Ulivyofunuliwa
Marshall Vian Summers
April 17, 2007
Boulder, Colorado
Hii ni sehemu ya Ujumbe Mpya ya Dunia inayohusu hatma ya mataifa na watu na wito kubwa unaouaita ubinadamu.
Watu na mataifa ya dunia sasa wanaingia wakati wa shida kubwa na mabadiliko. Rasilimali ya ulimwengu inapunguaka. Watu duniani wanaongezeka. Mambo yakiendelea hivyo, kutakuwa na ushindani wa rasilimali zilizobaki utakaoendelea kwa muda usiojulikana na na pia kutakuwa na hatari kubwa ya mapambano na vita. Hapa uadui wa kale utaamushwa. Chuki itatumiwa na wale ambao ni kabambe ndani ya serikali na mashirika ya dini kugombanisha watu. Udhaifu wa ubinadamu utatumiwa kutia hofu ndani roho ya watu.
Ni kwa sababu ya kizingiti hiki kikubwa, Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umetumwa ulimwenguni, kwa sababu una uwezo wa kuulinzi na kuuendeleza ubinadamu. Ili ubinadamu uweze kuelewa ukuu wa ujumbe huu na umuhimu wake kwa wakati huu, lazima uelewe na utambue mabadiliko hayo makubwa ambayo sasa yanatishia familia ya ubinadamu – yanatishia kutuma familia ya ubinadamu katika upungufu, yanatishia kuharibu mafanikio makubwa ya ustaarabu, yanatishia kudhoofisha ustawi na maisha ya watu kila mahali.
Hapa siasa na hata dini yenyewe itakuwa ikitumiwa kama silaha ya vita, kuwatenganisha watu na kuhaifisha vita kubwa, sio vita vya itikadi, lakini vita vya rasilimali ya dunia. Hapa migogoro itawekwa vinyago. Migogoro hii itasitiriwa kama migogoro ya siasa na dini, lakini kwa asili ni ushindani wa rasilimali. Ni vita vya upatikanaji na usambazaji wa rasilimali. Ubinadamu sasa unakabiliwa na hatari kubwa ya kuishi katika dunia ya upungufu–ulimwengu ambao ubinadamu umetweza mazingira yake, ulimwengu ambao ubinadamu umeadhiri hali ya hewa, ulimwengu ambao rasilimali yakuendelesha maisha inaharibiwa na ujinga na uchoyo wa ubinadamu. Hii ndiyo sababu Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umetumwa ulimwenguni.
Kuutambua Ujumbe Mpya na kuelewa chanzo chake na maana yake kwa wakati huu, wakati huu wa Ufunuo, lazima muitambue hatari kubwa ambayo ubinadamu sasa utaiingia na ile tayari unakabiliwa katika maeneo mengi ya maisha. Hamuwezi kuwa na uwezo wa kufahamu umuhimu wa Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu musipokuwa munaweza kuyakabili mambo haya, musipokuwa munaweza kutambua hali hii na kama munaweza kuona kwamba bila Ujumbe Mpya kutoka kwa Chanzo cha maisha yote, uwezekano wa ubinadamu kutafuta njia sahihi ya kukabiliana na hali hii ngumu nyakati hizi ngumu ni ndogo sana. Uwezekano wa ubinadamu kuepuka vita vinavyoendelea, migogoro na uharibifu wa mazingira ni ndogo sana. Ahadi ya ubinadamu ya kuanza mustakabali mkubwa, mustakabali utakaokuwa tofauti na siku zilizopita, itakuwa ndogo sana. Uwezo dhidi ya mafanikio ya ubinadamu sasa ni kubwa sana ndiyo maana lazima Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ufunuliwe. Lazima uuone Ujumbe Mpya katika hali kama hii ama hautaweza kuuelewa wakati huu wa Ufunuo ambao unaoishi. Huwezi kuelewa.
Kwa wale ambao watajaribiwa kuchukua upanga kwa jina la dini au faida ya kisiasa: Lazima wayatambue mawazo yenyu, dhamira yenyu na matendo yenyu ya kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa ubinadamu. Matendo hayo ni kinyume na kile Mungu anakusudia kwa ubinadamu. Mungu anakusudia ubinadamu uwe umoja na ujitegemee ndani ya Ulimwengu ya waangavu. Hata katika wakati huu, kuna mataifa ingine nje ya dunia hii ambayo yanasubiri ubinadamu ushindwe, yanasubiri nafasi ya kuingilia kati ili wapate faida kwa sababu ubunadamu ni dhaifu na unashindana.
Kama hamuwezi kuyaona au hamuwezi kuyakubali haya, basi hamuwezi kuelewa hatari kubwa inayokabili ubinadamu wakati huu. Hamuelewi taabu kubwa inayokabili familia ya ubinadamu. Na hamuwezi kuona hatari kubwa, hatari ya giza Kubwa ambayo iko hapa duniani, giza iliyotokea kwa sababu ya maingilio kutoka nje na giza oliyotokea kwa sababu ya ujinga, uchoyo, ushindani, migogoro na vita vya ubinadamu.
Nyinyi ambao mutakaochukua upanga kwa jina la dini au faida ya kisiasa: Lazima mutambue kwamba munaenda kinyume cha mapenzi ya Mungu kwa ubinadamu. Na ingawa Mwumba hatawaadhibu, ndani yenyu mutachukua hatua mbali na ujuzi, unaoitwa Knowledge, ya Mungu. Nyinyi wenyewe muntajiingiza katika giza na kivinyovinyo. Na nyiyni mutawaongoza watu wenyu na taifa yenyu katika vita, ganjo, na uharibifu. Kwa maana ubinadamu umepita wakati ambapo taifa moja inaweza kupata faida kutokana na upungufu wa taifa ingine, kwa sababu dunia nzima sasa iko hatarini.
Kama mutachukua upanga kwa jina la dini au faida ya kisiasa, mutaenda kinyume cha mpango wa Mungu kwa ubinadamu. Ingawa Mungu hatawaadhibu, mutajitenganisha na mutauonesha kisogo ujuzi wa Mungu, uitwayo Knowledge unaoishi ndani yenyu, Ujuzi huu unaoitwa Knowledge uliwekwa ndani yenyu na Mungu uwalinde na uwakomboe. Na nyinyi wenyewe mutajitia katika matata na migogoro, katika chuki na taabu, na mutauleta uharibifu na ukiwa kwa watu wenyu.
Hii ni hatari kubwa, na hii itakuwa majaribio makubwa kwa ubinadamu; kutumia nguvu, kwa sababu ya malalamiko yao, dhidi ya wengine, kutumia nguvu, kwa sababu ya uhasama wa zamani, dhidi ya wengine, Mataifa kuanza kushindana na kuingia katika mgogoro na mataifa mengine, wakiamini kuwa ni kwa ajili ya ustawi wa nchi yao au ni mapenzi ya Mungu. Lakini huo utakuwa ni uwongo. Hiyo itakuwa makosa. Hicho kitakuwa ni kinyume cha mapenzi ya Mungu na Mpango wake kwa ubinadamu. Ingawa Mungu hatawaadhibu, mutajitenga na Hekima ya Mungu na Mapenzi ya Mungu. Mutaingia katika kivinyovinyo na giza, katika kero na hatimaye katika kukata tamaa.
Sikilizeni kwa makini basi, mataifa ya dunia, viongozi wa dunia na wananchi wa dunia. Sikilizeni kwa makini maneno haya, yametoka kwa Mungu, yanawakilisha Ujuzi, uitwayo Knowledge, ambao umewekwa ndani yenu kuwaongoza na kuwalinda. Ujuzi huu, uitwayo Knowledge, uko hapa kuongoza na kulinda ubinadamu.
Hii ndio sababu Mtume ametumwa ulimwenguni – kuleta Ujumbe huu Mpya wa matumaini, ujumbe huu wa ukombozi na azimio, kwa familia ya ubinadamu kwa wakati huu wa taabu kubwa. Kwa maana munaingia wakati wa taabu kubwa. Muko mwanzo tu wa wakati ambapo vita kubwa na migogoro kubwa yanaweza kujitokeza. Makaa ya vita hivi tayari inang”aa. Dhamira ya vita hivi tayari iko hai katika akili na mioyo ya watu wengi. Na hali ya migogoro hii ya vita tayari iko nanyi.
Hapa ubinadamu una nafasi moja kubwa ya kuungana katika utetezi wake na kwa uhifadhi wake ndani ya dunia hii na katika Jumuiya Kuu ya maisha ulimwenguni, ambapo uhuru haujulikani na thamani ya ubinadamu haitambuliwi, ila kwa wachache tu.
Wale ambao watachukua upanga kwa jina la Mungu au kwa faida ya kisiasa watakuwa wameshindwa kutimiliza kazi yao na wito wao katika maisha, Na watawaongoza wengine kutotimiliza kazi yao. Ndani ya ukosefu huu, hakutakuwa na amani na azimio, kwa maana watu wenyewe watajikanya ujuzi, unaoitwa Knowledge, wa Mungu ulimo ndani yao. Wataikana mpango wa Mwumba kwa ubinadamu. Watakuwa wameigeuka Hekima Kuu ile Mungu aliyeiweka ndani yao na ndani ya mioyo yote. Watakuwa, kwa ujinga na kiburi na ubatili, wameharibu nafasi yao kubwa ya kufanya mchango halisi kwa watu wao, na taifa yao na kwa ulimwengu.
Sikilizeni kwa makini onyo hili. Iinaleta ujumbe wa madhara makubwa na maana makuu. Maana kamili ya onyo hili iko zaidi ya mafikara yenyu, na bado ujumbe mutakao upata utakuwa wazi, na rahisi kwa wale watawoza kuuelewa.
Jihadharini, viongozi wa mataifa na viongozi wa dini. Jihadharini kama munatafuta njia sa kuumiza au kushinda taifa zingine kwa faida ama kutumia nguvu wa sababu ya kero yenyu dhidi ya wengine au uhasama wenyu wa kale. Fahamu kwamba munajitia wenyewe katika giza na katika vivinyovinyo na taabu, na matokeo yatakuwa ganjo, umaskini na uharibifu kwa watu wenyu. Fahamu, raia wastani, kwamba wewe pia una wajibu wa kufuata hekima na Ujuzi, uitwayo Knowledge, ule Mungu aliuweka ndani yako, ndio ugundue hekima hii na ujuzi huu, uitwayo Knowledge, na usiihalifu kwa sababu ya hasira au kisasi, chuki au uchoyo. Wewe pia una wajibu, kwa ajili ya matokeo sio jukumu ya viongozi wa mataifa na dini pekee. Hatimaye ni jukumu ya kila mtu.
Sikilizeni kwa makini, basi, onyo hii kubwa. Onyo hili imetoka kwa upendo wa Mungu, lakini ni onyo hata hivyo. Inawaonya dhidi ya uwezekano mkubwa wa kufanya kosa. Inashauri dhidi ya ugeuzi wa sogo kwa Ujuzi, unaoitwa Knowledge, wa Mungu unaoishi ndani yenu-zaidi ya akili yenyu ya kufikiri na zaidi ya mawazo, dhana na imani ambayo yaliyo tayari imara katika kihistoria cha ubinadamu. Kwa kuwa kuna msingi wa maadili na kanuni ya maisha yenyu. mukieinda kinyume ama mukikataa hiki, mutateseka kwa sababu ya yale yatakayotokea , si kwa sababu Mungu ni anawaadhibu, bali ni nyinyi wenyewe, kwa kuwa mumeigeuka ile Mungu aliweka ndani yenu na kwa sababu, ya ujinga, kiburi, na ubatili, mutakuwa mumejipea mamlaka ya kuenda kinyume au kukataa ile Mungu aliweka ndani yenu.
Kuweni na ufahamu wa hatari kubwa kwako wewe binafsi, kwa watu wenyu, mataifa yenyu na dunia yenyu, kwa sababu wakati wa majaribio na dhiki tayari umetokea. Ubinadamu,viongozi na wananchi wote, wataamua matokeo, kulingana na vile watayajibu majaribio na dhiki yajayo. Nyinyi wenyewe muna uwezo wa uamuzi. Mapenzi ya Mungu yako wazi-Mungu anaandaa ubinadamu kukutana na maisha katika ulimwengu. Hii ni wazi na ni ile iliyotolewa katika Ujumbe Mpya.
Hata hivyo, ili muweze kuvuna thawabu kubwa ya Ujumbe Mpya, ili muweze kujiandaa kwa mustakabali ambao utakaokuwa tofauti na zamani, ili muweze kuepuka balaa na maafa, ni lazima musikize kwa makini. Lazima muwache. Lazima muweze kuzuia hasira yenyu na tamaa yenyu. Lazima muweze kuzuia hukumu yenyu kuhusu wengine. Lazima muweze kuzingatia hekima ya mawazo yenyu na vitendo na matokeo yao ya mustakabili.
Jitayarisheni, kwa sababu nyakati ngumu tayari zinatokea. Ni matokeo ya ujinga wa ubinadamu na unyanyasaji wa dunia. Ni matokeo ya ukosefu wa maono ya ubinadamu na ukosefu wake katika maandalizi ya mustakabali. Itakuwa ni wajibu wa kila taifa na viongozi kuneemesha watu wao cha kutosha katika nyakati zijazo, lakini hii itakuwa ngumu na changamoto zaidi. Matajiri watakuwa na wajibi wa kutunza maskini. Na maskini watakuwa na wajibu wa kutunza wenzao. Ni lazima kuwe na huduma kuu kwa mwanadamu na mawazo zaidi kuhusu mahitaji, furaha, nk ya watu wengine katika hali hii ngumu. Kwa sababu ubinadamu umeiba kutoka kwa dunia kwa kiasi dunia yenyewe itaweza kwa ugumu kuposha familia ya ubinadamu. Hali na mazingira ya maisha yenyu, muwe tajiri au maskini, muishi katika taifa ya utajiri au umaskini, yatawalazimisha muyatekeleze mahitaji haya.
Tambueni kuwa shida hii kubwa imeita Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu katika ulimwengu na Mtume wa Mungu ametumwa ulimwenguni kutoa ujumbe huu, ndio auufanye uwe wazi kwa kuueleza kikamilifu na awe lengo lake la msingi na pia awe mwakilishi wa Ujumbe huu. Musimuhukumu au kumulaani Mtume kwa sababu mutakihakumu na kukilaani kile Mungu alichokiweka ndani yenu. Kwa Maana, ingawa Mtume ni binadamu na hufanya makosa, yeye analeta Ujumbe uliyo zaidi ya uvumbuzi wa ubinadamu na hauna makosa, migogoro, na utata.
Pokeeni Ujumbe huu kutoka kwa Mungu. Yapime maneno yake kulingana dunia unayoiona na dunia unayoijua. Ifikirieni historia ya ubinadamu na vita vyake vikubwa, ushindi wake, na jinsi umekuwa wa uharibifu -kwamba watu wengi walijitoa mhanga ili wachache wanaweza kujitajirisha. Tambueni sasa kwa kuwa hamuwezi kuendelea hivyo katika siku zijazo ama familia nzima ya ubinadamu itaingia katika hali ya upungufu wa kudumu, ama mutajiingiza wenyewe katika mazingira magumu ya matatizo na mashambulizi kutoka kwa vikosi vinavyotoka nje ya dunia, ambayo hata saa hii yana mipango ya kupata faida kwa sababu ya migogoro na ufariki wa ubinadamu.
Kujijua mwenyewe ni kumuhisi Mungu katika maisha yako, na kujua kwamba Mungu aliuweka ujuzi, uitwayo Knowledge, ndani yako ili ukuongoze na ukulinde na utumie mamlaka ndio ukatae uharibifu wako wa kibinafsi na shughuli zako za kibinafsi. Kujijua wewe mwenyewe ni kuijua nini Mungu aliiweka ndani yako, sio kuielewa kielimu, lakini kwa kujua ukweli wake, kuuhisi na kuufuata mwelekeo wake. Wasiwasi, hangaiko na ushindani ukiongezeka duniani, mutahitaji mwongozo huu sasa zaidi kuliko hapo awali. Kwa sababu taasisi na faraja zile zilizowapatia faida zinaweza kuwa hazitapatikana katika siku zijazo. Uhakika na usalama mulizozipata, kwa kiasi chochote kile mulizozipata, zinaweza kuwa hazitapatikana katika siku zijazo. Mutajua aje vile mutakavyokuwa salama? Mutajua aje cha kufanya katika uhangaiko na mabadiliko yakiwakabili? Jibu la Mungu limo ndanu yenyu. Kuwakumbusha hiyo, Mungu ameuleta Ujumbe Mpya katika dunia na amemtuma Mtume wake duniani.
Hamujui ya kutosha ili kutoa shaka kuhusu Ujumbe Mpya ama kujadiliana nayo, maana kufanya hivyo ni kauli ya kiburi, ujinga na ubatili wenyu. Lazima uwaze juu ya Ujumbe Mpya. Lazima umusikilize Mtume ndio uweze kujua, kuona na kuelewa. Kwa sababu, bila majaliwa makubwa ya ujuzi, uitwayo Knowledge, hamuwezi kuwa na uwezo wa kuona, kujua na kuelewa. Tabia yenyu itadhamiriwa na wengine. Na mutafuata hofu badala ya hekima.
Kutokana na hatari kubwa na hatari iliyo mbele, labda munaweza kuanza kuona mwanga ambao umeletwa ulimwenguni wakati Giza Kubwa inayowakabili na inayopata kasi iliyo upeo wa macho.
Ipokee onyo hii kama zawadi ya upendo. Ipokee kama kitulizo cha kuthibitisha kwamba kile munachokihisi ndani yenyu ni ya ukweli, kwamba ubinadamu unakabiliwa na hatari kubwa sasa – hatari ya vita kutoka ndani na kuingiliwa kutoka nje. Kuweni na ujasiri wa kuikabili. Kuweni na uaminifu wa kuitambua. Kuwa na moyo wa kiasi wa kufikiria bila kujaribu kuifanya vile unavyotaka iwe au vile unavyofikiri iko.
Hii ni wajibu wenyu. Hii ni wito wa muda wenyu. Ni wakati wa Ufunuo, na Ufunuo tayari unafunuliwa.
Una hatima ya kukutana na watu fulani katika maishani. Una miadi nao. Wataongozwa kukutana na…
Ujumbe Mpya umo hapa kuagiza ubinadamu na kuhifadhi utamaduni wa binadamu. Ni jibu ya maombi…
Wakati fulani utakuja kutambua kwamba Ufunuo huu Mpya huko hapa ili kukupatia maisha mapya. Hauko…
Mtume yuko dunia. Yeye ameuleta Ujumbe mkubwa kwa binadamu, Ujumbe ambao amekuwa akiupokea kwa zaidi…
Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya, mwelekeo ambao binadamu hajawai kuupitia. Kwa kuwa dunia imebadilika…
Upendo dunia unadhaminiwa sana, kama mnara wa ufarisi wa binadamu. Upendo huimbwa katika nyimbo,…