Upendo Mkubwa

 

Upendo dunia unadhaminiwa sana, kama mnara wa ufarisi wa binadamu. Upendo huimbwa katika nyimbo, huandikwa katika mashairi. Hudhaminiwa katika maandiko makubwa. Huzungumzwa katika mazungumzo ya kawaida. Watu wanadai kuwa wamo katika upendo, kuwa upendo ndiyo ufarisi wa mwisho, kuwa kile mtu anahitaji duniani ni upendo tu na vengine vyote vitakuwa na matokeo mazuri. Lakini watu wachache tu ndio wanaelewa ukweli wa upendo. Na watu wachache tu ndiyo wana ufarisi wa upendo katika eneo ya ndani zaidi – zaidi ya mvuto, zaidi ya ghururi na mahaba. Watu wachache wana ufarisi wa nguvu halisi ya upendo.

Aidha, watu wengi hulinganisha baadhi ya aina ya tabia, imani na mitazamo kama upendo – upole, uwasilisho ni huhusishwa na upendo. Amani na utulivu huhusishwa na upendo. Lakini kwa kweli upendo huu wa ndani zaidi ni nini, sio upendo ambao tu ni mvuto , ama ghururi au mahaba, lakini aina ya upendo wa ndani ambao ni ukombozi, ambao huanza kutoka mahali ya undani ndani ya mtu binafsi.

Na zaidi ya haya, upendo wa Mungu ni nini? Ni ghururi, mvuto au mahaba? Watu wengi watasema hapana, lakini hawajui maana asili ya upendo wa Mungu na jinsi upendo huu unajieleza na jinsi unaweza kutafsiriwa katika dunia kwa ufanisi.

Hivyo leo tunazungumza kuhusu Upendo, upendo mkuu ambao unaishi ndani ya kila mtu na upendo mkuu wa Mungu, ambao ni jumla ya upendo wote Ulimwenguni, na ni chanzo cha upendo wote wa kweli kila mahali – katika dunia hii na katika Jumuiya Kubwa ya ulimwengu. Na hapo tutazungumza kuhusu kile Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu kwa dunia kinafundisha kuhusu upendo, kwa maana kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani, na upendo ni sehemu ya ujumbe wake.

Ni lazima hapa kuanza kwa kusema upendo sio nini. Upendo sio mvuto. Upendo sio ghururi. Upendo sio mahaba. Upendo si romance ambapo unavutiwa au kuchukuliwa na uzuri wa mtu mwingine au baadhi ya nyanja ya utu wake. Sio ibada ya sanamu, ambapo unaidolize mtu, unaabudu mtu, hata Uungu, hata Mtume, hata Mungu. Lakini haya hayawakilishi uhusiano halisi, uhusiano wa mafanikuo, uhusiano wa umoja.

Upendo sio tabia, mtazamo, staili. Sio etiquette. Sio mkataba. Upendo unaweza kujieleza katika njia tofauti – kwa upole au kwa kulazimishwa. Upendo unaweza kuonekana mpole. Upendo unaweza kuonekana imara. Upendo unaweza kuwa changamoto. Upendo unaweza kukukosoa. Upendo unaweza kufichua Illusions zako, fantasies zako na udanganyifu wako binafsi. Upendo sio kile watu humaanisha wakati wanajadiliana kuhusu upendo, katika karibu hali zote.

Upendo ni nguvu zaidi ambayo huongoza watu kufanya mambo ambayo ni tofauti na mawazo yao, imani zao na hisia zao za lazima. Upendo ni kitu kilicho zaidi ya upendo ambao unasikia katika mazungumzo. Kwa kweli, ni bora kuonyesha upendo kuliko kuzungumza kuhusu upendo, kwa kuwa upendo wa kweli huonyeshwa. Ni kile ambacho kinaongoza watu kubadilisha maisha yao, kubadilisha vipaumbele vyao, kwa kushirikiana na kile kilicho ndani zaidi na kubwa zaidi ndani yao. Ni kitu ambacho kina uwezo wa kuenda kinyume cha tamaa ya binadamu, ubinafsi wa binadamu, kero za binadamu na imani zote za mapendeleo na mitazamo, itikadi za kidini.

Kwa kuwa upendo haufungwi na mambo haya. Huzuliwa tu na haya, hurudishwa nyuma au hufichwa na haya. Lakini upendo husonga kwa hiari yake mwenyewe, kwa kuwa inahusishwa na Knowledge ambayo Mungu ameweka ndani ya kila mtu. Kwa kuwa, ulizaliwa na akili mbili – akili ya kufikiri na akili na kujua. Akilin ambayo unafikiri nayo ni bidhaa ya ushawishi wote kutoka jamii yako. Ni bidhaa ya kuwa duniani. Ni mkusanyiko wa mawazo ya vyama, na mwelekeo wa fikra ambazo umejifunza tangu siku uliyozaliwa. Fikra mengi ni muhimu, na baadhi yake ni madhara na hatari kwako. Hakika, umekuwa na ukijifunza jinsi ya kuishi duniani – jinsi ya kuishi kimwili, jinsi ya kuishi kijamii, namna ya kushiriki katika mazingira ya familia, katika utamaduni au labda ndani ya muundo wa kidini. Umekuwa ukijifunza jinsi ya kuwasiliana na mawazo yako na hisia. Umekuwa ukijifunza kile jamii imekuambia ni lazima ujifunze. Kama tulivyosema, baadhi ya haya ni mazuri na muhimu sana na baadhi ya haya ni hatari na hayana maslahi bora kwako.

Lakini ulizaliwa na akili ya ndani, akili ya Knowledge. Akili hii haifikiri kama akili yako ya kimwili inafikiri. Inaona na inajua. Sio ile watu wanadhani wakati wanazungumza kuhusu subconscious. Subconscious huhusishwa na akili yako ya kidunia, au uwekevu. Hii ni akili ya ndani na haiwezi kushawishiwa na dunia. Haifuati mfano au ushawishi wa dunia. Haiogopi au kutishwa na dunia. Akili hii ya ndani zaidi inaitwa Knowledge katika Ujumbe Mpya sababu inahusiana na ufarisi wa moja kwa moja wa kujua, ni ufarisi wa mshikamano, ni ufarisi wa utambuzi wa kweli na ufarisi wa uhusiano wa kweli.

Upendo wa kweli huanza kutoka uwepo wa Knowledge. Kwa asili ni uelezaji wa Knowledge. Wakati Knowledge inakuongoza kufanya jambo lolote – labda kitu kamwe haukuwa na mpango wa kukifanya, kitu ambacho haukielewi, kitu ambacho kinaenda kinyume cha mipango yako na malengo na matarajio. Hili linaonyesha upendo kwa sababu unaonyesha mapenzi ya Mungu, ambayo ni upendo wa Mungu. Kwa kuwa upendo wa Mungu hauko tofauti na nia ya Mungu. Mungu hafikiri kama vile akili yako hufikiri – ina furaha siku moja, na huzuni siku ijayo, inafurahia hiki, na kukasirikia kingine, ina ukatili na inawaadhibu wale waliofanya makosa au ambao wanaishi katika makosa. Hii si Mungu! Hii ni akili ya binadamu inahamisha akili ya binadamu kwa Mungu na kuhamisha kwa Mungu hisia na malalamiko ya binadamu. Haya ni matarajio yote ya akili ya binadamu. Lakini Mungu yumo zaidi ya haya yote. Na upendo na mapenzi ya Mungu yamo zaidi ya haya yote.

Hivyo kama unaishi katika akili ya kibinafsi au kile unakiita “ubapa wa akili,” basi, fikra zako zote kuhusu Mungu zinahusishwa na akili yako ya kibinafsi. Unafikiri kuwa Mungu ni kama utu mkubwa, akili kubwa mno, lakini akili ambayo inaweza kudhibitiwa na hofu na wasiwasi, chuki na mashtaka, hukumu na adhabu, mawazo ya kudumu, haki na uzushi. Huyu ni Mungu ambaye watu wanadhani anafikiri kama hao, anatenda kama hao, ana tabia kama zao.

Lakini ukifikiri Mungu kwa kweli ni nini, basi, Mungu wa Jumuiya Kubwa, Mungu wa maisha yote ya akili katika Ulimwengu, bila shaka Mungu wa Ulimwengu, wa Jumuiya Kubwa, hawezi kushawishiwa na imani za binadamu, mitazamo ya binadamu, hisia za binadamu, mikataba ya jamii ya binadamu na mambo yote ndogo ambayo yanaweka ubinadamu katika hali iliyo primitive na haijaendelea.

Kama Mungu ni Mungu wa Jumuiya Kubwa, basi Mungu ni mwandishi wa aina mingi ya maisha ya kiakili isiyohesabika, ya dunia zisizohesabika ambapo maisha ya kiakili inaishi. Mungu ni mwandishi wa mageuzi. Mungu ni mwandishi na chanzo cha upanuzi wa Ulimwengu. Mungu ni mwandishi wa ukweli wote ya kisayansi. Mungu ni muumba wa jamii zisizohesabika ya viumbe ambavyo havilingani nawe, havifikiri kama unavyofikiri au kuwa na mfumo wa thamani kama wako. Mungu ni mwandishi wa asili, ambayo inafanya kazi ndani ya dunia hii na kwingineko na ndani ya dunia zote katika Ulimwengu na zaidi ya Ulimwengu – katika eneo zote za udhihirisho. Huyu ni Mungu mkubwa sana na anapita mawazo yote ya kiteolojia, mifumo ya dini ya imani, mashirika ya dini. Ni bora kuweka kando mawazo yako kuhusu Mungu na kukifuata kile Mungu ameweka ndani yako ukifuate, na ukione kile Mungu amekiweka ndani yako ukione, ukisikie kile Mungu amekiweka ndani yako ukisikie.

Hapa tu ndipo unaweza kuwa na ufarisi wa Mungu na ufarisi wa uhusiano wako na Mungu, na hatimaye, ukifanikiwa katika kufuatia nguvu na uwepo wa Knowledge ndani yako, utaugundua mapenzi ya Mungu kwako katika maisha haya, katika dunia hii, kwa wakati huu.

Kwa sababu huwezi kuelewa Mungu, ina maana huwezi kuelewa mapenzi ya Mungu. Ina maana huwezi kuelewa upendo wa Mungu. Lakini unaweza kuhisi mambo haya kwa sababu Mungu amekupatia akili ya ndani, akili kubwa zaidi, akili ya Knowledge. Unaweza kubashiri, unaweza theorize, unaweza kuanzisha mifumo ya kufafanua ya mawazo, mifumo ya kufafanua ya akili, lakini kama huwezi kuwa na ufarisi wa harakati ya Knowledge katika maisha yako, hekima ya Knowledge katika maisha yako, ambayo inatoa shauri wakati wote – shauri ambayo huwezi kusikia, shauri ambayo hujibu kwa sababu mawazo yako yapo katika ubapa, katika akili yako ya kibinafsi na katika mtazamo wako wa dunia. Kama huwezi kuhisi harakati hii kwa undani, basi, Mungu ni wazo la kigeni kwako. Mungu ni wazo ambalo unaweza kukubali au kuweka kando.

Mungu ameweka uelezaji wa mapenzi ya Mungu na upendo ndani yako, zaidi ya eneo la ubapa, zaidi ya eneo la akili, mapenzi na upendo ambao huwezi kuidhibiti, huwezi kuitawala, huwezi kuitumia kupata utajiri, nguvu au ushawishi. Unaweza tu kuwasilisha nayo. Unaweza tu kuifuata na kujifunza kuihusu na kufanya kile ambacho kinakupa ukifanye ili uweze kuanzisha upya maisha yako, kujenga upya mawazo yako, kujenga afya yako, kubadilisha maisha yako, kuanzisha tena seti kubwa ya vipaumbele vyako na pamoja nazo nafasi kubwa zaidi katika mahusiano na wengine.

Ni upendo huu mkuu ambao umo mbali zaidi na tofauti na upendo unaousikia katika mazungumzo. Watu wanasema, “Ninakipenda hiki. Ninamupenda yule. Ninapenda chakula hii. Ninapapenda mahali hapa. Ninayapenda mavazi yako. Ninapenda asili. Ninapenda miti. Ninapenda bahari.”

Upendo wa kweli uko zaidi ya haya yote. Upendo wa kweli ambao unakuongoza ujitolee katika huduma, ambayo inabadilisha maisha yako, ambayo inakuambia kuwa uko katika upotovu, inakuambia ukweli kuwa maisha yako imekuwa ufujaji na unajaribu kuchukua mwelekeo ambao sio mwelekeo wa kweli, hii ni upendo!

Upendo ambao unaendelea kukuongoza katika dhamira yako kubwa ya kukuja duniani bila kujali mipango yako na malengo yako, upendo ambao haubadiliki, upendo ambao hauendani na matakwa yako, hii ni upendo!

Mara kwa mara, inaleta changamoto, na unaona kuwa unashindwa na huwezi tena. Na mara kwa mara, inafaraja na inatuliza, na unaikaribisha na kuwa na furaha ipo, kuwa ni ya kweli.

Huu ndio Upendo Mkuu – upendo wa Mungu na upendo wa Mungu uliowekwa ndani yako, kwa Knowledge ndani yako, katika akili yako ya ndani. Akili hii ya ndani iko hapa kwa misioni. Iko hapa kwa dhamira, kwa maana umekuja duniani kwa kutimiza misioni, kwa dhamira, kufanya mambo maalum na watu maalum. Na Knowledge ndani yako inajaribu kukuongoza ufike hapo, kukuongoza katika mwelekeo sahihi ndio uweze kufika pointi ya mihadi yako na wale ambao una dhamira ya kukutana nao na kupata hali na mazingira ambapo dhamira yako kubwa zaidi inaweza kujitokeza, inaweza kuwa activated. Wakati watu bado wanafanya mipango yao na kuimarisha kile wanakifanya na kile wanaamini, Knowledge ndani yao inajaribu kuwaongoza mahali fulani.

Kwa hivyo, kamwe usifikiri kuwa watu daima wako mahali wanafaa kuwa, wanafanya kile wanafaa kukifanya. Hio sio ukweli. Hio ni kisingizio tu. Ni aina ya njia ambayo watu husema ili mambo yawe sawa, ili kufanya mambo yote yawe haki, lakini kwa kweli, maisha yao yamo katika upotovu. Hawapo mahali wanahitaji kuwa. Wanafanya kazi katika eneo ambayo haiwakilishi dhamira yao kubwa zaidi ya kukuja duniani, au wamefungwa na umaskini au ukandamizaji wa kisiasa, au wamefungwa katika nafasi yao na hawawezi kupata njia nyingine.

Lakini upendo wa Mungu bado unaishi ndani yao. Kamwe upendo huu hautakata tamaa. Upendo huu sio kama akili yako ya kufikiri, ambayo haina msimamo katika tamaa yake, imani yake inayoshinda ikibadilika na vivivnyovinyo vyake, katika mawazo yake ya pinduani, ukali wake. Kitu pekee kwa kweli ni kile cha msingi ndani yako ni Knowledge kwa sababu hicho ndicho kitu pekee ambacho kitadumu. Na Knowledge hii haijafungwa na itikadi za kidini au kwa mapendeleo ya taifa. Haiwezi kutumika kama silaha. Haiwezi kutumika kuonea wengine. Haiwezi kutumika kwa kugawanya na kushinda wengine. Knowledge inaweza tu kufuatwa. Haiwezi kutumika. Akili lazima itumikie Roho. Sio kwa njia nyingine.

Watu wanataka Mungu afanye mambo mengi kwa maisha yao, kama Mungu ni mtumishi wao. Watu wanataka Mungu awalinde kutoka hatari au janga. Wanataka Mungu awapatie kile wanachotaka, kama Mungu ni aina ya, ni kama mtumishi. Hii ni akili inataka Roho itumikie akili. Akili inataka Mungu aitumike na aiimarishe. Huu sio mpango halisi. Hii ni kichwa chini. Kwa kweli, mwili wako unafaa kutumikia akili, na akili yako inafaa kumtumikia Roho, au Knowledge. Na Knowlegde hapa inatumikia Mungu. Huu ndio uongozi wa kweli wa kiumbe chako. Huu ndio mpangilio peke yake ambapo uadilifu wako unaweza kuwa na ufarisi na kuwa imara, ambapo unaweza kupata umoja ndani yako mwenyewe.

Hatimaye hapa, kila kitu ni mtumishi wa Mungu kwa sababu kama mwili ni mtumishi wa akili, na akili ni mtumishi wa Roho, na Roho ni mtumishi wa Mungu, basi, kila kitu ni mtumishi wa Mungu. Lakini ili kupata uadilifu, ili kupata maelewano ya ndani, muungano huu wa masuala yote ya maisha yako, inahitaji maandalizi makubwa – maandalizi ambayo huwezi kuyaumba mwenyewe, maandalizi ambayo si aina fulani ya mfumo wa mchanganisho ambapo unachukua kile unakipenda kutoka mila hii na kile unakipenda kutoka ingine alafu unayaunganisha, kulingana na mapendekezo yako. Hii ni kutumia Roho kuimarisha akili. Hii siyo sahihi kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Knowledge itakuongoza pale ambapo hungeweza kujipeleka mwenyewe. Knowledge itakuongoza kutoka kwa hofu yako na mapendekezo yako kwa sababu mapendekezo yote yanatokana na hofu – hofu ya kukosa, hofu ya kuwa na makosa, hofu ya kupoteza, hofu ya kifo.

Katika dunia hii, kuna mengi ambayo yamekamilika katika dini na katika kiroho. Kama unaweza kuelewa mageuzi ya maisha katika dunia zengine, basi utaona kiasi ambacho ubinadamu umeendelea, licha ya makosa yake mengi. Ungeona kuwa dini katika dunia hii kwa kweli imeendelea sana. Ungeona kuwa mataifa mengi yalioendelea kiteknolojia yamewacha dini zao zote, uelewa wao wote wa kiroho. Wamekuwa kama mitambo, kama mashine, kulingana na mawazo yao, kulingana na sayansi yao, kulingana na dikteta ya kisiasa na muundo wa kijamii.

Musidhani kuwa dini katika dunia hii ni kosa kubwa. Kwa kweli ni dini pekee yake ambayo binadamu anaweza kuchangia katika Jumuiya Kubwa kwa hatua hii. Kile ambacho kimekuwa na mafanikio katika suala la uhuru wa mtu binafsi na ufahamu wa kiroho kwa kweli ni kizuri sana kulingana na nafasi ya binadamu katika ulimwengu kwa ujumla. Na huu ni uelewa muhimu kwa sababu mustakabali wa binadamu utakuwa katika Jumuiya Kubwa, na kama mutabaki kama taifa iliyo huru na inayojitegemea itaamuliwa na mahusiano yenyu katika Jumuiya Kubwa.

Upendo ni nini? Upendo ni harakati ya Knowledge. Au ikisemwa kwa maneno mengine, upendo ni mapenzi ya Mungu yanayojieleza yenyewe kukupitia. Hapa upendo unahusishwa na inspiration, ambapo akili inaunganishwa na Roho, ambapo akili inatumikia Roho, ambapo akili inaongozwa na Roho. Wakati mwingine hii hufanyika mara moja yenyewe. Wakati mwingine hutokea wakati umekata tamaa sana, na unahisi kitu ndani yako ambacho inatoa matumaini wakati unajisikia kuwa unakata tamaa.

Lakini kupata faida ya Knowledge, kuchukua hatua kwa Knowledge, inahitaji mbinu inayotekelezwa kwa makini. Na mbinu hii inatakiwa itolewe na Mungu kwa sababu Mungu tu ndiye anajua jinsi ya kuunganisha tena mawazo yako na akili kubwa ya Knowledge ndani yako.

Kuna mengi ambayo akili yako inafaa kufanya na kuzingatia, na hata ujuzi wake mkubwa haujakuzwa kikamilifu ndani ya watu, lakini katika suala hili, lazima upokee neema ya Mungu, ambayo ni upendo wa Mungu. Maisha yako imepotea. Hujijui mwenyewe au kile unachokifanya na hatimaye unakuja katika pointi ya kukata tamaa ambapo unatambua kuwa huu ni ukweli wa hali yako na hali hii daima ilikuwa hali yako. Na Mungu anakutumia Hatua kwa Knowledge. Unaweza kutaka Mungu akupe kazi mpya, uhusiano mpya, mwili nzuri, au Mungu ayaondoe matatizo yako. Haya ndio yale watu wanataka Mungu awafanyie. Mungu anatuma kile kitawakomboa, sio kile wanachokitaka. Kile wanachokitaka kitaendeleza tu hali yao, utenganisho wao, kitazuia watu kuweza kupata fursa ya kupata Knowledge. Kwa hivyo Mungu kwa upendo wa Mungu anakitoa kile kinachohitajika kwa ukombozi.

Ni wakati tu unatambua kuwa kukipata kile unachokitaka haitatoa tofauti kwa maisha yako ndio utarejea Knowledge. Ni wakati itakapokuwa dhahiri kuwa mipango yako ya kujitimiza duniani ni dhaifu na hayatatimiza matarajio yako ndio utarejea kwa Knowledge. Hapa disappointment kubwa ni muhimu sana na inamiliki nafasi kubwa kwako. Lakini dissapointment ndio kila mtu anataka kuepuka, kwa hivyo watu wanaendelea kujaribu kupanga na kuzingatia maisha yao ili kwa wapate wanachotaka. Tatizo lao linazidi tu. Knowledge inawashauri, lakini hawawezi kusikia. Hawako wazi ndio waweze kupoea Knowledge. Wanakitaka kile wanachokitaka. Wanaendeshwa na hofu na upendeleo wao. Na hivyo hawaujui upendo.

Upendo ndio unawapatia wanachokitaka. Upendo ni kitu ambacho kinaonekana ni kizuri. Upendo ni kile ambacho wanachohisi kuwa ni kizuri katika wakati huu. Na matokeo yake ni, dhana ya watu kuhusu upendo inakuwa chanzo cha addictions zao. Na upendo unakuwa aina ya dawa la kulevya. Lazima uwe na mtu huyu. Lazima uishi katika eneo hili. Lazima uwe na chakula hiki. Lazima uwe na radhi hii. Lazima uwe na madawa haya ya kulevya.

Upendo wa Mungu ni harakati ya Knowledge ndani yeko, kwa sababu harakati hii inakuongoza kwa ukombozi wako na utimizo wako duniani. Kupata ukombozi na utimozo huu, ni lazima uwe huru kutokana na mahusiano na majukumu yanayokufunga katika maisha yako. Ukombozi si kitu tu ambayo unaongeza juu ya maisha yako, Sio kitu kingine ambacho unasimamia katika maisha yako. Si tu kitu cha kuongeza. Ni maisha yako. Kila kitu ambacho Knowledge inakuongoza ukifanye, kama inakuongoza kuepuka kitu au kukuongoza ukifuate kitu, yote yana lengo la kukuongoza kwa ukombozi wako. Na ukombozi wako una maanisha kuwa umelinganisha akili yako ya kufikiri na Knowledge, huu ndio ukombozi. Huu ndio mwanzo wa ahadi ya kweli kwako. Hukombolewi kwa Mungu. Hujawahi kutengwa na Mungu. Mungu hajakukasirikia. Umejiweka mwenyewe katika uhamishoni. Umeingia katika mazingira ambapo Mungu hajulikani, ambapo Mungu amesahaulika, ambapo Mungu ni ibada ya sanamu, imani na kiibada. Kile kinachokukomboa ni kuchukua hatua kwa Knowledge, kuunganisha akili na Roho, akili ya kufikiri na nguvu halisi ya Knowledge ndani yako – siyo na imani yako kuhusu Roho au kiroho au dini, lakini na ukweli.

Watu wengi hawawezi kutofautisha kati ya imani yao na hali iliyo halisi. Wanafikiri kuwa imani yao ni ukweli. Wanasema, „Kile ninachoamini ndio cha kweli.“ Wanasema , „Kile ninachoamini ndio ukweli.“ Wanasem, „Kile ninachoamini ndio mapenzi ya Mungu.“ Na bado vile wanazidi kuyazingatia mawazo yao inaonyesha kuwa bado hawajashikamana na Knowledge. Bado hawajaokolewa.

Akili lazima itumikie kile Mungu amekiweka ndani yako. Kile Mungu amekiweka ndani yako ni mapenzi na mpango wa Mungu kwa maisha yako, ambayo inashikamana na mapenzi na mpango wa Mungu kwa maisha yote ndani ya dunia hii, nje ya dunia hii, katika Jumuiya Kubwa ya dunia zote ulimwenguni ambapo unaishi. Kubwa sana! Baada ya kuuona ukubwa wake, utatambua kuwa mawazo yako kamwe hayataweza kuyaelewa na kuyafafanua. Lakini Knowledge inalingana na kila kitu. Iko katika maelewano na Knowledge ndani ya wengine. Na kuwa Knowledge ndio mpatanishi mkubwa duniani. Amani yoyote ya kweli ambayo imekuzwa na kuanzisha imetokana na Knowledge. Vinginevyo, makubaliano ya amani ni mipango ya kiuchumi au kisiasa ya kuzuia vita na migogoro. Hakuna amani hapa imeanzishwa. Amani ni matokeo ya watu kutambuana na kuwasiliana, si tu biashara ya mipaka, si tu kuangaliana kwa mbali, lakini kujifunza kutambua na kuwasiliana na kuhusiana pamoja.

Idadi ya watu duniani ikizidi kuongezeka, muna fursa kubwa ya kuanzisha umoja wa binadamu, umuhimu mkubwa wa kuanzisha umoja wa binadamu. Katika dunia ya rasilimali ambazo zinapungua, idadi hii ya watu ambao wanaoongezeka lazima iungana kimarisha uwezo wake wa kuishi. Hali halisi ya uhaba ambayo munaijenga inaleta msukumo mkubwa wa umoja wa binadamu. Hii ni kazi ya Knowledge.

Mungu hataki ubinadamu uishi katika dunia ambayo ina idadi ya watu wengi, dunia ya rasilimali zinazopunguka. Lakini Knowledge itaendelea kuongoza watu kwa ukombozi wao bila kujali hali ya dunia! Hata kama mutajenga mazingira ya ndoto mbaya katika dunia, Knowledge ndani yenyu na wengine itawaongoza katika ukombozi. Mungu basi sio mwandishi wa yale unayoyafikiri na unayoyafanya. Mungu ni mwandishi wa ukombozi wako. Mungu ndiye chanzo cha dhamira kubwa zaidi ambayo imekuleta na kila mtu duniani. Na yule ambaye ataweza kupata Kumbukumbu ya Kale atafarisi nguvu na mamlaka ya Mungu. Na yule ambaye anaweza kuchukua Hatua kwa Knowledge na kuleta Knowledge katika ufahamu wake atakuwa na ufarisi wa upendo wa Mungu.

Upendo ni kama hewa unayopumua. Hauidhamini. Kamwe hauiwazi. Lakini unaihitaji kila wakati. Upendo ni kama hewa. Unaweza kufarisi? Knowledge iko ndani yako. Imetulia. Inatoa ushauri. Unaweza kuihisi? Unaweza kuisikia? Uko tayari kwenda kwake kwa mikono iliyo wazi, bila madai, bila imani, kuenda kwake tu? „Ninaenda kwa Mungu.“ Enda kwa Mungu. „Nia ya Mungu kwangu ni nini? Nifanye nini katika hali hili? Ninafaa kuwa na mtu huyu? Ndiyo au hapana? Ninafaa kuenda mahali hapa? Ndiyo au hapana? Ninafaa kushiriki katika shughuli hili? Ndiyo au Hapana? “

Kila kitu ni rahisi. Hakuna mikataba. Hakuna maafikiano. “Naam, nitafanya kitu kudogo kuhusu haya kama Mungu anatoa kitu kidogo kwangu. Nitafanya mpango na Mungu. ” Hakuna mikataba. Utafuata uongozi ama hautaufuata. Uko tayari kukishuku kile unajitakia, au hauko tayari. Hii haimaanishi kuwa unajisalimisha kwa Mungu. Hii itatokea labda baadaye. Huu ni ufunguzi mdogo, utayari mdogo, mwanzo. Unaanza kama mwanagenzi. Huwezi tu kuruka katika hali ya kukomaa katika uhusiano wako na Mungu. Lazima uchukue hatua. Na Mungu ndiye anatoa hatua.

Upendo ni harakati ya Knowledge ndani yako. Knowledge ni akili ya ndani ile Mungu ameweka ndani yako, ikuongoze, ikulinde na ikuongoze kwa ugunduzi wa dhamira yako kubwa katika dunia hii kwa wakati huu. Kitu kiingine kinachojiiita upendo ni uonyesho tu. Haina staamani ndani yake. Haina hekima ndani yake. Na haina dutu. Maisha haitaitekeleza. Hii ndio maana watu huwa katika upendo, wanaanza uhusiano, na kisha wanajua katika uhusiano kama wanaweza hata kuwa katika uhusiano, na kwa mara nyingi hawawezi kuwa katika uhusiano. Kwa hivyo upendo uko wapi hapa? Upendo ni nini hapa? Ghururi ya awali? Mvuto wa kitu ambacho unafikiri kitakuokoa au kufanya uwe kile unataka kuwa?

Watu huzeeka. Wanapoteza uzuri wao wa kimwili. Wanapoteza mvuto wao. Maishani wanakabiliana na matatizo na mahitaji. Lazima wazalishe. Lazima wafanye kazi. Lazima wakabiliane na shida. Ni nini kilichotokea kwa upendo wao ule huko mwanzoni ulikuwa wa furaha na ajabu? Basi kile watu walidhani kuwa ni mapenzi inakuwa aina ya mkataba wa kuishi au ustaarabu.

Kuna upendo mkubwa. Kuna Upendo Mkuu, upendo ambao Mungu ameuweka ndani yako, ndani ya kila mtu, unaosubiri kugunduliwa, unaosubiri kuonyeshwa na ufarisi. Upendo huu hauna njia moja tu ya kujieleza. Haihusiani na aina fulani ya tabia au etiquette. Sio mkataba wa kijamii. Upendo huu utakuvuta mbali na hatari. Upendo huu utatoa changamoto kwa mawazo yako na mtazamo wako. Upendo huu utakuonyesha kuwa maisha yako haiendi popote. Upendo huu utakuongoza uelekee njia moja wakati unataka kupitia njia nyingine. Upendo huu utakuzuia. Upendo huu utakuelekeza upya. Huu ni Upendo Mkuu. Hiki ni kitu halisi! Hata kama uko peke yako maishani, kama unaweza kuhisi harakati ya Knowledge, utahisi upendo wa Mungu. Hutaielewa. Hutakuwa na hakia mahali ambapo utakuongoza. Hutakua na uhakika kuhusu maana yake. Lakini kama utaifuata, basi utakuwa na ufarisi wake. Na hatua kwa hatua, na nyongeza kwa nyongeza, itaongoza maisha yako katika nafasi tofauti na kufungua fursa kubwa kwako.

Hapa lazima ufanye mazoezi ya uvumilivu na forbearance. Lazima uahirisha hukumu na uchelewesha mahitaji yako ya kuwa na hitimisho kwa sababu unahitaji kupokea kutoka kwa Mungu. Kabla uweze kutoa kile ambacho Mungu amekupa utoe, lazima upokee kutoka kwa Mungu. Lazima basi Mungu aikomboe maisha yako.

Baadhi ya watu wanadhani kwamba kukombolewa ni kuchukua mfumo wa imani: „Nimekombolewa kwa sababu sasa ninaamini“ Lakini huu sio ukombozi. Imani ni dhaifu na inakosa uhakika. Daima lazima ishinikizwe. Haina nguvu ya Knowledge. Ni uvumbuzi wa binadamu! Ni lazima Uwe na imani kwa Knowledge ndani yako, lakini hata hapa unatambua kuwa Knowledge ni kubwa kuliko ufahamu wako. Na pale ambapo Knowledge inakuongoza ni mbali na ufahamu wako wa sasa.

Kama unaweza kufuata, unaweza kupata. Kama unaweza kupata, unaweza kutimiza. Kama unaweza kutimiza, unaweza kueleza.

Huu ndio Upendo Mkuu. Na haja ya Upendo huu Mkuu ni mkubwa. Angalia dunia inayokuzunguka. Kuna watu wengi. Kuna shida mingi. Kuna hatari mingi, na hatari kubwa ya kutishia katika upeo wa macho. Upendo Mkuu uko wapi? Katika maisha yako yote, kwa kazi na shughuli zako, preoccupations zako na wasiwasi, malalamiko yako, mivuto yako, Upendo Mkuu uko wapi? Upendo Mkuu ambao unakusisimua na unakuongoza na unakujumuisha? Huu ndio lazima uupokee, ni upendo wa Mungu, ambao ni harakati ya Knowledge. Hivi ndivyo Mungu atakukomboa. Umekuwa ukijaribu kujikomboa, lakini hivi ndivyo Mungu atakukomboa.

Unachukua kila kitu unachokifanya maishani, na kujiuliza, „Kimsingi, hiki ni kile ambacho ninahitaji kukifanya?“ Katika mahusiano yote, „Je, uhusiano huu unanisaidia? Je, ni muhimu kwangu wakati huu ?“ Kila kitu! Na utakuwa na maana zaidi ya hayo itakayotoka kwa Knowledge, ndani yako kabisa. Labda itakuwa hisia. Labda itakuwa picha. Pengine jibu litakuja wiki moja kutoka sasa. Lazima uendelee kuuliza na kusikiliza. Unaomba Upendo Mkuu ukukomboe, ukuungane, na ukuweke katika nafasi ambapo zawadi zako kubwa zinaweza kufikiwa na kuchangiwa duniani. Na hii inahitaji uwe katika baadhi ya mazingira fulani, uwe katika mahusiano na baadhi ya watu fulani, katika mazingira fulani. Kama hauko katika mazingira fulani na watu fulani, basi, ugunduzi hautatokea. Pale ambapo uko kimwili ni muhimu sana katika suala hili. Wale ambao unahusiana nao ni muhimu sana katika suala hili.

Kama utambuzi wako utatokea katika mji fulani kuhusu baadhi ya watu fulani walio pale na hauko katika mji huo, basi, ugunduzi utafanyika aje? Hata kama uko katika mahali sahihi, utaweza aje kuwapata watu halisi ambao una dhamira ya kutimiza pamoja nao? Huwezi kujua. Hii ni kubwa mno kwa akili. Ni Knowledge peke yake ambayo inaweza kukuongoza uende huko. Knowledge inaweza kuleta watu wawili kutoka sehemu za kinyume za dunia kwa kutimiza dhamira kubwa zaidi. Hiyo ni nguvu ya Upendo Mkuu. Na Upendo Mkuu ndio ambao dunia inahitaji sasa.