“Hapa lengo lako halitakuwa Mungu wa dunia yako na muda wako, bali ni Mungu wa dunia zote na wakati wote.”
Katika Ujumbe Mpya, Mungu hufikiriwa ndani ya muktadha mpana wa ulimwengu mzima, badala ya ndani ya hii dunia moja. Ni hatima ya binadamu kuibuka ndani ya Jumuiya hii Kubwa ya maisha ya waangavu.Katika Kiroho cha Jumuiya Kubwa, kitabu cha theolojia ya Ujumbe Mpya, hivi ndivyo Mungu ameelezwa,
“Katika Jumuiya Kubwa Mungu ni kamili. Katika dunia yenyu, Mungu ni Mungu wa dunia yenyu, Mungu wa jamii yenyu, Mungu wa historia yenyu, Mungu wa asili yenyu, Mungu wa hofu na matarajio yenyu, Mungu wa mashujaa wenyu, Mungu wa janga yenyu, Mungu aliye na mahusiano na kabila yenyu na wakati wenyu. Lakini katika Jumuiya kubwa, Mungu ni mkubwa sana, kamili zaidi ya ufafanuzi wa taifa yeyote, zaidi ya historia ya taifa yeyote zaidi ya asili, hofu na matarajio ya taifa yeyote, zaidi ya uelewa wa filosofia. Na hata hivyo, unapata Mungu katika sirika safi, katika wakati usio na muda wa utambuzi, katika hamu ya kutenda zaidi ya nyanja ya maslahi na nia yako binafsi,katika utambuzi wa wengine, katika maarubu ya kutoa, katika ufarisi usioweza kuelezwa wa mvuto. Hizi zinaweza kutafsiriwa. Hii ni Mungu katika vitendo.Kwenyu, hii ni Mungu.
Muwaze Mungu katika mtazamo kwa Jumuiya Kuu– sio kama Mungu wa binadamu. Sio kama Mungu wa historia yenyu, sio kama Mungu wa mateso na majaribu, lakini kama Mungu wa wakati wote, wa mataifa yote ulimwenguni,wa vipimo vyote, kwa wale walio katika mwanzo wa mfululizo wa mabadiliko ya utamaduni, na kwa wale walio mwisho wa mfululizo wa mabadiliko ya utamaduni, kwa wake wanaofikiri kama wewe na kwa wale ambao wanafikiro tofauti, kwa wale ambao wanaamini na kwa wale abao imani ni kile ambacho hakiwezi kuelezwa. Hii ndiyo Mungu katika Jumuiya Kubwa na hapa ndipo lazima uanze.”