Tag Archives: What Is the New Message from God?

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni nini?

 

“Ujumbe Mpya umetumwa na Mwumba wa maisha yote. Ni ujumbe wa kumutyarisha binadamu binafsi na kuwatayarisha watu wa dunia ili waishi na waweze kupenya hatari kubwa itayokabili binadamu. Ni zawadi kubwa katika uso wa haja ya haraka. “

Kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani. Ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwumba wa maisha yote ya kulinza na kuendelesha binadamu. Ina onyo, baraka na maandalizi kwa watu wote wa dunia.

Ujumbe Mpya hauna msingi na dini za utamaduni duniani au mafundisho ya kiroho. Ni zawadi kwa watu wa mataifa yote na imani zote. Ina heshimu ukweli unaodumu katika Ujumbe kuu ambazo Mwumba amewahi kutuma duniani, na sio kama chochote kile ambacho kishawahi kufuniliwa kwa binadamu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni mawasiliano ya halisi kutoka kwa Mwumba ambao umetumwa ulimwenguni wakati wa mabadiliko makubwa, migogoro na mapinduzi. Ujumbe Mpya unatoa maarifa, hekima na mwelekeo ambao ubinadamu wenyewe hauwezi kutoa ili ukabiliane na changamoto kubwa ambayo kwa sasa inakabiliwa na familia nzima ya binadamu.

Ujumbe Mpya ni jibu ya maombi ya dhati kutoka kwa watu mataifa yote na imani za utamaduni kwa uhuru, usalama na ukombozi. Ni ufunuo mpya kuhusu Kiroho Moja, hifadhi ya dunia na mustakabali ya binadamu na hatima ya binadamu ndani ya Jumuiya kubwa ya maisha ya waangavu katika ulimwengu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umo ndani ya mfululizo wa maandiko matakatifu na mafundisho. Ulifunuliwa katika kipindi cha miaka ishirini na tano. Ufunuo bado unaendelea mpaka leo.