha hapa.
Angalieni historia yenyu ya maingilio duniani. Angalieni vile watu wa kitamaduni walivyoshindwa katika uwepo wa maingilio ya kigeni. Hii sio lazima iwe hatima yenyu.
Mukianza kufikiri katika mazingira haya makubwa ya maisha. mutaanza kuona mambo ambayo hapo awali hamukuweza kuyaona. na mutaona kuwa umoja wa binadamu na ushiriki wa binadamu sio tu lengo ambalo linahitajika katika mustakabali au chaguo nzuri, ila ni muhimu kwa kuhakikisha uhuru na mustakabali wa familia ya binadamu.
Maingilio hayataki kuwaangamiza, lakini yanataka kuwatumia, kwa malengi yao wenyewe. Huu ni ukweli ambao hamuwezi kuepuka, na uongo ambao utatolewa kwa familia ya binadamu na pacification ambayo itatolewa kwa familia ya binadamu kusujudia na kutii ni mkubwa mno.
Watu wakipozeza imani kwa utawala na taasisi za binadamu, wataangalia nguvu ziingine kutoka ulimwenguni ziwaongoze, wakiamini kwa dhati kuwa nguvu ambazo zitakuwa za faida zitakuja hapa kurejesha na kuokoa binadamu. Ni tarajio hii, hamu hii, ingawa haitambuliwi, ambayo itatumiwa na Maingilio kwa malengo yao wenyewe.
Uhuru wenyu ni wa thamani kubwa, kwa kiasi chochote ambacho imeimarishwa duniani. Imepatikaka kutokana kwa njia ya juhudi kubwa na kwa kutolewa dhabihu kutoka kwa binadamu. Lazima ilinzwe kwa makini makubwa mno.
Mnashughilika na wengine katika mtazamo huu, lakini sasa mumepata shughuli kubwa, na shughuli hizo zimeleta hitaji kubwa ya kuwa na elimu kuhusu maisha katika ulimwengu na maandalizi ya ushiriki huu ulio mgumu na wa hatari kubwa mno.
Wale ambao ni washirika wa binadamu, mataifa yalio huru, hayataingilia shughuli za binadamu, kwa kuwa maingilio kwao ni ukiukaji. Wanatambuwa kuwa hata wakipata uaminifu wenyu, lazima waimarishe uwepo wa uthibiti hapa ndio waweze kuwaongoza katika Jumuiya Kubwa. Na hii, hawawezi kuifanya. Wanatambua kuwa binadamu lazima ipambane na iteseke, kufika katika pointi ya utambuzi na uwajibika kuhusu mustakabali wake na hatima yake hapa.
Wanaweza tu kutoa ushauri. Watatuma Maagizo, Maagizo kutoka Washirika wa Binadamu. Haya wameyafanya kama sehemu ya Ufunuo Mpya kutoka kwa Mungu, kwa kuwa Muumba anajua lazima mtambue kuwa hamuko peke yenyu katika ulimwemgu na uhuru na uwezo wa kujitawala upo na umepatikana na wengine. Lakini mafanikio haya hayakuwa rahisi kupata. Yana mahitaji ya msingi.
Watu hushtushwa na haya, sio kwa sabau ni ya uongo ama yanaonekana kuwa ni ya kusisimua, lakini kwa sababu hawajawahi kuyawaza, na hata hawataki kuyawaza, ni makubwa, ya ugumu na ya changamoto.
Lakini hii ni dunia yenyu. Hii ndio sababu umekuja. haukukuja kulala katika dunia iliyo nzuri, lakini kusaidi kuihifadhi na kulinda familia ya binadamu kutoka kwa upungufu na utawala wa kugeni.
Migogoro ya binadamu inawapoteza. Ujinga, upumbavu na ukosefu wa ufahamu kuhusu yale ambayo yanaishi katika mipaka yenyu, migogoro ya binadamu inawapoteza.
Huu ndio wakati wa ubunadamu upevuke, ukue wakubwa, utambue kuwa unaishi katika Jumuiya Kubwa ya waangavu – Jumuiya Kubwa ambayo hamuwezi kudhibiti, Jumuiya Kubwa ambayo iko zaidi ya juhudu yenyu, teknolojia yenyu na hata uelewa wenyu.
Hii ndio maana Muumba wa maisha yote analeta ufunuo kuhusu Jumuiya Kubwa katika dunia. Huu ndio wakati – kama binadamu anasimama katika ukingo wa dunia ya upungufu, dunia ya rasilimali zinazopunguka na dunia ya ukosefu wa utulivu wa kuichumi na siasa, wakati ambapo dini za dunia zinashiriki katika mgogoro na ushidnani unaoendelea kuhusu kukubalika na uongozi wa binadamu, wakati ambapo mataifa maskini hayana rasilimali za kutosha na mataifa tajiri yanaanguka katika madeni makubwa.
Huu ni wakati kamilifu wa maingilio. Ni wakati muhimu wa ufahamu mkubwa wa binadamu uibuke na kwa uwajibika mkubwa duniani – sio tu kwa taifa yake moja ama kikundi chake kimoja ama kwa dini yake, lakini kwa binadamu wote. Kwa kuwa taifa zikishindwa, basi dunia nzima itashindwa. Kama Maingilio yatafaulu katika sehemu moja ya dunia, hii itatia katika hatari mustakabali wa kila mtu hapa.
Watu wana manunguniko, wana mahitaji, wana, katika kesi fulani, mahitaji makubwa mno – umaskini na ukandamizaji. Viongozi wa dunia ni aidha vipofu ama hawawezi kushiriki yale waliomabiwa, wanaoona na wanajua. Kwa hivyo watu wa mataifa wanabaki wajinga kuhusu matukio haya makubwa ya historia ya binadamu, changamoto kubwa kwa uhuru wa binadamu na uwezo wake wa kujitawala na fursa kubwa ya umoja na ushirika wa binadamu.
Kwa kuwa hamutaweza kushiriki katika Jumuiya Kubwa ya waangavu kama muna vita na migogoro kati ya makabila na mataifa yenyu. Hamutakuwa na nguvu au ufanisi hapo, na udhaifu wenyu utakuwa wazi kwa wengine.
Ubinadamu unaharibu mali ya dunia, na hii pia imeleta maingilio.
Kuna mengi ya kujifunza. Haiwezi kuwasilishwa na maneno machache tu, lakini kwa mfumo mkubwa wa mafundisho, ambao ni sehemu ya Ufunuo wa Mungu.
Hapa mkristo lazima awe mkristo na ufahamu wa Jumuiya Kubwa. Muislamu lazima awe muislamu na ufahamu wa Jumuiya Kubwa. Buddhist ama Myahudi anapata panorama kubwa ya maisha ambapo mafundisho yake ya kidini lazima yawe ya muhimu. Kama dini duniani itakuwa ya kufunza na kuerevusha, lazima iwe na uwezo na ufahamu huu.
Hamuwezi kuwa wajinga mukikabiliana na Jumuiya Kubwa ama mukikabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko ambayo yanatokea duniani. Ni wakati wa kupevuka.
Binadamu ana nguvu yake. Hamujapoteza uhusiano na Knowledge ya ndani ambayo inaishi ndani ya kila mtu. Hamujakuwa jamii ya kijeshi, ya kidunia, ya kiteknolojia, ambayo ni kama kawaida ulimwenguni. Hamujapoteza uhuru wenyu ama hisia zenyu kubwa ingawa haya yote yanatokea kila siku.
Mahitaji ya maisha ni muhimu kila mahali. Teknolojia ya juu haitafanya muepuke mahitaji haya kikamilifu na kwa kweli inaweza kuyasambaza kwa kiasi kikubwa. Kweli munafikiri kuwa jamii kubwa ya kiteknolojia kutoka Jumuiya Kubwa haihitiaji rasilimali, rasilimali ambayo sasa haiwezi kutengeneza na ni lazima wafanye biashara na wayatafute, kutoka mmbali na dunia yao? Wamepoteza uwezo wao wa kujitawala. Wanadhibitiwa sasa na mitando ya biashara ambayo sasa wanaitegemea.
Kuwa na uhuru ulimwenguni lazima muwe na uwezo wa kujitawala, lazima muwe na umoja na lazima muwe na siri. Haya ndio mahitaji ambayo kila taifa inahitaji, kila taifa lazima iimarishe katika Jumuiya Kubwa ya waangavu.
Hapa munaona hatari na mvuto wa binadamu akipokea teknolojia na rasilimali kutoka nje ya dunia. Huu utakuwa mvuto mkubwa mno!
Mukipoteza uwezo wenyu wa kujilisha, kila kitu ambacho munathamini kitapotea, kwa sababu hamutaweza kuimarisha masharti ya kushiriki ili muweze kupata vitu vyote ambavyo sasa mnavyovitegemea. Mataifa ingine yataamua tabia yenyu na ushiriki wenyu. Hii ni ukweli wa maisha.
Hamuwezi kujaribu kutawala ulimwengu wenyu wa karibu mtapingwa na kila mtu. Hii ni picha tofauti kuliko ile picha ya filamu zenyu na science fiction zenyu na fantasies zenyu, matumaini yenyu, matarajio yenyu yasiotajwa. Hii inatoa picha tofauti na umuhimu wa umoja na ushiriki wa binadamu hapa duniani, umuhimi wa kulinda na kujenga uhuru wa binadamu na nguvu na uwepo wa Knowledge ambayo Mungu ameweka ndani ya kila mtu.
Hapa uhuru sio tu kujitumbukiza kwa mambo na kukosa kuwajibika kwa mtu yeyote au kitu chochote. Inakuwa kitu cha muhimu katika ushiriki wa maisha yako. Hapa vipawa vyako vikubwa vinaweza kutoka mbele, kwa kuwa unatambuwa uko hapa kutoa huduma katika hitaji na hatari kubwa ya binadamu. Hapa kila kitu ndani yako kilicho cha kweli na asili kinaanzishwa na kinaitwa. Hapa mataifa yanawacha mogogoro yao yasioisha na yanajaribu kujenga uimara kwao wenyewe na kwa majirani wao ndio wahakikishe usalama wao wakati wa mustakabali na kujilinda kutoka maingilio kutoka nje.
Dunia haitachukuliwa kwa nguvu, kwa sababu hii hauruhusiwi katika sehemu hii ya ulimwengu. Itachukuliwa kupitia mvuto na ushawishi, kupitia kupata faida kutoka kwa udhaifu na migogoro ya binadamu, ushirikina wa binadamu na mahitaji ya binadamu ambayo hayajatimizwa.
Kushambuliwa kwa kutumia nguvu hakutumiwi katika sehemu hii ya ulimwengu. Njia ya hila ndogo lakini ilio na matokeo makubwa inatumiwa ndio rasilimali za dunia zihifadhiwe na uwezo wa kutawala upatikane kwa kutumia ushawishi, oungo na siri. Ubinadamu ni taifa ambayo iliyo clumsy na iliyo na vurugu katika mtazamo huu, lakini hata hii inabadilika hapa Duniani.
Tunawapa mtazamo huu kwa sababu hii inawakilisha upendo wa Muumba. Ingawa itakuwa ni kubwa na ya kutisha mara ya kwanza, ni ukweli ambao lazima muwe na ufahamu wake na muuzoee. Sasa ni lazima mufikiri sio tu kwa kujitazama wenyewe ama jamii yenyu ama taifa yenyu, lakini kwa dunia nzima kwa sababu hii itaamua hatima yenyu na usalama wa watoto wenyu na watoto wa dunia.
Huu ni mgeuko mubwa wa ufahamu, mgeuko ambao ni mkubwa na wa muhimu. Watu watapinga haya, bila shaka. Watakimbilia dini yao. Watakimbilia ideolojia yao ya siasa. Watakimbilia fikira za binadamu. Lakini maisha katika ulimwengi haitegemei haya. Sio swala la mtazamo. Sio swala la ideolojia. Ni swala la kuwa makini, kujiangalia, kujiona bila hukumu na kuwa mwaminifu kwako mwenyewe.
Hii ni changamoto kubwa, lakini ni changamoto inayohitajika, changamoto inayokomboa kama inaweza kukabiliwa kwa uaminifu na kwa dhati. Muna macho ya kuona na masikio ya kusikia, lakini hamuangalii na hamusikilizi. Kila mtu karibu na wewe anaonekana kuwa yuko obsessed, na shughuli ama anakandamizwa. Ni nani atazungumza na hao? Labda hawatasikia maneno yetu. Ni nani atazungumza na hao?
Unahitaji tu kupointi kwa Ufunuo, kwa sababu Ufunuo ni mkubwa mno kiasi mtu moja peke yake hawezi kuielewa. Pointi kwa Ufunuo, kwa kuwa hii peke yake inashikilia maandalizi kwa mustakabali na hatima ya binadamu kaitka dunia inayoibuka.
Mungu anapatia binadamu kile ambacho binadamu hawezi kujipatia mwenyewe. Mungu anaagiza binadamu ndio awe macho kwa hatari na fursa akisimama katika kizingiti cha anga. Mungu anaagiza binadamu awe macho kwa hatari na fursa na umuhimu wa kuishi katika dunia ya upungufu. Mungu analeta duniani ufafanuzi wa asili na dhamira ya kiroho cha binadamu, asili na dhamira ambayo imepotea na imevikwa katika Ufunuo kutoka kwa Mungu za hapo awali.
Ufunuo ni mkubwa mno. Unazungumzia mambo mengi. Hamuwezi kufanya iishe, na lazima muitumie na mushiriki ukweli wake na wengine. Ni hapo tu ambapo mutaona maana yake halisi na kwa nini ni muhimu na kwa nini inashikilia ahadi kubwa ya mustakabali na uhuru wa watu wa dunia.
Kwa kuwa hakuna uhakika wa mafanikio. Watu wengi katika ulimwengu wameanguka kwa ushawishi na utawala. Imefanyika mara isiyohesabika. Ni tukio lisilozuika kwa watu ambao hawajaonywa na kutayarishwa kushiriki na mazingira makubwa ya waangavu.
Tahadharini fantasies na matarajio yenyu. Yajadili. Yafikirie katika mwangaza wa ukweli wa asili na historia ya binadamu.
Ukiwa mwaminifu kwako mwenyewe, lazima ukuje kuona kuwa hujui kile kilichi zaidi ya mipaka ya dunia hii, na matarajio ya matumaini yanaweza kukuvika. Lazima utayarishwe kwa kitu chochote, kama vile lazima utayarishwa kwa kitu chochote kinachofanya kazi hapa duniani – katika mahusiano ya binadamu na katika shughuli za maisha yenyewe.
Kuwa na uhuru lazima uwe na nguvu. Kuwa na nguvu lazima uwe wazi. Lazima uone wazi. Lazima usikie ukweli. Lazima uwe na mtazamo usio na hukumu kuhusu maisha yako na hali yako. Lazima uangalie dunia sio kwa kunungunika au kuepuka, lakini kwa huruma, uvumilivu na uamuzi. Kama lazima mujenge msingi wa mustakabali mpya hapa, kuchangia sehemu yako ndogo lakini muhimu hapa, lazima muwe na mtazamo huu.
Pokea zawadi hii ya upendo na Ufunuo. Inakuja na uwajibika mkubwa, lakini pia na nguvu kubwa na ahadi kubwa.
Bado hauishi ile maisha unafaa kuishi kwa sababu maisha yako haiko kaitka ushiriki na Ukweli Mkubwa ambao unaishi ndani yako na karibu na wewe. Kwa binadamu, hii ni pointi kubwa ya mageuko. Na kwako wewe, hii ni pointi kubwa ya mageuko.
Watu wa dunia lazima waamuke kwa Jumuiya Kubwa na kwa hali ya dunia ambayo wanaishi. Lazima mujifunze kuhusu nguvu yenyu kubwa na hekima yenyu kubwa ambayo Mungu ameweka ndani yenyu iwaongoze, iwatayarishe na iwalinde.
Mungu amezungumza tena. Ni kwa dhamira kubwa ya kukabiliana na seti kubwa ya mahitaji.