Tag Archives: How does God communicate to you?

Je, Mungu huwasiliana aje na wewe?

“Kupitia Knowledge unaweza kuhisi uwepo wa mahusiano yote. Hii ni ufarisi wa Mungu.”

 Mungu ni Chanzo cha Knowledge ndani yako, Knowledge ni roho ya ndani ya akili, ile Muumba ameweka ndani yako iwe nawe na iwe na viumbe vyote ambavyo vinamiliki hisia na fahamu isiyo na muundo, katika Ulimwengu.

Mungu aliumba ulimwengu wa kimwili, lakini sio vile wewe unafikiri. Mungu aliendesha mchakato wa mageuzi katika ulimwengu wa kimwili uchukue nafasi na muda kwa wale ambao wanaishi katika nafasi na muda, kwa wale ambao walitenganishwa na Muumba kwa mapenzi yao na nia yao.

Kuelewa taarifa hii, kwamba Mungu ndiye Muumba wa Knowledge ndani yako, lazima uelewe tofauti kati ya akili yako ya kiroho na akili yako ya dunia. Lazima uelewe tofauti kati ya Roho yako, akili yako na mwili wako. Knowledge ndani yako inawakilisha uhusiano wako na Mungu na maisha yako nje ya dunia hii. Uhusiano huu uwepo kati ya na zaidi ya dini zote za ukweli. Knowledge ni safi na ni ya kudumu na haiko kiasi ya nguvu au ushawishi wa chochote duniani.

Ujumbe Mpya utakufundisha jinsi ya kuyaelewa mambo haya kwa njia wazi iwezekanavyo. Lakini kwa sababu hiki ni kizingiti kipya na uelewa upya kwa binadamu, itachukua muda na kutia moyo kutoka kwa wengine ambao wanajifunza na wewe. Ni vigumu na changamoto kujifunza kitu kwa mara ya kwanza wakati kila mmoja aliye karibu na wewe anazingatia maadili na mawazo tofauti na wewe. Kama unaweza kuona kuwa Knowledge ndani yako ni ile sehemu itakayo dumu, ile sehemu iliyoumbwa na Mungu na bado inayoshikamana na Mungu, sehemu ambayo Mungu amerishai na hekima yake kuongoza na kulinda maisha yako katika dunia hii na kwa wakati huu, basi unaweza kuanza kuona hali halisi ya uandishi huu wa Mungu na umuhimu kwako wewe unayetaka kupata kusudi ya ukweli, maana na mwelekeo katika maisha yako.